My Salute Kwa Wabunge:- That is How We Treat Traitors!!

My Salute Kwa Wabunge:- That is How We Treat Traitors!!

- Leo nimejionea kwa macho na masikio yangu Wabunge wanaomkumbuka Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, sikutegemea kua bado tuna Wabunge wenye Uzalendo wa kukumbuka tulikotoka hili Taifa. Kumbe bado tunao Wabunge wenye uchungu na Taifa letu, kumbe bado tunao Wabunge wenye kuelewa kwamba Duniani hakuna Serikali ya Jamhuri yenye Marais 3. - Warioba alipoteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Rasimu aliapa kwa kiapo kile kile cha Jamhuri, kwamba ataulinda Muungano kwa akili zake zote na nguvu zake zote, aliapa viapo hivi maisha yake yote mbele ya Mwalimu muasisi wa Muungano, sasa leo Mwalimu hayupo Warioba amebadilika hataki tena Muungano, halafu kibaya hajawahi kusema hadharani kuwa Mwalimu was wrong na Muungano, halafuhajawahi kutuambia hili Taifa kwamba huko nyuma alikuwa anaunga mkono Muungano na sasa hautaki, ila aemjificha ficha nyuma ya Rasimu na kutaka kupenyeza agenda yake ya kisaliti, bravo wabunge wangu leo nimejisikia vizuri sana na hasa imenikumbusha zile enzi za JKT nilipokuwa Oljoro Arusha kwenye "OPERATION TEKELEZA", - JAMANI WALE WOTE KAMA WARIOBA MNAOTAKA KUVUNJA MUUNGANO SUBIRI SISI WOTE TULIOPITIA JKT TUSIWEPO, NDIO MTAPITISHA UPUUZI WENU WA KUVUNJA KILA KITU: WARIOBA ALIKUW WAZIRI MKUU NA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS ASIYETAKA MUUNGANO LAKINI HAKUSEMA HATA SIKU MOJA, ANAKUJA KUSEMA LEO TENA KWA KUJIFICHA NYUMA YA PAZIA LA RASIMU YA KATIBA, LEO AMEJIONEA MWENYEWE KWAMBA SIO WABUNGE WOTE NI SAWA WALE WANANCHI ALIOKUWA ANAWABURUZA KWENYE VIKAO VYAKE KULE MIKOANI. - KUTAKA SERIKALI 3 NI KUVUNJA MUUNGANO KWA KIONGOZI YOYOTE WA TAIFA ALIYEAPISHWA NA RAIS KUDAI HAYA NI USALITI, HENGERENI SANA WABUNGE WOTE MLIOSIMAMA KIDETE LEO, MTALIPWA NA MUNGU WA MBINGUNI TU WARIOBA NA KUNDI LAKE MTALIPWA HAPA HAPA DUNIANI KWA KUTAKA KUTUVURUGA SISI WANANCHI WA TANZANIA, MSHINDWE NA MLEEEGEEEE WOTE WASALITI WAKUBWA WA MWALIMU BABA WA TAIFA!! Le Mutuz

Mkuu mbona sikuelewi!! Kwani issue ni Serikali tatu ndiyo imesababisha Wabunge wapige makelele? Hebu jiridhishe upya.. Kilichopigwa kelele ni kutengua KANUNI ili Warioba aanze kuwasilisha then Rais JK aje azindue kwa lengo la kuja kuweka mambo sawa maana wanajua Wairoba atachafua hali ya hewa.. Huo mpango watu wameshaushtukia ndiyo maana watu wamekomaa Warioba asisome mpaka JK azindue Bunge...

Mimi nashangaa sana CCM kuifanya nchi hii kama ya kwao peke yao. Hayo maoni si ya Warioba ni maoni ya wananchi na hii Tume si ya kwanza kuja na mapendekezo haya ya Serikali tatu.. Ni tume ngapi zimeundwa na kutoa mependekezo ya Serikali 3. Naamini na sitaki kukubaliana na wewe Nyerere hakuwa rigid kihivyo na msitumie kichaka cha Nyerere kutetea serikali mbili..Mambo mangapi ya msingi ambayo Nyerere aliyasimamia mmeyapuuza na kuyazika.. Leo kwenye serikali tatu mnajifanya mnakumbuka Nyerere...

