My "World War One(WWI)" ndani ya ndoa.

My "World War One(WWI)" ndani ya ndoa.

Chapa Nalo Jr

JF-Expert Member
Joined
Dec 8, 2010
Posts
7,518
Reaction score
6,506
Ni vigumu kujuana kwa kina ndani ya uchumba maana kuonana kunakuwa kwa mara chache sana tunakoishi, na mara nyingi tunakutana bar, migahawani,bustani za mji, kwenye miti nk.

Unaweza tambua tabia fulani lakini ikawepo tabia ndogo tu usiifahamu na ndoa ikiwa tayari hapo lazima utaifahamu na pengine ikawapitisha kwenye kasheshe au katafrani.

My story; Nilipomuoa mke wangu hapo sasa inakuwa day to day ni kitanda kimoja, mke wangu yeye akaweka msimamo mdogo tu kuwa yeye toka kwao alipokuwa analala kitanda kimoja na dada yake huwa hapendi kulala ukutani, bali ule upande wa kutelemkia (sijui kwa wenzetu ambao vyumba vyenu vikubwa na mnaweka kitanda katikati). Wiki kama tatu tu baada ya ndoa kuna siku nikamuwekea ngumu na kuamua kulala upande wa kushukia, alilalamika sana, akaomba nimpishe nikagoma, akaamua kwenda kulala sebuleni (yaani kama utoto vile), mimi nikaendelea kulala. Baadaye aliingia chumbani na maji kwenye kibeseni kidogo akanimwagia nilishituka sana, nilimrukia na kupiga ngumi, akaanguka chini nami nikateleza kwenye zulia la plastiki lililokuwa na mji na kuanguka, akakamaka mkono wangu na kuning`ata, ikafuata tafrani kidogo lakini nikashituka kuwa majirani watasikia nikamwacha. Ni vugumu kueleza yote, lakini ukweli ni kuwa siku kama tatu nne hivi zilizofuata kulikuwa hamna peace kabisa ndani ya nyumba. Baadaye akaamua kuniomba msamaha na mimi nikasema naona ni vema niridhie uwe unalala upande unaotaka, na ndivyo ilivyo licha ya kwamba kuna siku huwa anaamua kulala ukutani.

Lilikuwa ni tukio la kipuuzi sana, na toka siku hiyo niliapa moyoni siji mrushia ngumi mke wangu, I have in mind destroyed all my "weapons of mass destruction", ni afadhali nimuonye kwa mdomo tu.

Je wewe member wa mmu unaweza kumbuka msukosuko wa mwanzo katika ndoa yako!?
 
Mkuu Story nzuri sana hiyo, du ulifanya kosa kumpiga wife alafu hizo battle ndogo ndogo huwe unamwachia anashinda si unajua kushinda battle is not winning a war..

Kwahiyo compromise mengine muachie ili na wewe akuachie... tena wewe unabahati sana yaani upande wa kulala tu wengine huwa wanagombania vitu ambavyo ni vigumu kuachia
 
Nahisi lengo la thread ni kuwa na mwendelezo wa visa vya kweli vya ndani ya ndoa, kinaweza kikawa cha kwanza, au kile unachokikumbuka zaidi. Wadau mlioko ndoani tunaomba mwendelezo, nataka mpaka kufikia 2018 nitakapooa, nikute thread iko hai na mimi nichangie....
Endeleaaaaa......
 
Mkuu ndio maana nemeapa kutofanya mashambulizi to my wife tena
 
Nahisi lengo la thread ni kuwa na mwendelezo wa visa vya kweli vya ndani ya ndoa, kinaweza kikawa cha kwanza, au kile unachokikumbuka zaidi. Wadau mlioko ndoani tunaomba mwendelezo, nataka mpaka kufikia 2018 nitakapooa, nikute thread iko hai na mimi nichangie....
Endeleaaaaa......

No no no no no!, ndugu sina maana ya mwendelezo wa visa ndani ya ndoa, bali mtihani wa kwanza katika ndoa, na zaidi kuwafunza watu waepuke mashindano katika masuala madogo madogo, please naomba ieleweke hivyo!, naheshimu sana taasisi ya ndoa.

