TANZIA My dad is gone

TANZIA My dad is gone

Tumepambana ila yeye (Mungu) kaamua yake simlaumu ila nina maswali mengi sana. Why now?

I lost my mother 4th February this year and today is 4th

I'm puzzled ila Ndio naanza uyatima leo
Pole kwa kupoteza wazazi.
Mara nyingi huwa tunajiuliza haya maswali, ni kwa sababu ya ubinadamu wetu. Ila jua tu hata Mungu angekuambia leo usingeelewa. Yeye anaona mwisho tangu mwanzo. Sisi tunaona kidogo sana. Yeye anajua yote, sisi tunajua katone kadogo sana. Akili zake hazina mwisho sisi hata chalinze hazifiki.

Kwa muktadha huu hatuwezi kumwelewa, si kwa nini amewachukua wazazi wako tu bali hata kwa nini aliruhusu wawe wazazi wako na sio uzaliwe kwingineko.

Cha msingi umshukuru Mungu kwa zawadi ya wazazi wako, waliokulea vizuri mpaka ukatamani wasiondoke. Kuna wengine hawakuwaona wazazi wao, wengine walikataliwa na wazazi wao na wengine hawajui hata wazazi wao ni akina nani.

Mwenye shamba kavuna shamba lake, ni nani wa kumhoji?
 
Pole sana kwa kuondokewa na mpendwa wako, Mungu awape faraja katika kipindi hiki.... apumzike kwa amani mzee, pole sana.
 
Pole sana Mkuu! Wengine tulishazoea muda ingawa kusahau ni vigumu.
Lakini nikutie Moyo tu kuwa hata kama wazazi hawapo Tena,Mungu yupo na yuko pamoja nawe.
 
Pole kwa kupoteza wazazi.
Mara nyingi huwa tunajiuliza haya maswali, ni kwa sababu ya ubinadamu wetu. Ila jua tu hata Mungu angekuambia leo usingeelewa. Yeye anaona mwisho tangu mwanzo. Sisi tunaona kidogo sana. Yeye anajua yote, sisi tunajua katone kadogo sana. Akili zake hazina mwisho sisi hata chalinze hazifiki.

Kwa muktadha huu hatuwezi kumwelewa, si kwa nini amewachukua wazazi wako tu bali hata kwa nini aliruhusu wawe wazazi wako na sio uzaliwe kwingineko.

Cha msingi umshukuru Mungu kwa zawadi ya wazazi wako, waliokulea vizuri mpaka ukatamani wasiondoke. Kuna wengine hawakuwaona wazazi wao, wengine walikataliwa na wazazi wao na wengine hawajui hata wazazi wao ni akina nani.

Mwenye shamba kavuna shamba lake, ni nani wa kumhoji?
Maneno yako yamenigusa[emoji120]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tumepambana ila yeye (Mungu) kaamua yake simlaumu ila nina maswali mengi sana. Why now?

I lost my mother 4th February this year and today is 4th

I'm puzzled ila Ndio naanza uyatima leo
Pole Sana,did you manage to tell him that you loved him???
 
Pole sana mkuu! Mungu akutie nguvu. Hauko pekee Yako katika njia unayopita, pamoja na jitihada kubwa tulizofanya ni week ya 3 sasa tangu Mzee wetu atangulie mbele za haki, mpaka sasa siamini naiona kama ndoto. Kufiwa kugumu hakuna uzoefu!
 
Back
Top Bottom