Nawapongeza Wabunge kwa kutumia fursa na huo ndiyo uwe utaratibu hakuna kuburuzwa kijinga... Nchi hii ni ya kwetu sote.. Mmeshindwa miaka 50 acha watanzania wajitete na kuendeleza nchi yao...
 
Inaonekana wazi mleta mda hata hajui kinachoendelea bungeni
Page
1
of
4
BARUA YA UMOJA WA KATIBA YA WANANCHI (UKAWA) KWA
MWENYEKITI WA BUNGE MAALUM, MHESHIMIWA SAMWEL J. SITTA,
KUHUSU UKIUKWAJI WA KANUNI ZA BUNGE MAALUM
Mheshimiwa Mwenyekiti,
Sisi ambao majina yetu yameorodheshwa hapa chini ni Wajumbe
wa Bunge Maalum ambao tunatokana na vyama vya CHADEMA,
CUF, NCCR Mageuzi, DP, UDP, CHAUSTA, CHAUMA, NRA, NLD na
CCK pamoja na Wajumbe walioteuliwa kutokana na makundi
yaliyotajwa katika kifungu cha 22(1)(c) cha Sheria ya Mabadiliko
ya Katiba, Sura ya 83. Tumeunda Umoja wa Katiba ya Wananchi
(‘UKAWA') wenye lengo la kuhakikisha kwamba mchakato wa
sasa wa Katiba katika Mkutano huu wa Bunge Maalum
unapelekea nchi yetu kupata Katiba Mpya na bora kwa ajili ya
nchi yetu.
Kwa sababu ya mwendelezo wa matukio ya ukiukwaji wa
makusudi wa Kanuni za Bunge Maalum, 2014, ambao umefanyika
tangu ulipoapishwa kuwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum, kama
tunavyoonyesha hapa, tunapenda kukufahamisha kwamba
hatuko tayari kuendelea kukaa kimya wakati unaendelea kuvunja
Kanuni za Bunge Maalum na kupelekea Mkutano wa Bunge
Maalum kuwa hatarini kuvunjika. Katika kipindi cha siku nne tangu
umeapishwa kuwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum umefanya
maamuzi yafuatayo yanayodhihirisha ukiukwaji wa Kanuni:
1. Tarehe 14 Machi, 2014, mara tu baada ya kuapishwa
ulitangaza kwamba Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya
Katiba atawasilisha Rasimu ya Katiba siku ya Jumatatu,
yaani leo. Aidha, ulitangaza kwamba baada ya Mwenyekiti
wa Tume kuwasilisha Rasimu, kutakuwa na kipindi cha siku
tatu kwa Wajumbe wa Bunge Maalum kufanya mjadala wa
jumla juu ya Rasimu kwa lengo la ‘kufungua vifua vyao.' Vile
vile, ulilitaarifu Bunge Maalum kwamba baada ya hapo
Mheshimiwa Rais atakuja kulihutubia Bunge Maalum kati ya
siku ya Jumanne au Jumatano.
Page
2
of
4
2. Licha ya Wajumbe kadhaa wa Bunge Maalum kukuomba
ubadilishe msimamo wako juu ya masuala haya, tarehe 15
Machi uliendeleza msimamo huo na ukaongeza kwamba
Mwenyekiti wa Tume atawasilisha Rasimu ya Katiba kwa
muda usiozidi dakika sitini na baada ya hapo kutakuwa na
siku tatu za semina itakayoongozwa na wataalamu kutoka
nje ya nchi yetu na baadaye ndiyo Mgeni Rasmi atakuja
kulihutubia Bunge Maalum.
3. Leo tarehe 17 Machi baada ya malalamiko ya Wajumbe
kadhaa umesema kwamba umeshauriana na Mwenyekiti
wa Tume jana tarehe 16 Machi na mmekubaliana kwamba
muda wa saa mbili (dakika mia moja ishirini) zitamtosha
Mwenyekiti wa Tume kuwasilisha Rasimu ya Katiba. Hii
inathibitisha kwamba ulipopanga muda wa dakika sitini kwa
ajili hiyo siku ya tarehe 15 Machi ulikuwa hujashauriana na
Mwenyekiti wa Tume kama inavyotakiwa na Kanuni za
Bunge Maalum. Aidha, kwa taarifa tulizo nazo, inaelekea
Mwenyekiti wa Tume analazimishwa kukubaliana na muda
ambao wewe mwenyewe na nguvu nyingine zilizo ndani na
nje ya Bunge Maalum mmempangia.
Kwa maoni yetu, yote haya ni ukiukwaji wa makusudi wa
Kanuni:
(a) Kanuni ya 7(1)(g) na (h) ya Kanuni za Bunge Maalum
