My diary: Mdogo Mdogo hadi 31st December 2034 - Uwekezaji na mtindo wa maisha

My diary: Mdogo Mdogo hadi 31st December 2034 - Uwekezaji na mtindo wa maisha

Share split iliyotangazwa na kutekelezwa na NMB imenipa majuto kidogo kwa sababu sikuchukua hatua yoyote. Kabla ya split kutangazwa, bei ya hisa moja ilikuwa around 13,000. Baada ya split kutangwazwa ilipanda mpaka kufika 18,000 plus. Hata baada ya split kutekelezwa iliendelea kupanda kwa muda. Wapo waliotengeneza hela nyingi kipindi hiki.

Niliamua kubaki na tembo kwa sababu I was not sure. Pia my strategy ni slow and steady when it comes to investment. Lakini hii sharp clmb ya NMB ilitaka kuyumbisha msimamo wangu. Nashukuru sikuyumba and still pressing on. Upepo wa NMB now umeanza kupungua and share price is slowly coming back to actual value. Lahaula, soko la hisa hakuna ajuaye. The person who eventually wins, is the person who is able to stay composed amidst uncertainty. Mungu bariki hii safari inshallah.

Kwa wale mlio tegeta, nipo hapa butterfly kwa ajili ya dinner kabla sijaenda home. Nimetoka safarini morogoro kwa kutumia SGR. Kesho weekend. Feeling good.

Matashi mema kwenu nyote 🙏
 
Blessed life
 
Salaam kutoka jiji la Mwanza. Hapa Adden City Hotel. Nimetoka soko la samaki kubeba kitoweo kwa ajili ya familia, majirani na ndugu. Ndoo kubwa mbili zatosha. Kesho safari ya kurudi Dar es salaam baada ya kazi za wiki nzima jijini Mwanza.

Haya, Niwatakie nyote matashi mema ya wekeend.
 
Tangu Jumatatu wiki hii, nimekuwa kwenye hekaheka za kuuguza. Nilipokea simu kutoka kwa kaka yangu aliyepo Morogoro kwamba dada (wa tatu kuzaliwa) kapatwa na shida ta kiafya na kwamba hali yake sio nzuri. Hii ilikuwa usiku wa Jumatatu, tarehe 21 Septemba 2026.

Usiku huo huo nikawasha gari na kuelekea sinza ambapo ndipo anaishi. Nikiongozana na ndugu zangu wengine wawili, tukafika sinza na kukuta hali ya sister sio nzuri. Kupumua kwa shida, kuongea shida na nguvu za kutembea hazipo. Safari ya kuitafuta Kairuki hospital ikaanza. Kufika emergency hatua ya kwanza ikawa ni kuwekeza oxygen na drip za kutosha. Tukaondoka hospital majira ya saa 10 alfajiri na kumuacha akiwa kwenye uangalizi wa madaktari.

Siku zimepita na hali imezidi kuimarika sana ingawa bado utimamu haujarudi kwa asilimia 100.

Jambo muhimu, hasa kwa ndugu na marafiki, ni kuhakikisha tunajuliana hali mara kwa mara. Sio tu kwa kupigiana simu. Kutembeleana majumbani mara kwa mara ni utamaduni tunaohitaji kuuhuisha. Hutufahamisha hali walizonazo wengine pasina kutumia maneno. Huimarisha undugu pasina kutumia nguvu.

Yote kwa yote, Maradhi na kuhudumia wagonjwa ni ibada na nashukuru kwamba mgonjwa na wote tunaondelea kumuhudumia tumejinasibisha katika hilo.

Nimetoka hospital na kupita hapa target kabla sijaanza safari ya kurudi nyumbani kuianza wekeend. Nawatakia kheri nyote.
 
Back
Top Bottom