Myanmar: Jeshi lawanyonga Wanaharakati 4 wa Demokrasia

Myanmar: Jeshi lawanyonga Wanaharakati 4 wa Demokrasia

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2021
Posts
1,147
Reaction score
2,008
Wanaharakati wanne wa demokrasia akiwemo Mbunge wa zamani Phyo Zeya Thaw wamenyongwa na jeshi la Myanmar wakituhumiwa kwa mipango na kufanya njama za vitendo vya ugaidi

Wanaharakati hao walihukumiwa kifo katika kesi za siri mwezi Januari na Aprili, kwa kituhumiwa kwa kusaidia waasi kupigana na jeshi lililochukua mamlaka katika mapinduzi ya mwaka jana

Mnamo mwaka 2021, jeshi la nchi hiyo lilipindua Serikali na kusababisha ukandamizaji wa kijeshi dhidi ya waandamanaji wanaounga mkono demokrasia, wanaharakati na waandishi wa habari

........................................................

July 25 (Reuters) - Myanmar's military junta has executed four democracy activists accused of helping to carry out "terror acts", it said on Monday, sparking widespread condemnation of the Southeast Asian nation's first executions in decades.

Sentenced to death in closed-door trials in January and April, the four men had been accused of helping insurgents to fight the army that seized power in a coup last year and unleashed a bloody crackdown on its opponents.

Myanmar's National Unity Government (NUG), a shadow administration outlawed by the ruling junta, condemned the executions and called for international action against the ruling military.

"Extremely saddened ... condemn the junta's cruelty," Kyaw Zaw, the spokesman of the NUG president’s office, told Reuters in a message. "The global community must punish their cruelty."

Among those executed were democracy campaigner Kyaw Min Yu, better known as Jimmy, and former lawmaker and hip-hop artist Phyo Zeya Thaw, the Global New Light of Myanmar newspaper said.

Kyaw Min Yu, 53, and Phyo Zeya Thaw, a 41-year-old ally of ousted leader Aung San Suu Kyi, lost their appeals against the sentences in June. The two others executed were Hla Myo Aung and Aung Thura Zaw.

"These executions amount to arbitrary deprivation of lives and are another example of Myanmar’s atrocious human rights record," said Erwin Van Der Borght, regional director of rights group Amnesty International.

"The four men were convicted by a military court in highly secretive and deeply unfair trials. The international community must act immediately as more than 100 people are believed to be on death row after being convicted in similar proceedings."

SOURCE: REUTERS
 
WANAHARAKATI wanne wa Demokrasia wa nchini Myanmar akiwemo mbunge wa zamani wameuawa kwa kunyongwa na Jeshi la nchi hiyo kutokana na kukutwa na hatia ya kujihusisha na njama za kutekeleza matukio ya kigaidi nchini humo.

Miongoni mwao alikuwepo mwanaharakati maarufu wa nchi hiyo Ko Jimmy pamoja na mbunge wa zamani Phyo ZeyaThaw ambao kabla ya kunyongwa kwao walihukumiwa kifungo cha maisha jela.

Mnamo siku ya Jumatatu familia za marehemu hao zilikusanyika nje ya Gereza la Insein lililopo nchini humo ambalo ni moja kati ya magereza hatari duniani ili kujua hatima za wapendwa wao.

Mama mzazi wa Zayar Thaw amesema hakupewa taarifa ni lini mtoto wake atanyongwa hali iliyomfanya ashindwe kuandaa vizuri maziko yake.

Tayari familia zote zimetuma maombi rasmi Serikalini kupewa maelekezo juu ya mauaji ya wapendwa wao.

Chombo cha habari cha Taifa hilo Global News kimeripoti kuwa wanaharakati hao wameuawa kwa kunyongwa kutokana na kutoa siri, maelekezo, kupanga njama pamoja na kusababisha kutekeleza mauaji ya kikatili ya raia wasio na hatia.

Mauaji hayo ya kunyonga ni ya mara ya kwanza nchini humo tangu ifanyike hivyo mwaka 1988, hiyo ni kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.
 
Back
Top Bottom