imeweka mpangilio wa shughuli zote za Bunge Maalum
ambapo ‘hotuba ya ufunguzi ya Mgeni Rasmi', i.e., Rais
wa Jamhuri ya Muungano au Rais wa Zanzibar,
itafuatiwa na ‘uwasilishaji wa Rasimu ya Katiba.' Kwa
jinsi ya mpangilio wa shughuli uliowekwa na Kanuni ya
7(1), uwasilishaji wa Rasimu ya Katiba kabla ya hotuba
ya ufunguzi ya Mgeni Rasmi ni ukiukwaji wa Kanuni za
Bunge Maalum na, kwa vyovyote vile, kunatoa picha
kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano atakuja
Bungeni kama mchangiaji wa hoja badala ya kuja
Page
3
of
4
kama Mkuu wa Nchi kwa lengo la kufungua Bunge
Maalum;
(b) Kanuni ya 47(a) inaelekeza kwamba "Mwenyekiti
baada ya kushauriana na Mwenyekiti wa Tume
watapanga muda unaofaa kwa ajili ya Mwenyekiti wa
Tume kuwasilisha Rasimu ya Katiba katika Bunge
Maalum." Pamoja na kwamba kanuni hiyo imeanza
kwa maneno ‘isipokuwa kama imeelezwa vinginevyo
kwenye Kanuni hizi au Mwenyekiti ameelekeza
vinginevyo', ufahamu wetu wa Kanuni za Bunge
Maalum unatuelekeza kwamba Mwenyekiti wa Bunge
Maalum hana uwezo kikanuni wa kujipangia yeye
mwenyewe muda ambao Mwenyekiti wa Tume
atahitaji kwa ajili ya kuwasilisha Rasimu ya Katiba.
Muda huo unatakiwa kupangwa kwa pamoja baada
ya mashauriano baina yao.
(c) Kwa mujibu wa kanuni ya 31(3), "baada ya Rasimu
kuwasilishwa ... Mwenyekiti atatangaza majina ya
wajumbe wa kila Kamati ... na kila Kamati itatekeleza
majukumu yake kwa mujibu wa masharti yaliyowekwa
na Kanuni hizi." Aidha, kwa mujibu wa mpangilio wa
kanuni ya 32, baada ya Kamati kuundwa, Rasimu
itajadiliwa katika Kamati na baadaye katika Bunge
Maalum. Kwa mtiririko wa Kanuni ulivyo, hakuna namna
yoyote halali kwa Bunge Maalum kufanya semina ya
wataalamu wa ndani au nje ya nchi kwa lengo la
wajumbe kufungua vifua vyao au kwa lengo lingine
lolote.
(d) Matumizi mabaya ya kanuni ya 85 inayohusu mamlaka
ya kutengua kanuni. Ijapokuwa kanuni ya 85(1)
inatamka kwamba "... kanuni yoyote inaweza
kutenguliwa kwa madhumuni mahsusi ...", kanuni hiyo
Page
4
of
4
imefungwa na masharti ya kanuni ya 85(4) inayoelezea
mazingira yanayoweza kusababisha kanuni itenguliwe.
Kwa kifupi, kanuni inaweza kutenguliwa kwa ajili ya
kuahirisha kikao au kuongeza muda wa shughuli au
kuongeza orodha ya shughuli yoyote ambayo
haikuwepo kwenye mpangilio wa shughuli za siku hiyo.
Nje ya mazingira hayo, Bunge Maalum haliwezi
kutengua kanuni zake.
Kwa sababu ya ukiukwaji huu wa Kanuni za Bunge Maalum
tunapenda kukujulisha kwamba sisi wanachama wa UKAWA
hatuko tayari kuunga mkono, na tutapinga kwa kadri ya
uwezo wetu mambo yafuatayo kufanyika ndani ya Ukumbi
wa Bunge Maalum:
(i) Uwasilishaji wa Rasimu ya Katiba na Mwenyekiti wa
Tume kabla ya hotuba ya ufunguzi wa Bunge
Maalum na Rais wa Jamhuri ya Muungano au Rais
wa Zanzibar;
(ii) Semina yoyote itakayoongozwa na wataalamu wa
ndani au nje ya nchi yetu kama ulivyolitangazia
Bunge Maalum;
(iii) Hotuba ya Mgeni Rasmi endapo itafuatia uwasilishaji
wa Rasimu ya Katiba;
(iv) Jambo lingine lolote linalokiuka Kanuni za Bunge
Maalum.
Tunatarajia kwamba utayapa masuala haya tafakuri ya kutosha ili
uweze kufanya maamuzi kwa kutumia Kanuni za Bunge Maalum.
Tunaamini utatumia busara na hekima ili kuliepusha Taifa letu na
fedheha ya vurugu zisizokuwa na sababu ndani ya Bunge
Maalum.
Tunatanguliza shukrani zetu za dhati.
 
