Mzazi adai kuwa na mashaka ya kifo cha binti yake kinachodaiwa kusababishwa na sumu, alikuwa akiishi kwa siri na mwanaume anayedaiwa kuwa mwanajeshi

Hata kama ni marehemu ila apaswa kulaumiwa.
Unachukuaje uamuzi wa kuishi na mtu informally!??
Aisee wanawake wa siku hizi majasiri sana.
Kwani aliishi peke yake? Ujasiri wa mjeda huuoni?
 
Ifike hatua tuongee ukweli, vijana na mabinti wa chuo wengi wako kwenye ndoa bubu, baadhi ya wasichana ndo huvuka had kwa hao watu wazima na kuishi km mke, kisa tyuuh kutaka urahisi wa maisha.

Km hili suala, binti anasoma Dar, ila kafia Tabora, je huko alifikaje? Tunaambiwa alikua anaishi nae kwa siri huyo mwanaume, ina maana aliacha chuo na kwenda kuishi huko? Au ilikua likizo time na yeye akaamua kuvuta ndo yakamkuta haya?

Tumeambiwa huyo mwanaume baada ya kuona mchumba ake ana matatizo ya afya, alimuita mdogo wake wakampeleka hospital, na walipofika alilipia matibabu ya awali,na kumuachia mdogo mtu elf 40, ina maana huyu mdogo mtu alijua haya mahusiano,na walikua na mawasiliano na huyo mwanaume (shemeji) ndo maana alitafutwa na akaachiwa hela ya matumizi hapo hospital.

Kwa mtazamo wangu waanze kumuhoji mdogo wa marehemu, huyu ndo anajua kila kitu,
 
Hata kama ni marehemu ila apaswa kulaumiwa.
Unachukuaje uamuzi wa kuishi na mtu informally!??
Aisee wanawake wa siku hizi majasiri sana.
Kwa maoni yangu, Uamuzi wa kuishi na mtu informally siyo tatizo hata kidogo kwa sababu hata ndoa nyingi za kimila au watu (mume&mke) kuishi kwenye maisha ya dhana ya ndoa (presumption of marriage) huwa zinaanzia na kwenye hatua kama hii hii. Isipokuwa tatizo ninaloliona Mimi ni kwamba huyo marehemu alifanya makosa kuficha uhusiano wake huo kwa kutokuwajulisha wazazi wake, ndugu zake au hata jamaa zake na marafiki zake wa karibu aliokuwa akifahamiana nao. Hilo ndilo kosa alilofanya.
 
Unamlaumu vipi marehemu? Atajiteteaje?
Marehemu analaumiwa kutokana na maelezo ya mzazi wake kama yatakuwa na ukweli.

Kama maelezo ya mzazi yatakuwa hayana ukweli, basi marehemu anaondolewa kwenye lawama hizo.

Lakini ninavyohisi lawama hizi za mzazi ni kidasi tu, binti yake alikuwa above 18 yrs bhana, alikuwa na uhuru wa maamuzi aishije.

Ni ngumu sana mpenzi aliye na dhamira ovu aanze kumhudumia mgonjwa hadi hospitali na kutoa gharama mbali mbali.

Kutoonesha sura baada ya kifo cha marehemu, saazingine ni kukwepa lawama toka kwa wazazi wa aina hii.

Jamaa alizihisi ngebe za kijinga za mshua, akaamua kula kona.

Kusema kwamba mjeda huyo kahusika na kifo hicho, sidhani.
 
Huyo Mjeshi anahusika moja kwa moja na mkasa wa kifo cha huyo Mwanamke, he is a KEY SUSPECT kwa jinsi taarifa za awali zilivyo kuhusiana na suala hili.
Mjeshi anahusika directly or indirectly ktk kusababisha kifo cha mtu huyo:
1. Huenda, Yawezekana yeye mwenyewe huyo Mwanaume ndiye aliyemuua kwa sumu kutokana na sababu zozote zile ambazo yeye anaona zinafaa.
2. Huenda, marehemu alijidhuru kwa namna yoyote ile baada ya kuhitilafiana au kugombana na huyo Mwanaume/Mwanajeshi.
3.Huenda, Yawezekana Mwanamke mwingine ambaye pia alikuwa na mahusiano ya kimapenzi (kimada) wa huyo Mwanaume/Mwanajeshi amehusika katika kumhujumu au kumdhuru kwa sumu huyo marehemu kutokana na sababu za wivu wa mapenzi.
4.Huenda Marehemu alikuwa ana matatizo yake binafsi ya kiafya ambayo ndiyo yaliyomsababisjia kifo chake wakati akiwa kwa huyo Mwanaume.

