My Story..

My Story..

Hapo kidogo nikaakaa home ndyo nikaanza kuona tofauti .Kwanza siku moja nikaona kopo la Arvs sijawahi yaona home yakiwepo lakini siku hyo lilikaaa karibu na mlango wangu kama masaaa kadhaa.Nami nikakausha siyajui.

Nina mdogo wangu alikuwa amemaliza chuo akaanza kunihadithia mambo ya Mzee toka amepona anahisi Mzee na mama washirikina ila wanaficha.Nikamwambia hamna..Huyo mdogo wangu mseminari alikuwa anasali sali.Akasema Mzee alikuwa anakuambia hafiki mbali ataona na BLA BLA nyingi!!Mm sikumuamini.Mara dogo akaanza kubadilika akawa kama anawehuka Kila mtu anamuona mchawi yaani hata aje mgeni.Peleka Kwa maombi wapi!Sitaki simulia yake ila mpka Leo hajapona...anaonaonaga vitu vitu ambavyo havieleweki.

Mdogo wangu aliponieleza hayo kama akili ilianza funguka..Nikawa naanza kukumbuka matukio ya nyuma mm na mama.Nikipata kazi mm na mama tulikuwa hatuelewani kabisa.Kazi za mwanzo nauli nilikuwa napata Kwa binamu zangu.Nilikuwa nikiwa na usingizi ndyo anakuja anaanza kaniambia habari habari.Kuna muda nimelala atasimama na kuniangaliaaa sanaaa.Niliona kawaida.Lakini nilipookoka Kwa kipindi hiko niliona ni tofauti sana wa hivi visa.Nilimshirikisha Mzee na yeye akiwepo.Ilikuwa ni kosa kubwa.Kwa kipindi kile niliona ni kawaida maana tulikuwa na Upendo na umoja sana Na Mzee alikuwa mshauri.Niliyakumbuka matukio yote ya nyuma.

Siku moja nikawauliza wazazi Kwa nini haya mambo yanatupata sisi tuliosoma wenzetu mbona hawana?Wakatupa majibu mazuri ambayo usingeweza kuendelea kuhoji tunayoyapitia.

Likizo ya uzazi iliisha salama sijawahi muelewa mtu yeyote habari za wazazi wangu.Kila nikisali nawaombea wawe na amani.Niliporudi kazini ile Hali ya kutengwa kwenye mambo mbalimbali ilikomaa.Nikaona Bora nimpate mshauri wa kiroho.Huyoo Nikaenda kanisani.Nikakutana na fadha mmoja.Nikaongea nae kumtaka ushauri..Akaniuliza historia ya kwetu.Toka nazaliwa sijawahi msikia mama anapasema vibaya kwao au ndugu Zake.Hutuhadithia ya upande wa baba.Nikahadithia ninayoyajua.Ukoo wetu ni wale walioupokea ukatoriki mwanzo mwanzo...hivyo una makuhani wa kutosha na wavaa vilemba wengiii.Basi nikawa nimetua mzgo nisijue ndyo nimeyachokoza!!!!

