Nimekua mfugaji kwa miaka miwili katika ufugaji wa bloirel na kienyeji asili
Bloirer 500 kienyeji nimefikisha 150 hao ni kuchi na kawaida.
CHANGAMOTO ZAU UFUGAJI KIENYEJI
1.Wanatumia muda mrefu kupata faida
Yaani unakaa na kuku hadi wanakuzoea
2.Magonjwa mengi na hivyo kupelekea vifo vingi
3. Upotevu mimi huwa nawafungia na kuwapa chakula ndani ya senyenge lakini wapi huwa wanaruka na kutoka nje. Na haswa vifaranga na kuku wakubwa. Chakula chao nachanganya zile pumba laini za dona na concentrator na funza nawatengenezea.
Hapa nimeshindwa pata ufumbuzi
CHANGAMOTO ZA BLOIRER
1. Uangalizi wa hali ya juu kwamuda mfupi.
2. Ukikosea kuwapa chanjo au dawa vifo ni vingi mno
3. Wanahitaji gharama kidogo kuwafuga. Hivyo bajeti yake isiingiliane na bajet yeyote ile kwenye familia vinginevyo hasara njenje.
FAIDA ZA KUKU WA KIENYEJI
1.Ukowauza kwa wingi unapata faida kubwa
2. Kuongeza afya na ni watam kwa mchemsho
3. Watazaliana kwa wingi hivyo utapata faida ya muda mrefu kwa kuuza mayai,nyama,vifaranga kama utatotolesha utauza tu.
FAIDA ZA BLOIRER
1. Faid chapchap kila baada ya miezi 4 unauza
2. Faida ya haraka kwa muda mfupi vice versa is true.
KARIBUNI WANANZENGO TUJADILI CHANGAMOTO ZA UFUGAJI NYAKATI HIZI NA TUELIMISHANE