Ukichunguza dhana zote hizi nilizoeleza hapa juu utagundua pasipo kuacha shaka kwamba huyo Mwanaume anahusika au anaguswa kwa namna zote kabisa na kifo cha huyo marehemu, ni mtu muhimu sana kwenye suala hili ili kuweza kusaidia Upelelezi wa Kesi kwenye kifo hiki. Huyo Mwanaume ana Kesi ya kujibu, he is a KEY SUSPECT and/or a KEY WITNESS.
 
huo uzi kama unaukumbuka nitajie jina lake

Hii hpa ndugu
 
Hii hali inaogopesha kwasababu kuna binti kanafunga chuo cha ualimu tarehe 21 sasa lengo langu nikaburudike nae kwa likizo yake yote ya wiki 2,, sasa ikitokea akanifia huko hotelini sijui nitafanyaje
Mkuu achana kabisa na habari za kulala na mtoto wa mtu wiki zima, kizazi cha siku hizi kinatembea na mwilini na Presha, homa ya ini, HIV hayo magonjwa suala la Kwenda ahera ni sekunde tu.
 
Kifo ni fumbo kubwa sababu lazima wote tutakufa. Tunapofanya mambo yetu tusisahau ukweli huo. Inawezekana kabisa mjeda hakufanya lolote baya, ila muda ulifika. Inawezekana pia alifanya baya.
Dada alifanya makosa kuanza kuishi na Mwanaume bila wazazi kujua.
 
Kuna msamalia mwema mmoja muuza mahindi aliokota bullets za risasi akazipeleka polisi cha ajabu wakamwambia alete na Risasi nyingine alizonazo, navyokwambia huu ni mwaka wa 7 yupo jela hata mahakamani kesi haijaanza kusomwa.

Unaweza kumsaidia mtu amegongwa kaanguka hapo. Ukienda kuchukua PF 3 ili atibiwe, unakamatwa wewe unayetoa msaada.
Inafikirisha sana. Inaogopesha sana. Tujiongeze laasivyo, kila mtu atakuwa mpenzi mtazamaji kwenye mambo yanayohitaji utu na huruma
 
Wanawake/watoto sahivi wao ni kuwadandiadandia tu wanaume
Wakipewa vijihela haoo washadandia

Ova
 

Inasikitisha sana kupoteza binti kwenye mazingira ya namna hii. Ila hawa watoto nao.. kwanza nilidhani labda hiki chuo kiko Tabora, nimerudia kusoma naona kiko Dar. Sasa kweli Dar to Tabora? Nahisi labda walitaka kutoa mimba hawa.
 
Pole sana kwa msiba. Hawa mabinti wa chuo baadhi ni majanga. Wanaishi vyuoni kama wake za vijana wa kiume. Pili wanaishi mitaani na wanaume kama mke na mume. Wakipata mimba ndio wanahangaika kuzitoa wengine ndio wanakufa au kuwa tasa nk. Huyo mwanamme asingemwita mdogo wake kama hafahamiki. Mkeo anajua issue yotee. Usihangaike kumshtaki.
 
Unaweza kumsaidia mtu amegongwa kaanguka hapo. Ukienda kuchukua PF 3 ili atibiwe, unakamatwa wewe unayetoa msaada.
Inafikirisha sana. Inaogopesha sana. Tujiongeze laasivyo, kila mtu atakuwa mpenzi mtazamaji kwenye mambo yanayohitaji utu na huruma
Hawa polisi wetu wa nchi za dunia ya tatu sijui ni elimu ndogo au ni uvivu hata sielewi maana hawafanyi kazi kwa weledi kabisa yani inasikitisha sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…