Mazingira magumu na ukosefu wa ajira umewalizimu kufanya kazi kwa wahind, sisupport ubaguz, ila kwa kweli ukiexperience manyanyaso ya wahindi walio wengi kwa Watanzania na mazingira magumu ya kazi kwa unskilled labourers aisee waweza wachukia kama bornagain anavyowachukia..
Jee, umeshafanya kazi kwa wahindi?
Nashangaa sana mnaposema mazingira magumu, wakati hii nchi ni yenu na kuna kila fursa za kujifanyia kazi mwenyewe kama hutaki kuajiriwa. Leo hii ukiwa na msingi wa Shillingi laki moja tu unaweza kufanya kazi yenye kukupatia faida ya kukulisha na kukuvisha kuliko mshahara wa kima cha chini na cha kati. Umeshayafikiria hayo? au ni bongolala na hujuwi 50,000/= zitakuzalishia vipi. Kama hujui niambie nikupe darsa la uwekezaji mdogo mdogo.
Leo hii, kuna watu wananyanyaswa na Waafrik wenzao na tunayaona kwenye magazeti kila siku.
Hao mnaosema Wahindi mkumbuke kuwa wengi wao ni Watanzania na wana Uzalendo kuliko nyinyi wabaguzi wa rangi.
Niambie leo Hii, Mohamed Dewji wa METL ameajiri directly na indirectly watu wangapi?
Niambie leo Hii, Manji wa Quality group ameajiri directly na indirectly watu wangapi?
Niambie leo Hii, Jeetu Patel na makampuni yake, ameajiri directly na indirectly watu wangapi?
Niambie leo Hii, GAPCO (inamilikiwa na Watanzania wenye asili ya kihindi) wameajiri directly na indirectly watu wangapi?
Hao ni wachache tu nnaoweza kuwataja ghafla ghafla. Hivi mnataka kusema nini? kushindwa kwenu wanapoweza wenzenu ndio muwachukie?
Kama huyo mtoto Miss Tanzani, babu yake, mama yake wote wazaliwa wa Tanga alikuyanyasa nini> mtoto anekaa Kariakoo toka kuzaliwa, kukuwa kwake. Mwenyeezi Mungu kamjaalia uzuri usio na mfano, leo eti eeh Mhindi. Hup Uhindi mlipa nyinyi?
Mbona nyinyi kutwa kucha mnajitia mikorogo na kubandika nywele za maiti kuutaka huo uhindi msiokuwa nao?
Huyu hapa na mama yake, na uzuri wake si wa makopo wala wa bahati mbaya ni wa asili, tazama mama'ke alivyo mzuri, MashaAllah:

Mnaacha mambo ya maana oohh eti wahindi "wabaguzi" wakati ubaguzi na roho mbaya ndio zimewakaa mioyoni mwenu.
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.