Mwongozo wa Ushiriki kwenye Mijadala katika JamiiForums

Mwongozo wa Ushiriki kwenye Mijadala katika JamiiForums

Status
Not open for further replies.
Mkuu Maxence Melo tumekuelewa sana.

Ila kuna wakati wahariri huwa wanaondoa maudhui ambayo yapo kinyume na mtazamo wao na sio sheria na kanuni za JF
 
Mkuu Maxence Melo tumekuelewa sana.

Ila kuna wakati wahariri huwa wanaondoa maudhui ambayo yapo kinyume na mtazamo wao na sio sheria na kanuni za JF
Unayo haki ya kuhoji. Tumeweka jukwaa maalum la kulalamikia vitendo hivyo au unaweza kutumia Contact us endapo hutokuwa na access ya jukwaa hilo (upo kwenye ban)
 
3) Kuwa mwenye mwenye adabu, mwenye heshima na muadilifu: Unapoamua kuwa mkosoaji au mtoaji wa maoni unapaswa kutambua kuwa wapo watu ambao masuala hayo yanawahusu au kuwagusa kwa namna moja au nyingine. Hivyo, unapawa kuwa mkarimu na kutumia busara ili usiumize hisia za watu wanaosoma andiko lako.[emoji120][emoji120][emoji120]

Jr[emoji769]
 
Kubali kuwa na mawazo au majibu yenye kujenga na wala yasiwe makali yenye kumshambulia mtu mwingine au kushambulia mawazo yao. Aidha, epuka kutumia herufi kubwa (CAPS), hati mkolezo au hati mlalo katika andiko lote. Kimsingi, andiko au uzi wako unapaswa kuwa wenye mawazo yenye mantiki yaliyosemwa vizuri. Hivyo, matusi yanayoelekezwa kwa mchangiaji hayakubaliki. Hata kama hukubaliani na mawazo yaliyotolewa na mshiriki mwingine haimaanishi kuwa mtu huyo hayupo sahihi (amekosea). Badala yake unapaswa toa maelezo au mtazamo tofauti ili kuchochea mjadala zaidi.

Jr[emoji769]
 
Epuka kutukana, kushambulia au kukwaza wengine: Maandiko ya chuki na yenye mrengo wa kuwashambulia watu hayatovumiliwa na JamiiForums. Wachukulie (waheshimu) wengine kama ambavyo wewe unataka uchukuliwe (uheshimiwe). Hivyo, kuleta andiko ambalo litachochea muitikio hasi kwa watu wengine inashauriwa kuepukwa.

Jr[emoji769]
 
Unayo haki ya kuhoji. Tumeweka jukwaa maalum la kulalamikia vitendo hivyo au unaweza kutumia Contact us endapo hutokuwa na access ya jukwaa hilo (upo kwenye ban)

Kuhusu matangazo ya biashara, hebu fafabua zaidi! Kwa mfano kwenye jukwaa la biashara zipo nyuzi biashara tofauti tofauti, mfano magari, viwanja na bidhaa nyingine!

Je, hao wenye nyuzi huwasiliana na uongozi wenu? Au ni matangazo ya biashara gani ambayo mdau anapaswa kuwasiliana na uongozi..!?
Lakini, pia pengine kuna matangazo yakulipia..!?
 
Shukrani sana kwa kutukumbusha jambo hili.

Hivi kosa la kutumia maandishi ya mtu mwingine kujenga hoja ama kuleta uzi mpya Jukwaani (JF) bila kumtambulisha mtu huyo iwe maandishi hayo yametolewa kwenye Nyuzi za Jf ama za mitandaoni mingine, ama vyombo vya habari vingine vya ndani ama nje ya nchi; je linaangukia katika masharti yapi!? Na adhabu yake ni nini!?

Kwa kifupi kosa la plagiarism JF inalishughulikiaje!?

Natanguliza Shukrani ya majibu.
====

Pendekezo ili kuongeza morali wa watu kutekeleza sheria za JF bila shuruti, iwepo Zawadi kwa watakao timiza jambo hili na iwepo Adhabu ya jumla kulingana na idadi ya makosa yaliyofanyika. Zawadi na Adhabu vitolewe kwa mwaka. Adhabu hizi hazibatilishi adhabu ya makosa mlioainisha kwe masharti yaliyopo kwenye post namba moja.
 
Hivi kosa la kutumia maandishi ya mtu mwingine kujenga hoja ama kuleta uzi mpya Jukwaani (JF) bila kumtambulisha mtu huyo iwe maandishi hayo yametolewa kwenye Nyuzi za Jf ama za mitandaoni mingine, ama vyombo vya habari vingine vya ndani ama nje ya nchi; je linaangukia katika masharti yapi!? Na adhabu yake ni nini!?

Kwa kifupi kosa la plagiarism JF inalishughulikiaje!?

Natanguliza Shukrani ya majibu.
 
Kuhusu matangazo ya biashara, hebu fafabua zaidi!
Kwa mfano kwenye jukwaa la biashara zipo nyuzi biashara tofauti tofauti, mfano magari, viwanja na bidhaa nyingine!
Je hao wenye nyuzi huwasiliana na uongozi wenu?
Au ni matangazo ya biashara gani ambayo mdau anapaswa kuwasiliana na uongozi..!?
Lakini, pia pengine kuna matangazo yakulipia..!?

Matangazo yaliyo jukwaa la matangazo ni bure; ukitaka kufikia watu zaidi ndo unalipia
 
Neno buku saba linakela ! Czani km niutani km cyo tusi! Hili lisimamiwe mkuu.
 
Mkuu, Maxence Melo. Mimi nipo huku JF kwa muda mrefu, zaidi ya miezi 6. Nifanyeje ili na Mimi niruhusiwe kuanzisha mada/bandiko hapa JF. Hasa kwenye General forum (habari mchanganyiko na matangazo madogomadogo). Maana nimekuwa Mara nyingi nikijaribu kuweka bandiko/mada LAKINI LAKINI sifanikiwi.Thanx.
 
Hapo No7 kwenye kuwapuuza wanachama wasumbufu umeongelea kuhusu ignore. Naomba mpafanyie maboresho kidogo ukim-ignore mtu usipate notifications zake kabisa.

Mfano, kuna mtu nimem-ignore nikajua tatizo limeisha ila aki-like post zangu napata notifications.
Hata Mimi hapa nakazia... Haiwezekani um-ignore mtu then still uwe unapata notification zake
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom