My Salute Kwa Wabunge:- That is How We Treat Traitors!!


Mkuu mbona sikuelewi!! Kwani issue ni Serikali tatu ndiyo imesababisha Wabunge wapige makelele? Hebu jiridhishe upya.. Kilichopigwa kelele ni kutengua KANUNI ili Warioba aanze kuwasilisha then Rais JK aje azindue kwa lengo la kuja kuweka mambo sawa maana wanajua Wairoba atachafua hali ya hewa.. Huo mpango watu wameshaushtukia ndiyo maana watu wamekomaa Warioba asisome mpaka JK azindue Bunge...

Mimi nashangaa sana CCM kuifanya nchi hii kama ya kwao peke yao. Hayo maoni si ya Warioba ni maoni ya wananchi na hii Tume si ya kwanza kuja na mapendekezo haya ya Serikali tatu.. Ni tume ngapi zimeundwa na kutoa mependekezo ya Serikali 3. Naamini na sitaki kukubaliana na wewe Nyerere hakuwa rigid kihivyo na msitumie kichaka cha Nyerere kutetea serikali mbili..Mambo mangapi ya msingi ambayo Nyerere aliyasimamia mmeyapuuza na kuyazika.. Leo kwenye serikali tatu mnajifanya mnakumbuka Nyerere...

Nawapongeza Wabunge kwa kutumia fursa na huo ndiyo uwe utaratibu hakuna kuburuzwa kijinga... Nchi hii ni ya kwetu sote.. Mmeshindwa miaka 50 acha watanzania wajitete na kuendeleza nchi yao...
 
Inaonekana wazi mleta mda hata hajui kinachoendelea bungeni
 
- Mkuu hakuna baba yako hapa kuna siasa za Taifa, Warioba anamsaliti Mwalimu Baba wa Taifa hili aliyekuwa akimuamini sana mpaka kumpa Uwaziri kila wakati, mimi Warioba angesema Mwalimu akiwa hai kwamba hataki Muungano nisingekuwa na tatizo na hoja zake leo, kama ninavyomuheshimu Kasaka Njelu, yule alisimama mbele ya Mwalimu akasema hataki Muungano, wengine wote ambao hawakusema ni WASALITI!! - Warioba aliteuliwa kukusanya maoni sio kutengeneza maoni kama alivyofanya, huwezi kupanda mahindi ukavuna mihogo leo Warioba amevuna alichopanda!! Le Mutuz
 
Naomba uniambie faida tatu tu za huu muungano wa tembo na huyu sisimizi mnyonyaji.
 

Kwa maana hiyo wabunge waliokaa kimya (CCM) ni traitors!
 
Sometimes try to think outside the box
Mwalimu sio Mungu kwamba mawazo yake yako sahihi wakati wako, tunaishi dunia inayobadilika
Alikua muumini wa Ujamaa na chama kimoja na kura zikapigwa watu wakasema wanataka chama kimoja,,,,,,,jiulize kwanini alisema wapewe waliotaka vyama vingi?
 
W. J. Malecela
Baba yako aliwahi kutaka serikali tatu, je yeye ni sawa na warioba??? muungano ni kitu chenye uhai wa kisheria, kinaweza kufa, kushitaki au kushitakiwa, kinaweza kupitia uhai wake kukua na kubadilika sura, je ni dhambi leo kuwa na serikali tatu vile tu marehemu Nyerere alisema wakati wa uhai wake sio lazima??? Warioba ametaka wazi serikali tatu kwa vile wanzibar wametmka wazi serikali moja ambalo ndo best option hawataki, sasa unamlaumu warioba kwa kuja na majibu ya swali na suala ambalo bia kuuma maneno CCM imekosea sana kuwa na serikali 2??? ni ama moja au tatu. Wananchi DHIDI YA CCM, tutaona nani mshindi.
 
We bonge kwani warioba si alitumwa akakusanye maoni mbona unamshambulia yeye binafsi?

Hatutaki huo muungano wenu,we uliona wapi muungano wa nchi 2 unakuwa na serikali 2?

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
 
- Hakuna baba wa mtu yoyote hapa wala baba yako, please tumia akili kidogo tu!! Le Mutuz
 

Baba ako mbona humtaji aliporuhusu issue ya Serikali tatu enzi zile ijadiliwe bungeni? Isingekuwa vile leo ungekuwa na wewe unachezea Tausi Ikulu pale coz kutofautiana na Nyerere ndo kulimponza mzee wetu
 
Hivi kuna VITI MAALUM kwa ajili wa "wa kiume"? Kama vipo no doubt huyu jamaa atapata!!!!!
 

