Chapa Nalo Jr
JF-Expert Member
- Dec 8, 2010
- 7,518
- 6,506
Ni vigumu kujuana kwa kina ndani ya uchumba maana kuonana kunakuwa kwa mara chache sana tunakoishi, na mara nyingi tunakutana bar, migahawani,bustani za mji, kwenye miti nk.
Unaweza tambua tabia fulani lakini ikawepo tabia ndogo tu usiifahamu na ndoa ikiwa tayari hapo lazima utaifahamu na pengine ikawapitisha kwenye kasheshe au katafrani.
My story; Nilipomuoa mke wangu hapo sasa inakuwa day to day ni kitanda kimoja, mke wangu yeye akaweka msimamo mdogo tu kuwa yeye toka kwao alipokuwa analala kitanda kimoja na dada yake huwa hapendi kulala ukutani, bali ule upande wa kutelemkia (sijui kwa wenzetu ambao vyumba vyenu vikubwa na mnaweka kitanda katikati). Wiki kama tatu tu baada ya ndoa kuna siku nikamuwekea ngumu na kuamua kulala upande wa kushukia, alilalamika sana, akaomba nimpishe nikagoma, akaamua kwenda kulala sebuleni (yaani kama utoto vile), mimi nikaendelea kulala. Baadaye aliingia chumbani na maji kwenye kibeseni kidogo akanimwagia nilishituka sana, nilimrukia na kupiga ngumi, akaanguka chini nami nikateleza kwenye zulia la plastiki lililokuwa na mji na kuanguka, akakamaka mkono wangu na kuning`ata, ikafuata tafrani kidogo lakini nikashituka kuwa majirani watasikia nikamwacha. Ni vugumu kueleza yote, lakini ukweli ni kuwa siku kama tatu nne hivi zilizofuata kulikuwa hamna peace kabisa ndani ya nyumba. Baadaye akaamua kuniomba msamaha na mimi nikasema naona ni vema niridhie uwe unalala upande unaotaka, na ndivyo ilivyo licha ya kwamba kuna siku huwa anaamua kulala ukutani.
Lilikuwa ni tukio la kipuuzi sana, na toka siku hiyo niliapa moyoni siji mrushia ngumi mke wangu, I have in mind destroyed all my "weapons of mass destruction", ni afadhali nimuonye kwa mdomo tu.
Je wewe member wa mmu unaweza kumbuka msukosuko wa mwanzo katika ndoa yako!?