Salum Maawali
New Member
- May 25, 2016
- 3
- 7
SalaamTipp Tip alikuwa ni Mchotara kama Obama, hata Obama amemuua Gadafi pia!
Waungwana
Ukoo wa huyu muungwana unaitwa Al marjeby. Lakini la kushangaza sana huyu bwana hakuwa mfanya biashara ya utumwa kama mlivyofunzwa historia ya uongo na wazungu na vibaraka wao. Huyu ndie aliyekuwa anaaminiwa kuijua Tanganyika hadi Kongo wakati huo na alikuwa mfanyabiashara wa kawaida na mtu pekee ambae ameishi na kuona tawala za masultani tofauti Zanzibar kuliko mtu yeyote. Wakati Livingstone na Stanley wanafika Zanzibar yeye ndie aliepewa watu hawa wawili ili awafikishe Tanganyika na walikuwa hawana pesa. Aliwachukua kwa gharama zake hadi kufika safari yao. Samahani kwa sasa sitaweka source. La kushangaza walipofika London walizua uongo wa utumwa ili kuraise fund kwa ajili ya kupambana nao watakaporudi Afrika Mashariki. Na ukitaka kujua kama wazungu waongo kuhusiana na utumwa nenda Bwagamoyo, fika kwenye banda la historia ya mji la serikali kasha tazama rekodi ya historia fupi ya mji huo kwenye ubao uliombatana na picha utakuta pia wameweka picha ya Bushiri bin Salim Al harthy pamoja na picha ya huyu jamaa kuwa walikuwa vinara wa bishara hiyo. Huo ni ushahidi mdogo tu ambao naomba msomaji akifika kwenye mji ule ajidhirishe mwenyewe.
Kuhusu uko wake, mimi najua mji walio vitukuu vyake ila sitoutaja na wala sio Tanzania walipo wale direct discendants na wala hawatumii hili jina la Tip tip ambalo lilikuwa la utani. Baadhi wapo Zanzibar hadi leo na kama ujuavyo mali zao zimetaifishwa na serikali dhalim ya kimapinduzi.
Naomba niishie hapa.