MAMBO YA MUHIMU KUZINGATIA
Kwanza nakupa hongera kwa kuwa na mawazo ya kujiajiri. Entrepreneurs walio wengi waliaanza pale ambapo jambo fulani halikwenda sawa mathani ajira.
Naomba kuwakilisha mchango wangu mdogo wa mawazo.
1. Super market ni sehemu ambayo inaruhusu kuuza bidhaa mbalimbali. Wengi hudhani ni sehemu ya mboga tu, kumbe waweza weka kila kitu. Kwakuwa space ni ndogo na ni mwanzo weka mboga kidogo sana ili usipate loss ya rotten stuff.
2. Wasiliana na bakeries, chagua moja uingie nayo mkataba iwe inaleta mikate unawauzia na una wacharge commission. Commission yaweza hata kuwa kwenye bei, yaani wakupe discouted price. Pia wawe wanachukua mikate ambayo haijauzwa ili hasara wewe usiwemo.
3. Import juice za pact toka South Africa au penginepo. Hapa Canada kuna super market inauza box moja la apple juice lenye chupa 6 za plastic
Lita 1.5 kwa dola 10 tu box zima. Hivyo nadhani SA itakuwa cheaper zaidi.
4. Tafuta wanao supply uyoga, ingia nao makubaliano walete uyoga uwauzie. Nao pia wacharge commission
5. Wauzaji wa mayai pia walete uwauzie
6. Nunua na kuuza mchele safi sana na kwa bei nzuri
7. Tafuta mtu mwenye kuuza simu, mpe sehemu ndogo yaani space auze bidhaa yake na alipie kidogo kodi ya pango.
8. Baadae wekeza pesa kwenye cameras kwa ajili ya shop-lifters yaani wadokozi.
Waweza fanya mengi na kwa bajeti ndogo, hivyo zidi tafakari