:juggle: :flypig: :kev:😛layball::llama::llama::llama::violin::deadhorse::llama::deadhorse::llama::llama::bump2::bump2::flypig::tea::hippie::msela::msela::shetani::majani7:.......Huu ni mtazamo wako binafsi.. usimsingizie mwalimu wala Warioba... warioba hakujichagua kuwa mwenyekiti wa tume.. la sivyo mlaumu aliyemchagua... Warioba hakuandika rasimu peke yake alipita kwa wananchi na hayo ndio matakwa ya wananchi.... watanzania wa leo sio wale wa mika ya nyuma .. ni watafiti ni watu wasikubali kuburuzwa sio wanaoamuliwa .... kumlaumu warioba ni kumuonea... maneno yako uliyoyatoa pamoja na kejeli na matusi kwa Warioba ni ukosefu wa adabu na heshima kwa wakubwa ... umri wa Warioba unafanana na Mzee JS Malecela sio vizuri kutukanaa matusi ya kejeli kwa watu waliokuzidi umri na hasa ukizingatia wanaumri sawa na baba yako...
- Mkuu hakuna baba yako hapa kuna siasa za Taifa, Warioba anamsaliti Mwalimu Baba wa Taifa hili aliyekuwa akimuamini sana mpaka kumpa Uwaziri kila wakati, mimi Warioba angesema Mwalimu akiwa hai kwamba hataki Muungano nisingekuwa na tatizo na hoja zake leo, kama ninavyomuheshimu Kasaka Njelu, yule alisimama mbele ya Mwalimu akasema hataki Muungano, wengine wote ambao hawakusema ni WASALITI!! - Warioba aliteuliwa kukusanya maoni sio kutengeneza maoni kama alivyofanya, huwezi kupanda mahindi ukavuna mihogo leo Warioba amevuna alichopanda!! Le Mutuz
 
- Wale wanaotaka Serikali 3 nia na madhumuni yao ni kuvunja Muungano, alianza Jumbe, akaja Sefu, sasa wao wasaliti I mean ni TRAITORS hawana jipya badala ya kutuletea mawazo mapya wanatuletea habari za kuvunja kila kitu, hapana sasa leo ndio wamejionea kwamba sio wananchi wote wa Tanzania ni wajinga wa kuyumbishwa yumbishwa na watu wachache wenye tamaa ya madaraka!! Le Mutuz
Naomba uniambie faida tatu tu za huu muungano wa tembo na huyu sisimizi mnyonyaji.
 
Kwa maana hiyo wabunge waliokaa kimya (CCM) ni traitors!
 
- Wale wanaotaka Serikali 3 nia na madhumuni yao ni kuvunja Muungano, alianza Jumbe, akaja Sefu, sasa wao wasaliti I mean ni TRAITORS hawana jipya badala ya kutuletea mawazo mapya wanatuletea habari za kuvunja kila kitu, hapana sasa leo ndio wamejionea kwamba sio wananchi wote wa Tanzania ni wajinga wa kuyumbishwa yumbishwa na watu wachache wenye tamaa ya madaraka!! Le Mutuz
Sometimes try to think outside the box
Mwalimu sio Mungu kwamba mawazo yake yako sahihi wakati wako, tunaishi dunia inayobadilika
Alikua muumini wa Ujamaa na chama kimoja na kura zikapigwa watu wakasema wanataka chama kimoja,,,,,,,jiulize kwanini alisema wapewe waliotaka vyama vingi?
 