Mimi mwenyewe baada ya kufahamiana vizuri na mke wangu sasa mambo yanakwenda vizuri katika kila nyanja ya maisha (simaanishi hakuna tatizo kabisa)
 
this story is crazy....duh!
sasa wewe ulimpiga ngumi kwa hasira au ulidhani mwizi?
hahahaha...funny stuff!
 
Duuu hicho kipindi cha ndimu katika stage ya mapenzi, hongera uliamua kujifunza na kumsoma mwenzio ukamfahamu. Otherwise mngekuwa kwenye SHUBIRI wakati huu!!
 
Pole nyingi kwa wife kwa kipigo alichopata,

Ubaguzi huo mbona hunipi pole na mimi niliyeng`atwa na kumwagiwa maji!? Hata hivyo hayo ni mambo ya kale sasa tunaishi maisha ya raha mstarehe, miaka 4 sasa!
 
this story is crazy....duh!
sasa wewe ulimpiga ngumi kwa hasira au ulidhani mwizi?
hahahaha...funny stuff!

Hapo kwenye nyekundu; Wanasheria wanasema "if done under the heat of passion before time to cool" is the defence for criminal act/charge of assault(sic)
 
this story is crazy....duh!
sasa wewe ulimpiga ngumi kwa hasira au ulidhani mwizi?
hahahaha...funny stuff!
Hakuna Funny stuff Hapo kaka, soma ukiwa conscious na uelewe nini maanake
 
Ubaguzi huo mbona hunipi pole na mimi niliyeng`atwa na kumwagiwa maji!? Hata hivyo hayo ni mambo ya kale sasa tunaishi maisha ya raha mstarehe, miaka 4 sasa!
Kichapo ulichompa ni sahihi kabisa na ulitakiwa usingempa kabisa nafasi ya kukungata. Na baada y kichapo ungeondoka zako ukarudi asubuhi. Siku hiyo2 angekuomba samahani. Alichokifanya ni kupima strength yako na jambo la kawaida kwa African women hasa kama mnatoka makabila tofauti kama mlivyo nyie. I stand 2b corrected. Na hayo huwa ndo mafunzo wapewayo wadada kuwa wafahamu mapema weaks n strength za wenzi wao ili waweze kuzitumia.
 
Hapo kwenye nyekundu; Wanasheria wanasema "if done under the heat of passion before time to cool" is the defence for criminal act/charge of assault(sic)

sorry mate...i have never heard that line of defence before! ama sivyo cases nyingi za assault zingetupwa nje.
 
Kichapo ulichompa ni sahihi kabisa na ulitakiwa usingempa kabisa nafasi ya kukungata. Na baada y kichapo ungeondoka zako ukarudi asubuhi. Siku hiyo2 angekuomba samahani. Alichokifanya ni kupima strength yako na jambo la kawaida kwa African women hasa kama mnatoka makabila tofauti kama mlivyo nyie. I stand 2b corrected. Na hayo huwa ndo mafunzo wapewayo wadada kuwa wafahamu mapema weaks n strength za wenzi wao ili waweze kuzitumia.

Hivi umekisikia kisa chenyewe cha kupigana??
 
mara nyingi ugomvi wa kwenye ndoa huanzia kwenyecvitu vidogo vidogo na vya kipuuzi sana kugombania channel za kuangalia baba anataka mpira mama anataka tamthilia mnaishia kununiana. hiyo ya kulala ukutani mimi inanikuta mara nyingi saana basi nikimkuta kalala hampo simfukuzi wala kumtwanga mingumi nachofanya ni kupewa ticket ya kummega mzee ntashika **** kiuno ataanza kulalamika mmh mwanaume hutosheki asubuhi umekula na sasa unataka km hataki atasogea upande wake. na yeye siku akiwa horny anawahi kulala upande wangu au mkishaingia kulala utasikia na mimi nataka kulala mwanzoni basi atajisogeza hapo mtabanana hapo so as a man najua kabisa huyu anahitaji dozi nzito na kweli atatoa ushirikiano mzuri tu na atamaliza game kwa furaha na atarudi sehemu yake.
 
Dah hakuna mwingine anaki2ko kama hiki? this stuff dah.
 
duh....burudani kweli....mwingine tafadhali mwenye adisi yake atuadisie.....
 
Just thinking...je hii lugha ni sahihi? Sio lugha inayodhalilisha wanawake?

Back
Top Bottom