Sina uhakika kama hii ni kweli unatafuta mtu au ni changa moto hapa JF kuijadili. Kama ni kweli au la, naomba nitoe angalizo. Mara nyingi mambo yanayoleta shida na ugomvi kati ya wenza wawili ni mambo yasiyo na maana lakini ndi hasa mambo yanayomsibu mtu. Hakuna good reasoning katika tabia na mapenzi ya mtu. Hapa umeweka mambo unayoyaona wewe, lakini hujaweka mambo mengine nyeti pia katika maisha ya wawili (pengine si mahali pake) lakini utashangaa watu wakiulizwa ni mume gani wanataka watakupa vigezo muafaka lakini wakifika kuchagua utashangaa vitu vinavyowavuta, RANGI TU YA NGOZI inaweza ikawa ndio kivutio.
Mara nyingi kuna mambo mengi ambayo hatuyaweki wazi toka mwanzo, ntatoa mfano,watu wengine wanahamu ya tendo la ndoa kila mara, hata kama ni mume anaweza akaja huko akakuta unapika na akataka uache kila kitu mwenda chumbani kidogo, wewe unafanyaje pengine utakataa, kwa sababu wewe hauko kwenye mood, mara mbili, mara tatu nini kinatokea???????????????? je ulijua hayo, maana vipengele vyako pale havionyeshi hilo. je kama wewe hujui kupika vizuri nae kila siku anataka pilau, lasanya ya kifaransa, mtori wa kichaga nawe mmakonde, inakuwaje?????????? maisha magumu ndani ya nyumba hayasababishwi na mambo ya msingi la hasha hayo huwa kisingizio tu kwa vile yale ya kweli hayawezi semwa waziwazi, wengine wanapenda staili hii nawe unaichukia SASA inakuwaje???!!!!!!!!!!!! anapenda ndugu zako, mama yako akija atamfurahia vile ambavyo wewe ungetaka, asije akawe anachelewa kurudi kwa vile mama mkwe anamboa, je akija mdogo wako bado mbichi naye asimwangalie hata kama ni kwa upendo wa kweli kwa ndugu yako (nao wakati mwingine wanamtamani shemeji yao, anapendeza wakamjia na kanga moja) mpendwa yako mengi ya kuangalia na mengi hayakai hapa. Nina mfano halisi mmoja, nilipokuwa chuo, darasa letu lilikuwa na wadada kumi, wawili kati ya hao walikuwa hivi
- mmoja alikuwa (na bado) anachukia boyfriend/mme anaevuta sigara, yaani hata kumwangalia tu mtu anayevuta sigara anakasirika hata kula anaweza acha, HAPENDI HAPENDi, HATAKI hakuna mjadala hapo na hataki kitu hapo,
- wa pili, anataka na anapenda boyfriend/mme anayevuta sigara, yaani alikuwa anasema yeye lazima aolewe na mme anavuta sigara tu (aliolewa na mvutaji, ni miaka 18 mpaka sasa na wako safi mpaka leo)
++++ sasa, wote hawa wadada walikuwa wazuri tu wa maumbo, wote wanasome chuo kikuu, kozi moja, wote wachaga++++++++++
je kama hao wangeandika mambo ya mumu wanaetaka wangeweka hayo???? je huyu anaependa sigara si kila mmoja angesema wewe vipi sigara inaharibu afya n.k. n.k. n.k. lakini ndio anachopenda na yuko tayari kugombana kwa hilo.
Wazo langu,
- Kwanza kaa peke yako, andika vitu vyote, vyote, vyote unavyopenda hata kama ni vibaya, vibaya namna gani lakini ndio vitu unapenda (hata kama ni kula chakula uchi huku umekaa juu ya choo) hii si kwa kumridhisha mtu mwingine bali wewe mwenyewe, usijali ni vibaya kijamii, wako wadada wanapenda majambazi, hata wengine wanapenda walio rafu katika tendo la ndoa, sio soft soft (mdada mwingine yeye alikuwa hapendi romance romance, anataka moja kwa moja kwenda kwenye shughuli yenyewe, na alikuwa anasema hivyo) tutamcheka lakini ndicho anachotaka. HIVYO JIONYESHE UNATAKA NA KUPENDA NINI KUKWELIIII
- PILI endelea hivo hivyo ukiwa peke yako, unachukia nini kwa moyo wako wote, hata kama ni kitu kizuri kwa jamii, pengine hupendi mtu msafi sana, hupendi mcha Mungu sana, hupendi kufanya tendo la ndoa mara kwa mara, hupendi kupika, hupendi kusalimi salimu watu hata kama ni wakwe zako, n.k. n.k. n.k.
Baada ya hayo ndipo sasa unasema katika hayo yote,
ni yapi niliyotayari kuyavumilia na yapi sitaki mjadala
yapi niko tayari kuyapokea hata kama siyapendi
YAPI SITAKI WALA KUSIKIA hata kama ni mazuri, (wewe unasema hutaki mme shingo feni, lakini mmimi namfahamu mke mmoja anapenda wanawake wengine wakimtaka mme wake, maana anajidai kumbe ana kifaa, na huwa anahakikisha anapendeza ili wamtamani, na hata anamwambia aongee nao tu na akiweza kumtoroka akapa kidogo sio mbaya HAYA SASA, UKISHANGAA YA MUSA UTAONA YA FIRAUNI, nae kaolewa wana watoto mpaka leo INAKUWAJE
+++++++++++ MPENDWA WATU WAKO VILE WALIVYO SI VILE WANATAKIWA KUWA+++ na hiyo haiwabadilishi