W. J. Malecela
Baba yako aliwahi kutaka serikali tatu, je yeye ni sawa na warioba??? muungano ni kitu chenye uhai wa kisheria, kinaweza kufa, kushitaki au kushitakiwa, kinaweza kupitia uhai wake kukua na kubadilika sura, je ni dhambi leo kuwa na serikali tatu vile tu marehemu Nyerere alisema wakati wa uhai wake sio lazima??? Warioba ametaka wazi serikali tatu kwa vile wanzibar wametmka wazi serikali moja ambalo ndo best option hawataki, sasa unamlaumu warioba kwa kuja na majibu ya swali na suala ambalo bia kuuma maneno CCM imekosea sana kuwa na serikali 2??? ni ama moja au tatu. Wananchi DHIDI YA CCM, tutaona nani mshindi.
 
We bonge kwani warioba si alitumwa akakusanye maoni mbona unamshambulia yeye binafsi?

Hatutaki huo muungano wenu,we uliona wapi muungano wa nchi 2 unakuwa na serikali 2?

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
 
W. J. Malecela Baba yako aliwahi kutaka serikali tatu, je yeye ni sawa na warioba??? muungano ni kitu chenye uhai wa kisheria, kinaweza kufa, kushitaki au kushitakiwa, kinaweza kupitia uhai wake kukua na kubadilika sura, je ni dhambi leo kuwa na serikali tatu vile tu marehemu Nyerere alisema wakati wa uhai wake sio lazima??? Warioba ametaka wazi serikali tatu kwa vile wanzibar wametmka wazi serikali moja ambalo ndo best option hawataki, sasa unamlaumu warioba kwa kuja na majibu ya swali na suala ambalo bia kuuma maneno CCM imekosea sana kuwa na serikali 2??? ni ama moja au tatu. Wananchi DHIDI YA CCM, tutaona nani mshindi.
- Hakuna baba wa mtu yoyote hapa wala baba yako, please tumia akili kidogo tu!! Le Mutuz
 
- Wale wanaotaka Serikali 3 nia na madhumuni yao ni kuvunja Muungano, alianza Jumbe, akaja Sefu, sasa wao wasaliti I mean ni TRAITORS hawana jipya badala ya kutuletea mawazo mapya wanatuletea habari za kuvunja kila kitu, hapana sasa leo ndio wamejionea kwamba sio wananchi wote wa Tanzania ni wajinga wa kuyumbishwa yumbishwa na watu wachache wenye tamaa ya madaraka!! Le Mutuz

Baba ako mbona humtaji aliporuhusu issue ya Serikali tatu enzi zile ijadiliwe bungeni? Isingekuwa vile leo ungekuwa na wewe unachezea Tausi Ikulu pale coz kutofautiana na Nyerere ndo kulimponza mzee wetu
 
Hivi kuna VITI MAALUM kwa ajili wa "wa kiume"? Kama vipo no doubt huyu jamaa atapata!!!!!
 
- Leo nimejionea kwa macho na masikio yangu Wabunge wanaomkumbuka Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, sikutegemea kua bado tuna Wabunge wenye Uzalendo wa kukumbuka tulikotoka hili Taifa. Kumbe bado tunao Wabunge wenye uchungu na Taifa letu, kumbe bado tunao Wabunge wenye kuelewa kwamba Duniani hakuna Serikali ya Jamhuri yenye Marais 3. - Warioba alipoteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Rasimu aliapa kwa kiapo kile kile cha Jamhuri, kwamba ataulinda Muungano kwa akili zake zote na nguvu zake zote, aliapa viapo hivi maisha yake yote mbele ya Mwalimu muasisi wa Muungano, sasa leo Mwalimu hayupo Warioba amebadilika hataki tena Muungano, halafu kibaya hajawahi kusema hadharani kuwa Mwalimu was wrong na Muungano, halafuhajawahi kutuambia hili Taifa kwamba huko nyuma alikuwa anaunga mkono Muungano na sasa hautaki, ila aemjificha ficha nyuma ya Rasimu na kutaka kupenyeza agenda yake ya kisaliti, bravo wabunge wangu leo nimejisikia vizuri sana na hasa imenikumbusha zile enzi za JKT nilipokuwa Oljoro Arusha kwenye "OPERATION TEKELEZA", - JAMANI WALE WOTE KAMA WARIOBA MNAOTAKA KUVUNJA MUUNGANO SUBIRI SISI WOTE TULIOPITIA JKT TUSIWEPO, NDIO MTAPITISHA UPUUZI WENU WA KUVUNJA KILA KITU: WARIOBA ALIKUW WAZIRI MKUU NA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS ASIYETAKA MUUNGANO LAKINI HAKUSEMA HATA SIKU MOJA, ANAKUJA KUSEMA LEO TENA KWA KUJIFICHA NYUMA YA PAZIA LA RASIMU YA KATIBA, LEO AMEJIONEA MWENYEWE KWAMBA SIO WABUNGE WOTE NI SAWA WALE WANANCHI ALIOKUWA ANAWABURUZA KWENYE VIKAO VYAKE KULE MIKOANI. - KUTAKA SERIKALI 3 NI KUVUNJA MUUNGANO KWA KIONGOZI YOYOTE WA TAIFA ALIYEAPISHWA NA RAIS KUDAI HAYA NI USALITI, HENGERENI SANA WABUNGE WOTE MLIOSIMAMA KIDETE LEO, MTALIPWA NA MUNGU WA MBINGUNI TU WARIOBA NA KUNDI LAKE MTALIPWA HAPA HAPA DUNIANI KWA KUTAKA KUTUVURUGA SISI WANANCHI WA TANZANIA, MSHINDWE NA MLEEEGEEEE WOTE WASALITI WAKUBWA WA MWALIMU BABA WA TAIFA!! Le Mutuz

