Hapo kidogo nikaakaa home ndyo nikaanza kuona tofauti .Kwanza siku moja nikaona kopo la Arvs sijawahi yaona home yakiwepo lakini siku hyo lilikaaa karibu na mlango wangu kama masaaa kadhaa.Nami nikakausha siyajui.
Nina mdogo wangu alikuwa amemaliza chuo akaanza kunihadithia mambo ya Mzee toka amepona anahisi Mzee na mama washirikina ila wanaficha.Nikamwambia hamna..Huyo mdogo wangu mseminari alikuwa anasali sali.Akasema Mzee alikuwa anakuambia hafiki mbali ataona na BLA BLA nyingi!!Mm sikumuamini.Mara dogo akaanza kubadilika akawa kama anawehuka Kila mtu anamuona mchawi yaani hata aje mgeni.Peleka Kwa maombi wapi!Sitaki simulia yake ila mpka Leo hajapona...anaonaonaga vitu vitu ambavyo havieleweki.
Mdogo wangu aliponieleza hayo kama akili ilianza funguka..Nikawa naanza kukumbuka matukio ya nyuma mm na mama.Nikipata kazi mm na mama tulikuwa hatuelewani kabisa.Kazi za mwanzo nauli nilikuwa napata Kwa binamu zangu.Nilikuwa nikiwa na usingizi ndyo anakuja anaanza kaniambia habari habari.Kuna muda nimelala atasimama na kuniangaliaaa sanaaa.Niliona kawaida.Lakini nilipookoka Kwa kipindi hiko niliona ni tofauti sana wa hivi visa.Nilimshirikisha Mzee na yeye akiwepo.Ilikuwa ni kosa kubwa.Kwa kipindi kile niliona ni kawaida maana tulikuwa na Upendo na umoja sana Na Mzee alikuwa mshauri.Niliyakumbuka matukio yote ya nyuma.
Siku moja nikawauliza wazazi Kwa nini haya mambo yanatupata sisi tuliosoma wenzetu mbona hawana?Wakatupa majibu mazuri ambayo usingeweza kuendelea kuhoji tunayoyapitia.
Likizo ya uzazi iliisha salama sijawahi muelewa mtu yeyote habari za wazazi wangu.Kila nikisali nawaombea wawe na amani.Niliporudi kazini ile Hali ya kutengwa kwenye mambo mbalimbali ilikomaa.Nikaona Bora nimpate mshauri wa kiroho.Huyoo Nikaenda kanisani.Nikakutana na fadha mmoja.Nikaongea nae kumtaka ushauri..Akaniuliza historia ya kwetu.Toka nazaliwa sijawahi msikia mama anapasema vibaya kwao au ndugu Zake.Hutuhadithia ya upande wa baba.Nikahadithia ninayoyajua.Ukoo wetu ni wale walioupokea ukatoriki mwanzo mwanzo...hivyo una makuhani wa kutosha na wavaa vilemba wengiii.Basi nikawa nimetua mzgo nisijue ndyo nimeyachokoza!!!!
Yule fadha aliumwa Nyiee....akarudishwa kwao.Mimi nikapita Kwa magumu kazini nikasingiziwa kesi nikafukuzwa kazi kipindi Cha korona.Nikarudi kwetu Nina mtoto mdogo.Home nikaomba nikae nyumba ndogo Kuna wapangaji ila Kuna chumba kimoja kopo free nikakaa.Ghafla nikiwa natembea nasikia kama watu wananisema..Nikawa napuuzia hizo sauti..Akaja mama mmoja akasema Nina laana ya mama yangu.Ndyo maana nimerudishwa kazini.Siku nuingineakaniambia nimeathirika .Lile likaniuma nikamueleza mama yangu ananiambia aliniambia niskae na wale wapangaji wana maneno kwanza yule mwanamke ni mshirikiina.Nikanyamaza kimya,mama akaenda kuwauliza wakaruka kimanga.Siku moja umeme ukakata nikatakiwa kuchangia umeme..Nikawaambia nachangia ila hawajanipa taratibu.Huyo mpangaji Acha aanze kunigimbeza Kwa nguvu.Nikaingia ndani nikaanza kusalimia.Hapo bado nasali nasali Kwa nguvu nikalia.Sijui nikasema wanatka wanifanye chizi Mzee alitoka na bakora nikachapwa..Nikakimbilia Kwa shangazi yangu jirani
Baada ya muda mm nilihama home kabisa.Nikaenda panga sehemu nyingine..Nikaa kama miezi SITA nikapata Kazi mkoa mwingine.Mshahara mzuri kuliko nilikotokea.Kumbe sikujua kama Kilemba kimeloa,mkuti u Hali Gani?
