Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
King Savi nimepata dalali wa kunipeleka shamba Ruaha, je nyanya ya eneo hili ikoje?Nina experience kidogo kwa kutokea makambako
1.Fika makambako eneo linaitwa soko la nyanya hapo, utapata nyanya kutokana na uhitaji wako, yaani Kuna wamama hapo watakutafutia nyanya na watakutafutia vijana wa kupanga kwenye box (mtakubaliana bei ya kukaba nyanya)
2. Being ya box empty la nyanya Ni 1200-1500
3.Kamba + karatasi inategemea na box za nyanya ila karatasi moja Ni tsh 150-200, Rola ya kamba Ni Tsh 12,000/=
4.Usafiri utapata hapohapo sokoni Kuna jamaa anaitwa Mwenye Akili Nick name maarufu sana hapo sokoni, Jamaa wako vizuri sana Kuhusu usafiri pia wanamadalali wao masoko ya Dar, kwahiyo unaweza kupakia mzigo kwao halafu wakakuuzia kutokana na bei ya sokoni Dar. Bei ya usafiri sikumbuki vizuri ila inacheza kwenye 1,800-2,500 kwa box.
Wish you the best, karibu kwa maswali zaidi.
King Savi nimepata dalali wa kunipeleka shamba Ruaha, je nyanya ya eneo hili ikoje?