Mzaliwa wa kwanza afe, kwa ukombozi wa Israel

Mzaliwa wa kwanza afe, kwa ukombozi wa Israel

SIPOHURU

New Member
Joined
Jul 29, 2025
Posts
2
Reaction score
0
Katika biblia, kuna habari ya wana Israel chini ya Musa waliokuwa wanaomba ruhusa kwa FARAO, ili waende nchi ya ahadi. FARAO alikataa pamoja na kupewa mapigo kadhaa lakini hakutoa ruhusa. ndipo pigo la mwisho likawa la kuua mzaliwa wa kwanza wa binadamu na mnyama wafe. Walipokufa, kesho yake kila mji ulikuwa ni kilio tupu Misri nzima.

Kutoka 11:5
Nitakapopita, kila mzaliwa wa kwanza nchini Misri atakufa: Kuanzia mzaliwa wa kwanza wako wewe Farao ambaye ni mrithi wako, hadi mzaliwa wa kwanza wa mjakazi anayesaga nafaka kwa jiwe. Hata wazaliwa wa kwanza wa mifugo nao wote watakufa.


Kwa hali tuliyofikia, ni bora wazaliwa wa kwanza wa serikali, chachama, vyombo vya dola, uchaguzi, vyama vya siasa, vigogo wa wilaya wafe, tuamke tukiwa na kilio nchi nzima, pengine tunaweza kubali kujirekebisha.

Nchi imejaa unafiki. Wanaotakiwa kushauri, wako kimya wakiruhusu watu kuumizwa kwa ajili ya FARAO. Ndiyo maana wanapaswa wafe ili kutoa funzo kwa wengine kuheshimu haki za binadamu. Ni kwa vile tu Mungu siyo Athumani, angekuwa Athuman, tungeomba hili liwe leo wala siyo kesho.

Nchi imefikia hatua mbaya sana, Eeee Mungu tusaidie na tuepushe na huu uovu.
 
Back
Top Bottom