My Story..

My Story..

Nililia eti ananibembeleza mwanaharamu yule!!!Basi nikajikongoja akanisondikiza like nachechemea ..Enzi hizo hakuna magari mengi kutoka hiko chuo mpka barabarani...basi ghafla njiani mvua ikaporomoka kama yote nikalowa hatari....mpka nafika stand nimeloa chapachapa...na machozi yamekauka!
Baada ya wk narudi shule ndyo tunajiandaa na mitihani ya Taifaya advance.Kusoma hakusomeki huko shuleni tafrani...Nawaza nimeachika Tena mara kwanza Nakutana na mwanaume!!!ila najipa moyo Nina Miaka 18.Nikaa nafeli feli muda waote. Nakuwaza Mangiii...Sasa kabla ya kwenda shule Kuna mtu alinitonya jamaa baada ya pale anaaply chuo kikuu..Ile kauli nikaifanyia kazi..Nikjisemea nikfel ataniona Boya sana ..Ngoja nisome tkutane kwenye hizo ngazi za chuo..Nikaacha kufikiria hayo mambo kabisaaa....Siku moja kabla ya mtihani jamaa ananipigia simu njia za magendo best wishes...
Mitihani ilipita Vyema..Nikafanya Vyema nikafaulu(Mkasa wa mtihani sitausimulia itafanya Mimi ajulikane)
 
Mungu si athumani!!Nikadahiliwa chuo kinachoitwa kikubwa Afrika Kiko Tanzania(hahahahaha msinipopoe)..

Hapo nishasahau mambo ya usister,nimepata kibwana kinasoma IFM.Huyu alijua kinipeleka mpka nikinya nataja jina lake.Huyu tuliishi nae mtaa wa Tabata relini Kwa mama Mdogo.So kila Wkend lazima nirudi home tuonane..Bwana huyu hakupta boom Kwa wakati basi alivyopata Boom niliona Kila aina vituko..Alijua kuutia nyongo hasa moyo.Kwangu Kila mwanaume aliyenijia alijua Nina mchumba IFM.

Ikafika kipindi kuonana shida utaweka vocha hata ya elfu Tano muwasiliane kabla ya vifurushi!!Kumbe kazuzuka na kabinti kengine huko...Enzi hizo nami nilikuwa mzuri wa Sura si Jana
.japo sikuwa na nyama za kuwafanya wanaume wenye tamaa watoke udenda.
Mpka kufika second year...Nilikuwa mekonda...Nikakutana na feminist wanaosoma Literature wakanipa lecture kuhusu ufeminist nikasema ahsanteni dada zangu.Hili Penzi Sasa akiweka pilau naweka kachumbari...akiweka uji natia chumvi.
 
Inaedelea
Sasa Kuna muda Mzee akaumwa sanaaa...ile kuumwa...basi akapelekwa hospitali wakarudi.Sasa nikaagizwa kitu chumbani kwao nilete naona kijicheti. positive...Moyo ukaenda pa pa pa pa pa!!!Nikavurugwa kabisa...Nokapeleka nolichoagizwa..Nikakaa nayo moyoni...Nikawa najiuliza status ya mama yangu ikoje...Nikawachukia wanaume wote ghafla..

Ghafla tuu nikawa Nina chuki na visasi na wanaume!!!Nzuri dawa hizi zilikuwa zishaanza kuingia...Mzee akaendelea na Hali nzuri kama awali.Tukahamia nyumba yetu nyingine.Mzee alijenga.Nikawa nasoma sana.Mm nilikuwa wa kwanza kufika chuoni.Hali hii lilivuruga sana nikiwaangalia wadogo zangu!
Chuo Nilimaliza nikiwa na ndoto nyingi sanaaa!!Maisha ya home yalitengamaa Kila kitu kikaa sawa!Tulipomaliza chuo zilitokea nafasi nyingi nilipofuatilia ili nipate tracript niliambiwa Nina deni la ada!!

Kuna kipindi mgomo ulitokea chuoni hivyo muhula wa masomo ulihairishwa..Tuliporudi tulitakiwa kulipa pesa zote..Kumbe kwangu hawakuandika ada sahihi.Ikaja kuonekana nilipomaloza...Wazee walikataa kuilipa..Nikitafuta kibarua kupata pesa..Nafasi zilinipita...ila nikipata pesa Nikalipia transcript.

Siku moja nikiwa kazini ni kiwanda cha kinywaji nikaanza kuona mashine mbilimbili..Mashine moja naona mbili.Mtu mmoja naona wawili...Hali hyo ilinifanya nishindww kusimama vyma na kuipapasa ukuta.Walinisaidia kinitoa nje.Baada ya wk moja nilosimamishwa kibaruani pasipo sababu ya msingi.Kibarua kikaoshia hapo!!!!(sitataja position ya kazi)
 
Nikaanza kuhangaika mtaani tena...nikapata ishu ya utafiti kampuni Moja hivi..Miezi mitatu.. Hapo maumivu ya kuachwa nikaoka kabisa Nyiee hahahhaha....Nikajua kupata kazi kampuni Moja ya simu za mkononi(jina kapuni)hapo nikaona mbingu kama zinafunguka kumbe ndyo zinafunga!!!
Siku moja nikiwa kazini ghafla nikaona wadudu weusi tii wengi jamani nikaishiwa nguvu nikazima...Niko hospitali nikaambiwa niende Kwa maombi.
Nikapanda gari mwenyewe mpka Kwa maombi..Kufika kule Nako nikazimia...kuamka sauti yangu imepotea Nyiee!!!!Nikikaa wk Tatu ndyo ikarudi...Naenda kazini haitoki ...nikiwa home ipo...Hapo Kuna kapromo nilipta..Kazi nikaacha nikaamua nikasomee fani nyingine.


Mzee akapta ajali mbaya sana..akapalalaizi kabisa...Maisha yakawa shida home...ukisikia Kula mahindi ya kuchemsha mpka jioni...Kupika Kuni...Kula mara Moja...Sijawahi experience maisha hayo toka utotoni....(sihadithii sana...naficha uhalisia)..Nyumbani ikawa ugomvi ugomvi...Amani ikaisha kabisa...Kila siku wazee wanagombana hatujawahi shuhudia toka tuzaliwe..Hapo Mzee bado mgonjwa.
Ndyo nikapta kazi mahala.(Tarime).Kidogo wanalipa...Nikawa sisahau home...Nyie nikaanza ona maluwe luwe Kila iitwayo Leo...Mara wamemwaga maji..Mara nimekatwa katwa.....Nikila chakula hakipiti..Nikakonda nikaisha..Ukikaa unatembelewa na wadudu usoni huwaoni...Vitu vinatembea...Noliishi Kwa shida takribani mwaka mmoja.
 
Back
Top Bottom