Yule fadha aliumwa Nyiee....akarudishwa kwao.Mimi nikapita Kwa magumu kazini nikasingiziwa kesi nikafukuzwa kazi kipindi Cha korona.Nikarudi kwetu Nina mtoto mdogo.Home nikaomba nikae nyumba ndogo Kuna wapangaji ila Kuna chumba kimoja kopo free nikakaa.Ghafla nikiwa natembea nasikia kama watu wananisema..Nikawa napuuzia hizo sauti..Akaja mama mmoja akasema Nina laana ya mama yangu.Ndyo maana nimerudishwa kazini.Siku nuingineakaniambia nimeathirika .Lile likaniuma nikamueleza mama yangu ananiambia aliniambia niskae na wale wapangaji wana maneno kwanza yule mwanamke ni mshirikiina.Nikanyamaza kimya,mama akaenda kuwauliza wakaruka kimanga.Siku moja umeme ukakata nikatakiwa kuchangia umeme..Nikawaambia nachangia ila hawajanipa taratibu.Huyo mpangaji Acha aanze kunigimbeza Kwa nguvu.Nikaingia ndani nikaanza kusalimia.Hapo bado nasali nasali Kwa nguvu nikalia.Sijui nikasema wanatka wanifanye chizi Mzee alitoka na bakora nikachapwa..Nikakimbilia Kwa shangazi yangu jirani
Baada ya muda mm nilihama home kabisa.Nikaenda panga sehemu nyingine..Nikaa kama miezi SITA nikapata Kazi mkoa mwingine.Mshahara mzuri kuliko nilikotokea.Kumbe sikujua kama Kilemba kimeloa,mkuti u Hali Gani?

Nikaanza kazi Tena...mtoto nikamrudisha home..Nikafanya kazi Kwa bidii zote. Home sijawaambia nafanya kazi wapi.Basi mi kilanga siku moja nikamuambia ndugu yangu mm nimepata kazi,sehemu nzuri mshahara mzuri.akawa ananipa michapo ya home mama anavyomlalamikia baba mambo ya ushirikina.Mm nikamwambia hao itakuwa wanajuana wenyewe.Kuna mtumishi aliniambia mama alienda akapandwa mapepo akasema baba sijui anachezea.Kuna mtumishi tulienda na mama wakasema Kuna ndugu yake baba sijui anatuchezea.Mm siamini maneno ya watumishi shida watakuwa nayo.Ndugu yangu akawa analalamika kama tunasali mbona hayo mambo hayaishi .Akamtaja ndugu yangu anayesali yule mseminari...Akasema Hali mbaya wanamuita mchungaji aje aombewe.Basi si nikamshirikisha ndugu yangu huyo kuhusu status za wazazi wangu!!

Nilikaaa kwenye mji ule wenye bandari kongwe takribani miezi sita.Nikaanza Sikia sauti nikiwa natembea Kwa mbali sana.Siku moja usiku kama saaa saba baada ya kumaliza kuongea na simu.Nikaanza Sikia sauti zinaongea dirishani kwangu.Nikafungua dirisha nauliza hamjalala?Nilijua ni wapangaji wenzangu!!!Toba!!Dirishani hamna mtu.Narudi kitandani mwangu sauti za vitisho zinaongezeka.Nachukua biblia yangu.Nikaambiwa sijakariri...Nikisema sauti zinasema uongo!!!Nikasali usiku kucha!!Pasipo kulala .Sauti hazikuisha...Woga ukanivaa..Hofu ikanitanda.Nikienda kuoga wanasema wapo bafuni!!!Nyiee sikieni hyo Hali!!!

Asubuhi hii hapa.Ungama dhambi zangu zote!Sauti hola!Nikifika kazini nikaomba ruhusa.Niko kwenye gari.Vitisho vinaongezeka.Sasa nikawa naona wanaosema ni wale wa kwenye gari.Nashuka ndani ya gari.Napanda lingine..Mpaka nafika safari yangu nilikuwa Niko nusu mtu nusu hayawani.
Natafuta mtumishi wa Mungu ananipa neno naombewa.Sauti wapi zipo Nami!!Simu imezima charge hakuna anayejua nilipo..Napuyanga tu mjini.Naona vivuli vya ndugu zangu .Napanda gari nawekewa recording ya ndugu zangu wanayoongea nyumbani..Naanza poteza balansi.Nikazurura mpka usiku.Nikaamua kupanda gari kurudi nilikotokea.Nikaghairi kurudi nyumbani.Nikiwa Kwa gari nikaona nishuke tu Nikaenda Kwa ndugu yangu mmoja upande wa baba.Nilale.Nafika sauti zinazidi..Nikitoka kulala zinanitishia kunivua.Nikaanza kujibizana nazo mpka asubuhi.Siku ya pili sijalala!Nikaanza kuona vimvuli vya ndugu zangu wanakiri makosa Yao.Naongea kama mwehu Sasa.Ndugu yule akanishauri nirudi nyumbani.Ikabdi kufungua safari y kurudi nyumbani.