Sina kawaida ya ku-quote taarifa ndefu kama hii yako lakini imenibidi. Naona kabisa udhaifu wako. Kwa nini unalazimisha mawazo yako yawe ndo wazomeaji? Umewaona wanaozomeya au ni kitu gani kichwani?

Sababu uliyotaja haikuwa bungeni leo kabisa. Naamini una rafiki au marafiki wanaoweza kukusimulia mara ya pili. Tatizo ni kukiuka kanuni, kutengua kanuni ambayo imemruhusu Warioba kusoma rasimu kabla ya hotuba ya Rais. Sasa hapo uzalendo umeanzia wapi? Udhaifu unaweza kuwa ni wa Mwenyekiti, anaonyesha umwamba usiokuwa na sababu, madaraka na kujinadi busara bila mipaka.

Hili Bunge linahitaji mwenye uwezo wa kufikiri siyo mzoefu tu ambaye ana sifa ya kukumbuka aliyokuwa akifanya miaka yote.

Tusiendelee kuambiwa mambo ya baba wa Taifa, baba mpaka lini? Mbona hutamani Azimio la Arusha kiasi hicho? au ktk mambo ya maana ni muungano tu! Nilitamani sana kuona CV yako maana kumbe sasa tuko hatarini, kila tunachotaka kufanya mtu anaibuka na kusema 'baba wa Taifa', so what? Ni simba kwamba atatung'ata kama lugha ya kitoto inayotumika? Tangu alipokufa sisi tuache kufikiri utadhani alifariki na ubongo wetu!
 
You are less informed, kumbe hata kinachoendelea hujui.

Achana naaye huyo mbaba, kwani alichoandika nimekipitia mwanzo mwisho sijui ameandika nini na sijui alikuwa anangalia Tv gani....
 
Naomba uniambie faida tatu tu za huu muungano wa tembo na huyu sisimizi mnyonyaji.

Mkuu naona unatekeleza kwa vitendo ile kauli mbiu yako ya Taifa kwanza vyama baadae. Yani kama tulivyoungana JF members wote kum-support JK kwenye bifu lake na Kagame, na sasa tumeungana tena kwenye Katiba ya nchi yetu.

My note kwa Le mutuz: Wakati ukuta usijaribu kupigana nao
 
Yumezoea kupewa na uongozi watu waliofanya vizuri kwenye jukwaa.Napendekeza tupewe poll ya kumtafuta Flop of the forum ili ashushwe kwenye jukwaa milele!
Kwa kuanzia my flop/kilaza of the Jukwaa la siasa is W:Malechela.
 
