Mwongozo wa Namna ya Kuanzisha na Kuendesha Biashara ya Mini Supermarket

Mwongozo wa Namna ya Kuanzisha na Kuendesha Biashara ya Mini Supermarket

Nimepata chumba maeneo mazuri sana sio kikubwa sana ila kinafaha sana kwa biashara hiyo sbb kuna watu wengi sana wanapita, hivyo naomba sana kupata ushauri wenu na shm za kununua vifaa jamani, Nisaidieni maisha ya ajira nimehangaika nimechoka nimefanya intrview sipati nimeamua kuingia kwa biashara ss hv. Nishauri kwenye hii biashara.
 
Najuwa kuna watu wanfahamu na uzoefu wa hii biashara kwa hiyo ushauri wa kiutendaji na maangalizo wanaweza kunishauri. Wewe kwa fikira zako unafikiri ushauri ni wajambo gani la kufaya tu? Mambo ni mengi kwenye biashara ndg yangu.
 
najuwa kuna watu wanfahamu na uzoefu wa hii biashara kwa hiyo ushauri wa kiutendaji na maangalizo wanaweza kunishauri.ww kwa fikira zako unafikiri ushauri ni wajambo gani la kufaya tu?mambo ni mengi kwenye biashara ndg yangu

Wanan

Kwanza kabisa, biashara hii itahitaji u-dedicate muda wako full time in a working day, hivyo kuwa tayari kwa hilo.

watu wengi labda ni Tanzania kwa uelewa wao wanadhani supermarkets ni kwa ajili ya matajiri na watu wenye kipato kikubwa. Jibu ni hapana. Hivyo basi ujitahidi kuweka bei za vitu ambazo kila mteja atazimudu tena ikiwezekana ziwe pungufu kidogo profit margin iwe ndogo lakini sales ziwe kubwa. Hakikisha measurement za bidhaa kama uzito na ujazo (kg,gm,mls, liters etc) vipo intact yaani havichakachuliwi Pia epuka close to expiry products. Ni hatari na hasara

all the best
 
Changamoto ya kwanza jiandae kutupa bidhaa zilizoharibika. Kabla ya faida.
 
Nashukuru kwa ushauri mdizi na chabo hayo yote nitayafanyia kazi. Swala la bei nitalizingatia vilivyo.
 
MAMBO YA MUHIMU KUZINGATIA

Kwanza nakupa hongera kwa kuwa na mawazo ya kujiajiri. Entrepreneurs walio wengi waliaanza pale ambapo jambo fulani halikwenda sawa mathani ajira.

Naomba kuwakilisha mchango wangu mdogo wa mawazo.

1. Super market ni sehemu ambayo inaruhusu kuuza bidhaa mbalimbali. Wengi hudhani ni sehemu ya mboga tu, kumbe waweza weka kila kitu. Kwakuwa space ni ndogo na ni mwanzo weka mboga kidogo sana ili usipate loss ya rotten stuff.

2. Wasiliana na bakeries, chagua moja uingie nayo mkataba iwe inaleta mikate unawauzia na una wacharge commission. Commission yaweza hata kuwa kwenye bei, yaani wakupe discouted price. Pia wawe wanachukua mikate ambayo haijauzwa ili hasara wewe usiwemo.

3. Import juice za pact toka South Africa au penginepo. Hapa Canada kuna super market inauza box moja la apple juice lenye chupa 6 za plastic Lita 1.5 kwa dola 10 tu box zima. Hivyo nadhani SA itakuwa cheaper zaidi.

4. Tafuta wanao supply uyoga, ingia nao makubaliano walete uyoga uwauzie. Nao pia wacharge commission

5. Wauzaji wa mayai pia walete uwauzie

6. Nunua na kuuza mchele safi sana na kwa bei nzuri

7. Tafuta mtu mwenye kuuza simu, mpe sehemu ndogo yaani space auze bidhaa yake na alipie kidogo kodi ya pango.

8. Baadae wekeza pesa kwenye cameras kwa ajili ya shop-lifters yaani wadokozi.

Waweza fanya mengi na kwa bajeti ndogo, hivyo zidi tafakari
 
kama upo tayari hongera sana kwa hilo ila kwa mini super market siyo mbaya lkn ushauri wangu kwako kwa kuanza iweke kwa mtindo wa duka hivyo basi mambo yakichanganya utaweka full hiyo idea yako. Na upataji wa biidha si kila ki2 unanunua vitu vingine unachukua kwa mali kauli km mchangiaji wa hapo juu alivokushauri. plz mwanzo mgumu usikate tamaa kwa sasa wewe jilipue whatever happen God knows!
 
Jaman JF kuna vipaji vingi sana nawashukuru kwa ushauri natawapatia matokeo, na wengi wanaweza kunishauri ndgugu zangu nawaombeni.

Ahsante sana
 
Pia chukua deep freezer uwe unaweka kuku. Tuwasiliane mie nitakusupply kuku kwa credit utalipa baada ya kuuza. Tutaanza na idadi kidogo lakini kadri uaminifu utakavyozidi kujionesha itakuwa full kujiachia. It can only be business if both stakeholders make profit out of it. Njoo tufukuze umaskini.
 
Waungwana nisaidieni nina kamtaji kadogo nataka nifungue biashara ya mini supermarket preferably maeneo ya tegeta au bunju, naomba ushauri kwa wenye uzoefu

ahsanet sana
 
Wadau,

Nina kama milioni kumi hv, nataka kufanya biashara na biashara ninayoiwaza kwa sasa ni mini supermarket, mimi ni graduate nimetafuta kazi mpaka nimechoka lkn sasa nimepata mchongo na kupata milioni kumi na nataka kufungua hii biashara April mwaka huu. Tafadhali wadau naomba kujua A B C za hii biashara na challenges zake. Hii itakuwa ndo ajira yangu ya kudumu nipo maeneo ya Dar es Salaam.

Natanguliza shukrani.
 
Tafuta eneo zuri kisha uanze kuweka vitu vile muhimu kwa matumizi ya ulazima wa binadamu. Na utafanikiwa.

Inalipa hiyo
 
Ni kweli duka la vifaa vya umeme linalipa,tafuta eneo zuri na ikiwezekana kwenye iyo pesa toa angalau mil.2 ununue kiwanja kama asset yako endapo biashara itabuma au utahitaji kuongeza mtaji itakusaidia kupata mikopo kwenye mabank kwa namna moja au nyingine. Take a note on this.
 
Mkuu hardware pia ni moja ya biashara ambayo naiona ni very booming. Thanx for your advice.

Fungua hardware mkuu. Hutajuta. Return ni kubwa na in short time.

Sent from my Nokia Lumia using Tapatalk
 
Ina disadvantages nyingi don't do it. Kwani inatakiwa ufanye visibility studies, vya kuweka ni food products, drinks ambavyo utakuwa unamwaga kwa expire dates ni kazi ngumu mkuu kwa hapa labda hardware ingawa mtaji ni mdogo sana
 
Ukishafungua nitaomba kuwa mmoja kati ya suppliers wako.
 
Back
Top Bottom