Matukio yaliyotokea kati ya October 29 na Novemba 3 yalinitafakarisha sana. Naishi nje ya mji kidogo Dar es salaam, Barabara ya Bagamoyo. Huwa nina kawaida ya kufanya mazoezi ya kutembea kwa lisaa kila asubuhi kabla ya kuanza shughuli zangu za siku.
Kama zilivyokuwa siku nyengine, tarehe 30 alfajiri nikatoka kwa ajili ya mazoezi, nikipita kwenye njia zile zile za kawaida. Lahaula, mwendo si mrefu, macho yangu yakaona maiti tatu za vijana wa kiume ambao, kwa kuwaangalia, walikuwa na majeraha mwilini. Nikiwa kwenye butwaa lile, nikasikia mlio wa risasi kwa mbali. Ikabidi nigeuze kurudi nyumbani.
Tangu siku ile, picha ile ya maiti zile tatu haijatoka bado kwenye kichwa changu na nimekuwa nikitafakari sana kuhusu kifo, uhai, umuhimu wa kuandika mirathi, kufanya toba, unyama wa binaadamu na mengi mengineyo. Roho za marehemu zipate Rehema kwa Mungu na zipumzike kwa amani. Amen.
Anyway, leo ni siku yangu ya kwanza kuhudhuria ibada ya asubuhi parokiani kwangu tangu nimalize kidato cha nne mkoani Morogoro miaka kadhaa iliyopita