- Leo nimejionea kwa macho na masikio yangu Wabunge wanaomkumbuka Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, sikutegemea kua bado tuna Wabunge wenye Uzalendo wa kukumbuka tulikotoka hili Taifa. Kumbe bado tunao Wabunge wenye uchungu na Taifa letu, kumbe bado tunao Wabunge wenye kuelewa kwamba Duniani hakuna Serikali ya Jamhuri yenye Marais 3. - Warioba alipoteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Rasimu aliapa kwa kiapo kile kile cha Jamhuri, kwamba ataulinda Muungano kwa akili zake zote na nguvu zake zote, aliapa viapo hivi maisha yake yote mbele ya Mwalimu muasisi wa Muungano, sasa leo Mwalimu hayupo Warioba amebadilika hataki tena Muungano, halafu kibaya hajawahi kusema hadharani kuwa Mwalimu was wrong na Muungano, halafuhajawahi kutuambia hili Taifa kwamba huko nyuma alikuwa anaunga mkono Muungano na sasa hautaki, ila aemjificha ficha nyuma ya Rasimu na kutaka kupenyeza agenda yake ya kisaliti, bravo wabunge wangu leo nimejisikia vizuri sana na hasa imenikumbusha zile enzi za JKT nilipokuwa Oljoro Arusha kwenye "OPERATION TEKELEZA", - JAMANI WALE WOTE KAMA WARIOBA MNAOTAKA KUVUNJA MUUNGANO SUBIRI SISI WOTE TULIOPITIA JKT TUSIWEPO, NDIO MTAPITISHA UPUUZI WENU WA KUVUNJA KILA KITU: WARIOBA ALIKUW WAZIRI MKUU NA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS ASIYETAKA MUUNGANO LAKINI HAKUSEMA HATA SIKU MOJA, ANAKUJA KUSEMA LEO TENA KWA KUJIFICHA NYUMA YA PAZIA LA RASIMU YA KATIBA, LEO AMEJIONEA MWENYEWE KWAMBA SIO WABUNGE WOTE NI SAWA WALE WANANCHI ALIOKUWA ANAWABURUZA KWENYE VIKAO VYAKE KULE MIKOANI. - KUTAKA SERIKALI 3 NI KUVUNJA MUUNGANO KWA KIONGOZI YOYOTE WA TAIFA ALIYEAPISHWA NA RAIS KUDAI HAYA NI USALITI, HENGERENI SANA WABUNGE WOTE MLIOSIMAMA KIDETE LEO, MTALIPWA NA MUNGU WA MBINGUNI TU WARIOBA NA KUNDI LAKE MTALIPWA HAPA HAPA DUNIANI KWA KUTAKA KUTUVURUGA SISI WANANCHI WA TANZANIA, MSHINDWE NA MLEEEGEEEE WOTE WASALITI WAKUBWA WA MWALIMU BABA WA TAIFA!! Le Mutuz

Msomi mzima umechukua muda mrefu kuandika kitu kidogo tu na ueshindwa kueleweka.........unafikiri ni akili za wale watu wako ndio zimesababisha Walioba asitoe hutuba? Unajua chanzo ni nini soma hapa acha kubeba mwili tu....https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...anzo-cha-bunge-kuahirishwa-2.html#post8981561
 
Kweli nimeamini ukiona mtu analia au anapiga kelele kila mtu aweza kuja na tafsiri Yake maana hajui sababu ya Sauti itokayo. Ndivyo ilivyotokea bungeni na huyu mtu ameamua kupotosha. Sababu ni mwenyekiti wa bunge sitta kukiuka kanuni Za bunge maalum na si Kama asemavyo huyu mwana CCM mvivu wa kutafuta uhalisia.
 
Wacha ujinamizi ,hivi kwa akili zako haya au hyo rasimu ni mawazo ya Warioba ? zimepita tumengapi kuhusiana na Muungano na zote zimekuja na serikali tatu ,kwa aliyoyakusanya Warioba si mageni kwa Watanzania ,wewe kama unafaidika na urithi ambao hutokana na jasho la walala hoi ,one day yes itawatoea puani jasho lao ,baba kadhulumu na watoto nao pia wadhulumu ,kwa taarifa yako Tanganyika ya leo ni tofauti na ile waliyoiacha wazee wenu ,kama Uccm karibu WaTz wote walikuwa CCM.

Msiwe malimbukeni na hapo bungeni kilichopingwa ni hujuma za CCM na ndio hivyo zimepingwa na mliyoyapanga hayakuwa ,pole sana unasifu usichokifahamu.

Sasa jipimeni vizuri sana ikiwa hapo mmetulizwa je huko kunakoelekewa ? Na huo ujeshi unaojilabu nao ,sidhani kama utamtisha mtu kwani zama za kutishana zimepitwa na wakati UJKT!!! watu wana UJWTZ wametulia tuli . Heshima mliokuwa mkipewa mmeipoteza na haitorudi tena ,Muungano utajadiliwa na serikali tatu ndio hitimisho vyenginevyo mtakufa na donge la roho.
 
Back
Top Bottom