Njiani namuona mtu anakuja kabisa ila kama amebeba kisu.Akinikaribia Hana kitu.Nafika home usiku Kwa sababu ya kuchoka.Naanza kibishan nao upya.Sikulala Tena.Jamani msiniulize kuhusu kula sikumbuki kama nilikuwa nakula au nakojoa.

Asubuhi nasali na kuomba...Akili imevurugika.Naona watu w kazini wananitishia kuniua.Nikirudi kazini.(Sohadithii sana..italeta uhalisia)
Jioni napelekwa hospitalini..Kufika nikaambiwa nijieleze..Nakumbuka nilimuambia Daktari kuwa natka kulala basi.Nimechoka lakini silali!!

Turudi nyuma,Niliporudi nyumbani niliona kama ndugu zangu wananing'ong'a ili pia lilinitia Hofu.Hivyo nikawa niliona kile kitendo nawapiga .Wakataka kunifing kamba.

Hapo hospitali kulikuwa na tv..nikawa naona matangazo tofauti na Yale..Nilikuwa naona matangazo ya kuathirika tu na matumizi ya dawa.Na kelele za honi za treni nisizozilewa.

Tulipotoka hospitali nikawa napewa dawa nilizopewa.Sauti zinasema ni za kuathirika na mm hulia na kupiga kelele kuwa sijaathirika.Nikawa nafungwa kamba ili nipewe dawa.Ndyo nikaanza kulala.Ila nikiamka najibizana na sauti.Au husali Kwa sauti kubwa kama mchungaji.Siku moja asubuhi nilibeba mtoto wangu nikapita mtaani na kutaja majina yangu kisha nasema nimeathirika.
Niliumaliza mtaa ninaokaa,Nikaja kamatwa wakanifunga kamba nikarudishwa home.Nikapewa dawa za kusinzia nikalala.Baada ya wk mbili kupiga nikawa Sasa naelewa. Hali kama ya usingizi ikaishia.Zikabkia sauti kwa mbali sana.
Nikaacha kuongea nikawa nasoma neno tu.Niliporudi katika Hali ya kawaida nikaacha kabisa kuwawazia wazazi vibaya.Maisha yakasonga.Kule kazi niliacha.Nikaona nipumzike!
 
Duh! Pole sana kwa uliyopitia mkuu. Kumbe mbaya wako ni yule unaeishi nae.
 
Nilikaa nyumbani sana.Nikaanza kusoma nakala za kitabibujinsi ya kujitibia tatizo la audio hallucinations.Nikaanza kunifanyia kazi ili kicopy na mazingira.Hapo naenda Kwa maombi Hadi Kwa Mzee wa upako nikafika.Atlist nikaanza kuzielewa sauti.. ukiwa na hofu zinazidi.Kuna kipindi ziliisha kabisa.Ila siku moja tulikosana na mama yangu kuhusu maji.Jamani Mwenzenu zilirudi Tena.Hali ikarudi upya.Kila ninachofanya hutolea maoni.Nikahangaika na hyo Hali mpka nikajua kicopy nayo.Nilipojua kucopy nayo nikatafuta kazi Tena.
Nikapta kazi..Mzee ananiambia kazi umepata..ila haitadumu kokote utakakoenda utakorofishana na watu.Nikamuambia mm nimepona.

Hapo nikaadapt maisha ya kuishi kijinga.Mambo ya kuamini ushirikina nikaacha kichwani mwangu.Hata nimuone mtu Anafanya mambo yanayohusiwa na ushirikina nikawa I dnt care.Nasema ni illusion.So hii ilinisaidia Kwa muda.