Nikaanza kazi Tena...mtoto nikamrudisha home..Nikafanya kazi Kwa bidii zote. Home sijawaambia nafanya kazi wapi.Basi mi kilanga siku moja nikamuambia ndugu yangu mm nimepata kazi,sehemu nzuri mshahara mzuri.akawa ananipa michapo ya home mama anavyomlalamikia baba mambo ya ushirikina.Mm nikamwambia hao itakuwa wanajuana wenyewe.Kuna mtumishi aliniambia mama alienda akapandwa mapepo akasema baba sijui anachezea.Kuna mtumishi tulienda na mama wakasema Kuna ndugu yake baba sijui anatuchezea.Mm siamini maneno ya watumishi shida watakuwa nayo.Ndugu yangu akawa analalamika kama tunasali mbona hayo mambo hayaishi .Akamtaja ndugu yangu anayesali yule mseminari...Akasema Hali mbaya wanamuita mchungaji aje aombewe.Basi si nikamshirikisha ndugu yangu huyo kuhusu status za wazazi wangu!!
Nilikaaa kwenye mji ule wenye bandari kongwe takribani miezi sita.Nikaanza Sikia sauti nikiwa natembea Kwa mbali sana.Siku moja usiku kama saaa saba baada ya kumaliza kuongea na simu.Nikaanza Sikia sauti zinaongea dirishani kwangu.Nikafungua dirisha nauliza hamjalala?Nilijua ni wapangaji wenzangu!!!Toba!!Dirishani hamna mtu.Narudi kitandani mwangu sauti za vitisho zinaongezeka.Nachukua biblia yangu.Nikaambiwa sijakariri...Nikisema sauti zinasema uongo!!!Nikasali usiku kucha!!Pasipo kulala .Sauti hazikuisha...Woga ukanivaa..Hofu ikanitanda.Nikienda kuoga wanasema wapo bafuni!!!Nyiee sikieni hyo Hali!!!
Asubuhi hii hapa.Ungama dhambi zangu zote!Sauti hola!Nikifika kazini nikaomba ruhusa.Niko kwenye gari.Vitisho vinaongezeka.Sasa nikawa naona wanaosema ni wale wa kwenye gari.Nashuka ndani ya gari.Napanda lingine..Mpaka nafika safari yangu nilikuwa Niko nusu mtu nusu hayawani.
Natafuta mtumishi wa Mungu ananipa neno naombewa.Sauti wapi zipo Nami!!Simu imezima charge hakuna anayejua nilipo..Napuyanga tu mjini.Naona vivuli vya ndugu zangu .Napanda gari nawekewa recording ya ndugu zangu wanayoongea nyumbani..Naanza poteza balansi.Nikazurura mpka usiku.Nikaamua kupanda gari kurudi nilikotokea.Nikaghairi kurudi nyumbani.Nikiwa Kwa gari nikaona nishuke tu Nikaenda Kwa ndugu yangu mmoja upande wa baba.Nilale.Nafika sauti zinazidi..Nikitoka kulala zinanitishia kunivua.Nikaanza kujibizana nazo mpka asubuhi.Siku ya pili sijalala!Nikaanza kuona vimvuli vya ndugu zangu wanakiri makosa Yao.Naongea kama mwehu Sasa.Ndugu yule akanishauri nirudi nyumbani.Ikabdi kufungua safari y kurudi nyumbani.
Njiani namuona mtu anakuja kabisa ila kama amebeba kisu.Akinikaribia Hana kitu.Nafika home usiku Kwa sababu ya kuchoka.Naanza kibishan nao upya.Sikulala Tena.Jamani msiniulize kuhusu kula sikumbuki kama nilikuwa nakula au nakojoa.
Asubuhi nasali na kuomba...Akili imevurugika.Naona watu w kazini wananitishia kuniua.Nikirudi kazini.(Sohadithii sana..italeta uhalisia)
Jioni napelekwa hospitalini..Kufika nikaambiwa nijieleze..Nakumbuka nilimuambia Daktari kuwa natka kulala basi.Nimechoka lakini silali!!
Turudi nyuma,Niliporudi nyumbani niliona kama ndugu zangu wananing'ong'a ili pia lilinitia Hofu.Hivyo nikawa niliona kile kitendo nawapiga .Wakataka kunifing kamba.
Hapo hospitali kulikuwa na tv..nikawa naona matangazo tofauti na Yale..Nilikuwa naona matangazo ya kuathirika tu na matumizi ya dawa.Na kelele za honi za treni nisizozilewa.
Tulipotoka hospitali nikawa napewa dawa nilizopewa.Sauti zinasema ni za kuathirika na mm hulia na kupiga kelele kuwa sijaathirika.Nikawa nafungwa kamba ili nipewe dawa.Ndyo nikaanza kulala.Ila nikiamka najibizana na sauti.Au husali Kwa sauti kubwa kama mchungaji.Siku moja asubuhi nilibeba mtoto wangu nikapita mtaani na kutaja majina yangu kisha nasema nimeathirika.
Niliumaliza mtaa ninaokaa,Nikaja kamatwa wakanifunga kamba nikarudishwa home.Nikapewa dawa za kusinzia nikalala.Baada ya wk mbili kupiga nikawa Sasa naelewa. Hali kama ya usingizi ikaishia.Zikabkia sauti kwa mbali sana.
Nikaacha kuongea nikawa nasoma neno tu.Niliporudi katika Hali ya kawaida nikaacha kabisa kuwawazia wazazi vibaya.Maisha yakasonga.Kule kazi niliacha.Nikaona nipumzike!