Sina kawaida ya ku-quote taarifa ndefu kama hii yako lakini imenibidi. Naona kabisa udhaifu wako. Kwa nini unalazimisha mawazo yako yawe ndo wazomeaji? Umewaona wanaozomeya au ni kitu gani kichwani?

Sababu uliyotaja haikuwa bungeni leo kabisa. Naamini una rafiki au marafiki wanaoweza kukusimulia mara ya pili. Tatizo ni kukiuka kanuni, kutengua kanuni ambayo imemruhusu Warioba kusoma rasimu kabla ya hotuba ya Rais. Sasa hapo uzalendo umeanzia wapi? Udhaifu unaweza kuwa ni wa Mwenyekiti, anaonyesha umwamba usiokuwa na sababu, madaraka na kujinadi busara bila mipaka.

Hili Bunge linahitaji mwenye uwezo wa kufikiri siyo mzoefu tu ambaye ana sifa ya kukumbuka aliyokuwa akifanya miaka yote.

Tusiendelee kuambiwa mambo ya baba wa Taifa, baba mpaka lini? Mbona hutamani Azimio la Arusha kiasi hicho? au ktk mambo ya maana ni muungano tu! Nilitamani sana kuona CV yako maana kumbe sasa tuko hatarini, kila tunachotaka kufanya mtu anaibuka na kusema 'baba wa Taifa', so what? Ni simba kwamba atatung'ata kama lugha ya kitoto inayotumika? Tangu alipokufa sisi tuache kufikiri utadhani alifariki na ubongo wetu!
 
You are less informed, kumbe hata kinachoendelea hujui.

Achana naaye huyo mbaba, kwani alichoandika nimekipitia mwanzo mwisho sijui ameandika nini na sijui alikuwa anangalia Tv gani....
 
Naomba uniambie faida tatu tu za huu muungano wa tembo na huyu sisimizi mnyonyaji.

Mkuu naona unatekeleza kwa vitendo ile kauli mbiu yako ya Taifa kwanza vyama baadae. Yani kama tulivyoungana JF members wote kum-support JK kwenye bifu lake na Kagame, na sasa tumeungana tena kwenye Katiba ya nchi yetu.

My note kwa Le mutuz: Wakati ukuta usijaribu kupigana nao
 
Yumezoea kupewa na uongozi watu waliofanya vizuri kwenye jukwaa.Napendekeza tupewe poll ya kumtafuta Flop of the forum ili ashushwe kwenye jukwaa milele!
Kwa kuanzia my flop/kilaza of the Jukwaa la siasa is W:Malechela.
 

Msomi mzima umechukua muda mrefu kuandika kitu kidogo tu na ueshindwa kueleweka.........unafikiri ni akili za wale watu wako ndio zimesababisha Walioba asitoe hutuba? Unajua chanzo ni nini soma hapa acha kubeba mwili tu....https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...anzo-cha-bunge-kuahirishwa-2.html#post8981561
 
Kweli nimeamini ukiona mtu analia au anapiga kelele kila mtu aweza kuja na tafsiri Yake maana hajui sababu ya Sauti itokayo. Ndivyo ilivyotokea bungeni na huyu mtu ameamua kupotosha. Sababu ni mwenyekiti wa bunge sitta kukiuka kanuni Za bunge maalum na si Kama asemavyo huyu mwana CCM mvivu wa kutafuta uhalisia.
 
Wacha ujinamizi ,hivi kwa akili zako haya au hyo rasimu ni mawazo ya Warioba ? zimepita tumengapi kuhusiana na Muungano na zote zimekuja na serikali tatu ,kwa aliyoyakusanya Warioba si mageni kwa Watanzania ,wewe kama unafaidika na urithi ambao hutokana na jasho la walala hoi ,one day yes itawatoea puani jasho lao ,baba kadhulumu na watoto nao pia wadhulumu ,kwa taarifa yako Tanganyika ya leo ni tofauti na ile waliyoiacha wazee wenu ,kama Uccm karibu WaTz wote walikuwa CCM.

Msiwe malimbukeni na hapo bungeni kilichopingwa ni hujuma za CCM na ndio hivyo zimepingwa na mliyoyapanga hayakuwa ,pole sana unasifu usichokifahamu.

Sasa jipimeni vizuri sana ikiwa hapo mmetulizwa je huko kunakoelekewa ? Na huo ujeshi unaojilabu nao ,sidhani kama utamtisha mtu kwani zama za kutishana zimepitwa na wakati UJKT!!! watu wana UJWTZ wametulia tuli . Heshima mliokuwa mkipewa mmeipoteza na haitorudi tena ,Muungano utajadiliwa na serikali tatu ndio hitimisho vyenginevyo mtakufa na donge la roho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…