Pole kwa kupoteza wazazi.
Mara nyingi huwa tunajiuliza haya maswali, ni kwa sababu ya ubinadamu wetu. Ila jua tu hata Mungu angekuambia leo usingeelewa. Yeye anaona mwisho tangu mwanzo. Sisi tunaona kidogo sana. Yeye anajua yote, sisi tunajua katone kadogo sana. Akili zake hazina mwisho sisi hata chalinze hazifiki.
Kwa muktadha huu hatuwezi kumwelewa, si kwa nini amewachukua wazazi wako tu bali hata kwa nini aliruhusu wawe wazazi wako na sio uzaliwe kwingineko.
Cha msingi umshukuru Mungu kwa zawadi ya wazazi wako, waliokulea vizuri mpaka ukatamani wasiondoke. Kuna wengine hawakuwaona wazazi wao, wengine walikataliwa na wazazi wao na wengine hawajui hata wazazi wao ni akina nani.
Mwenye shamba kavuna shamba lake, ni nani wa kumhoji?