Nikapata Kazi mahali,Maisha yakawa mazuri tu Kwa miezi nane.Sikuwa Napokea mshahara mkubwa.Kazi ilinifanya nitoke nyumbani Tena.Nikapanga mahali.Nikawa busy na mambo yangu.Sipigi stori za ushirikina wala sisikilizi chochote kinahusu ushirikina na uchawi.Hata humu stori za uchawi uchawi nikaacha kabisa kusoma.Ile Hali ilinifanya kuacha vitu nilivyovipenda kusoma vitabu,kusikiliza habari za siasank.Na ni kama mambo muhimu yalifutika akilini mwangu.

Hapo nilipopanga tulikuwa wapangaji wawili.Tunatazama vyumba vyetu.Huyu mpangaji alikuwa mmama ana watoto wakubwa tu wakumaliza kidato Cha nne.Tuliishi Vyema Kwa kuheshimiana Miezi Sita ya mwanzo.Ghafla tukaanza kukwazana .Kupitia Hawa nikajua mambo mengi sana!!Kwanza nikiwa kwangu wakawa wanawasema wazazi wangu.Wazazi wangu hawajawahi fika hapo Wala hawajawahi kuwa ona.Sehwmu ninayofanyia kazi ni mbali na eneo la nyumbani..Inachukua takribani masaa 3 au nne njiani.Stori walizokuwa wanasema ni za kweli mno.
Kama nilivyohadithia kuhusu masikio..muda mwingi walikuwa wanajua siwasikii.Mwanzoni nilidhani ni sauti lakini nilikaa kimya Kwa mwezi mzma nielewe kinachoendelea tukiwa tuankwazana wakawa wanaongea mambo ya kwetu Hadi wakamtaja Babu yangu mmoja alaishawahi fariki.

Ila mm nikasema hapa sihami,Siamini mambo ya ushirikina Tena.Nilikomaa kwenye ile nyumba mpka siku walipokuja kutaja jinsi wazazi wangu wanavyofanya kazi nyumbani na bro wangu anayeona maluemalue..Ndyo nikaona pale nimeyatimba!!!

Sadly,Mambo ya kusikia sauti yakafika sehemu ya kazi!Nikaanza kudhihakiwa flani na kutengwa Hata sijui nani aliyapeleka.Ghafla yakazagaa mtaani.Mm Nina kisauti.Hapo nimepona mzma.Hivyo mtu utaongea nae vizuri ila mwisho ataigiza kisauti anaongea Kwa sauti ndogo ndogo ili uamini ni kisauti.
Hawakujua kuwa nilikuwa nishazimasta hivyo sizisikii Kila mara.Kuna muda nilitukanwa kabisa.Then ukimuangalia mtu ana pretend sio yeye..Baada ya hyo kisauti kuenea matusi kwangu ilikuwa mboga..Lakini sikujibu.Sikutaka wajue ninasikia kiasi Gani.So mtu alipojifanyisha kisauti nikawa Nami najitia sijasikia!!
Nyie kamshahara kaka panda.Nikasma Sasa hivi Acha Nami nifanye maendeleo...Kila nipatapo kazi nawaza home ma mtoto.Ngoja ninunue nunue vitu.Nilikaa mwezi nyieee....Nikapewa suspension Kwa kosa la kusingiziwa!!!!

Nikarudi home,ndugu zangu wamefurahi hatari...Nikaakaa wiki ya kwanza ya pili...Nyie haya yanafanywa na watu wa kunizaa..Ndugu zangu wakaanza kunifanyia visa.Siku moja ndugu yangu akaweka kipimo Cha hiv positive mm nikakiona nikajifanya nimelala.Wakawa wanaongea huyu si Huwa angalia huyu...wakacheka Kwa nguvu!!!Nikiwa nimelala akaja ndugu yangu anajitia anaongea na simu kule umekimbia wachawi ss tutakuonyesha!!!Nikajua labda ananitisha tuu!!!Sasa nikawa najifanya sisikii sana ili nisikie mengi.Basi ndyo nikamsikia Mzee anasema lazima nikae mwaka home bila Kazi!!!
Huku mtaani wamewaambia mm jeuri...Chizi sitaki kutumia dawa.Hivyo nimerudi nyumbani Tena.Watu wanaamini coz nilijitambulisha mwenyewe!!

