Mungu si athumani!!Nikadahiliwa chuo kinachoitwa kikubwa Afrika Kiko Tanzania(hahahahaha msinipopoe)..
Hapo nishasahau mambo ya usister,nimepata kibwana kinasoma IFM.Huyu alijua kinipeleka mpka nikinya nataja jina lake.Huyu tuliishi nae mtaa wa Tabata relini Kwa mama Mdogo.So kila Wkend lazima nirudi home tuonane..Bwana huyu hakupta boom Kwa wakati basi alivyopata Boom niliona Kila aina vituko..Alijua kuutia nyongo hasa moyo.Kwangu Kila mwanaume aliyenijia alijua Nina mchumba IFM.
Ikafika kipindi kuonana shida utaweka vocha hata ya elfu Tano muwasiliane kabla ya vifurushi!!Kumbe kazuzuka na kabinti kengine huko...Enzi hizo nami nilikuwa mzuri wa Sura si Jana
.japo sikuwa na nyama za kuwafanya wanaume wenye tamaa watoke udenda.
Mpka kufika second year...Nilikuwa mekonda...Nikakutana na feminist wanaosoma Literature wakanipa lecture kuhusu ufeminist nikasema ahsanteni dada zangu.Hili Penzi Sasa akiweka pilau naweka kachumbari...akiweka uji natia chumvi.