Siku moja ndugu yangu Akamuambia mama anitie stress na kule kung'ong'wa nang'ong'wa live sasa..Nikaja kigundua yale mabaya yote ninayofanyiwa kazini ni ndugu zangu.Na mtaani husema uongo.Kwamba sitoi hela nyumbani nikiwa kazini.Nakosa hata elfu kumi ya kutoa
Wazee wangu ni wale wa kwenda kanisani sanaaa..Hawakosi ibada ya asubuhi Kila siku.Kuna muda naamini ni illusion Kuna muda naona ni kweli!!

Hakuna yeyote anayeweza amini..Mwanzoni nilidhani ni fitina ya kukosanishwa kifamilia ila baada ya kurudi home Tena naona shida wanayo wazee wetu.Sisi tumesoma Mzee aliuza mpka Ng'ombe tuliofika chuo kikuu watatu na wote ni kuona maluwe luwe...Ambao wameishia form fofofo watatu maisha Yao hayana maluwe luwe...Bata kama zote....
Nikasema Mungu nisamehe nimehangaika vya kutosha...Naomba niishi Leo tuu!!Hivyo naishi Leo.Najipa furaha Leo!!Mtu aniseme asinisme shauri yake!!Kanisani nimepunguza spidi...Mara chache naenda Kwa Mwamposa...Mpka Sasa sijawahi enda Kwa Mganga..Sauti zipo sio za kichanganya akili..nimeona nikipambana sna ntapotea kama mwenzangu.Niko mbali na home nw nimeona nitapata stress..Sina kazi Wala nini...Kuna muda Naomba Kuna muda naona napoteza muda!!!ila nikiviangalia vyeti machozi yananitoka.Nikimuangalia mwanangu nasema y God have chosen me kunipa zawadi nzuri hii ije ihangaike na maswahiba yangu!!!Toba yallah!!!

Ni kama ukimueleza mtu anakuambia nenda hospital unaumwa akili!!!
Ushirikina upo...Ila mm pamoja na hayo nimegoma kuamini!!!!
Ndugu yangu mpka Leo anaongea ongea!!!
 
Dada...mimi pia nilikua nasikia Sauti kama zako. Lakini nilitibiwa mirembe....hospital ya rufaaa ya Magonjwa ya akili.

Kubali kuwa una ugonjwa wa akili....tafuta tiba... unaweza pata dawa nzuri ukamlea mwanao vizuri.....
Hakuna ushirikina hapo.... huo ni ugonjwa wa akili....hata mimi ninao
Sawa... soma habari nishaenda huko. nimeficha uhalisia.Nikieleza zaidi italeta uhalisia
 
Wandugu sipingani na wanasayansi kuwa ni magonjwa ya akili..Ukweli usiopingika ni ugonjwa wa akili.Nami niilitumia tiba hospital...ila mara mwisho tulipoenda tuliambiwa tutafute njia nyingine pia..Kwani nilochomwa sindano ya usingizi na sikulala!!

Na nilielezwa nina hofu ..Ila nikitathmini katika hayo sijawahi kuwa nina hofu na mambo ya ushirikina!!Nami nilifanyia kazi ushauri wa madr ikiwemo kumeza vidonge nilivyopewa na kutrain akili jinsi ya kutosikliza sauti.
Sitazungumza Kila kitu..Kwani hata mm siamini yanliyoniyokea bado
 
Back
Top Bottom