Hata kama ni marehemu ila apaswa kulaumiwa.Unamlaumu vipi marehemu? Atajiteteaje?
Unachukuaje uamuzi wa kuishi na mtu informally!??
Aisee wanawake wa siku hizi majasiri sana.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hata kama ni marehemu ila apaswa kulaumiwa.Unamlaumu vipi marehemu? Atajiteteaje?
Kwani aliishi peke yake? Ujasiri wa mjeda huuoni?Hata kama ni marehemu ila apaswa kulaumiwa.
Unachukuaje uamuzi wa kuishi na mtu informally!??
Aisee wanawake wa siku hizi majasiri sana.
Kwa maoni yangu, Uamuzi wa kuishi na mtu informally siyo tatizo hata kidogo kwa sababu hata ndoa nyingi za kimila au watu (mume&mke) kuishi kwenye maisha ya dhana ya ndoa (presumption of marriage) huwa zinaanzia na kwenye hatua kama hii hii. Isipokuwa tatizo ninaloliona Mimi ni kwamba huyo marehemu alifanya makosa kuficha uhusiano wake huo kwa kutokuwajulisha wazazi wake, ndugu zake au hata jamaa zake na marafiki zake wa karibu aliokuwa akifahamiana nao. Hilo ndilo kosa alilofanya.Hata kama ni marehemu ila apaswa kulaumiwa.
Unachukuaje uamuzi wa kuishi na mtu informally!??
Aisee wanawake wa siku hizi majasiri sana.
Marehemu analaumiwa kutokana na maelezo ya mzazi wake kama yatakuwa na ukweli.Unamlaumu vipi marehemu? Atajiteteaje?
Huyo Mjeshi anahusika moja kwa moja na mkasa wa kifo cha huyo Mwanamke, he is a KEY SUSPECT kwa jinsi taarifa za awali zilivyo kuhusiana na suala hili.Marehemu analaumiwa kutokana na maelezo ya mzazu wake kama yatakuwa na ukweli.
Kama maelezo ya mzazi yatakuwa hayana ukweli, basi marehemu anaondolewa kwenye kawama hizo.
Lakini ninavyohisi lawama hizi za mzazi ni kidasi tu, binti yake alikuwa above 18 yrs bhana, alikuwa na uhuru wa maamuzi aishije.
Ni ngumu sana mpenzi aliye na dhamira ovu aanze kumhudumia mgonjwa hadi hospitali na kutoa gharama mbali mbali.
Kutoonesha sura baada ya kifo cha marehemu, saazingine ni kukwepa lawama toka kwa wazazi wa aina hii.
Jamaa alizihisi ngebe za kijinga za mshua, akaamua kula kona.
Kusema kwamba mjeda huyo kahusika na kifo hicho, sidhani.
Wala sio maisha mazuri, ni uhuru unaokuja bila mipaka unawachanganya watoto.Si wanataka maisha mazuri, acha majanga yawakutee.
huo uzi kama unaukumbuka nitajie jina lake
Mkuu achana kabisa na habari za kulala na mtoto wa mtu wiki zima, kizazi cha siku hizi kinatembea na mwilini na Presha, homa ya ini, HIV hayo magonjwa suala la Kwenda ahera ni sekunde tu.Hii hali inaogopesha kwasababu kuna binti kanafunga chuo cha ualimu tarehe 21 sasa lengo langu nikaburudike nae kwa likizo yake yote ya wiki 2,, sasa ikitokea akanifia huko hotelini sijui nitafanyaje
Kuna msamalia mwema mmoja muuza mahindi aliokota bullets za risasi akazipeleka polisi cha ajabu wakamwambia alete na Risasi nyingine alizonazo, navyokwambia huu ni mwaka wa 7 yupo jela hata mahakamani kesi haijaanza kusomwa.Unatoa taarifa polisi, ikionekana hukuuwa huna kesi.
Kuna msamalia mwema mmoja muuza mahindi aliokota bullets za risasi akazipeleka polisi cha ajabu wakamwambia alete na Risasi nyingine alizonazo, navyokwambia huu ni mwaka wa 7 yupo jela hata mahakamani kesi haijaanza kusomwa.Unatoa taarifa polisi, ikionekana hukuuwa huna kesi.
Kuna msamalia mwema mmoja muuza mahindi aliokota bullets za risasi akazipeleka polisi cha ajabu wakamwambia alete na Risasi nyingine alizonazo, navyokwambia huu ni mwaka wa 7 yupo jela hata mahakamani kesi haijaanza kusomwa.
Ifike hatua tuongee ukweli, vijana na mabinti wa chuo wengi wako kwenye ndoa bubu, baadhi ya wasichana ndo huvuka had kwa hao watu wazima na kuishi km mke, kisa tyuuh kutaka urahisi wa maisha.
Km hili suala, binti anasoma Dar, ila kafia Tabora, je huko alifikaje? Tunaambiwa alikua anaishi nae kwa siri huyo mwanaume, ina maana aliacha chuo na kwenda kuishi huko? Au ilikua likizo time na yeye akaamua kuvuta ndo yakamkuta haya?
Tumeambiwa huyo mwanaume baada ya kuona mchumba ake ana matatizo ya afya, alimuita mdogo wake wakampeleka hospital, na walipofika alilipia matibabu ya awali,na kumuachia mdogo mtu elf 40, ina maana huyu mdogo mtu alijua haya mahusiano,na walikua na mawasiliano na huyo mwanaume (shemeji) ndo maana alitafutwa na akaachiwa hela ya matumizi hapo hospital.
Kwa mtazamo wangu waanze kumuhoji mdogo wa marehemu, huyu ndo anajua kila kitu,
Pole sana kwa msiba. Hawa mabinti wa chuo baadhi ni majanga. Wanaishi vyuoni kama wake za vijana wa kiume. Pili wanaishi mitaani na wanaume kama mke na mume. Wakipata mimba ndio wanahangaika kuzitoa wengine ndio wanakufa au kuwa tasa nk. Huyo mwanamme asingemwita mdogo wake kama hafahamiki. Mkeo anajua issue yotee. Usihangaike kumshtaki.Copy and Paste kama ilivyokutwa;
"Moyo wangu unavuja damu kuhusu binti yangu wa kwanza Maria Izidory Petro ambaye alikuwa anasoma Chuo, Institute of Tax Administration kilichoko Dar es Salaam akichukua Shahada ya Kodi. Alipata changamoto ya kiafya ghafla kwa ambacho kilidaiwa kuwa sumu kwa mujibu wa madaktari tarehe 26 na kufariki 27 Septemba 2024 katika Hospitali ya Rufaa Kitete, baada ya kupelekwa na mwanaume nisiyemjua."
"Mwanaume huyo alipomfikisha hospitali, alilipa pesa ya awali hospitali na kumwachia mdogo wa marehemu elfu 40 ya dharula. Mdogo wa marehemu aliitwa na mwanaume baada ya dada yake kupata shida hiyo. Watu waliokuja nyumbani baada ya mazishi ni wafanyakazi wenzake tu kwa kadiri ya maelezo yao."
"Wakati tatizo linampata tayari mwanaume huyo alikuwa akiishi naye kwa siri, inasemekana ni mwanajeshi wa kambi ya Mabama Tabora, alimchukua bila ya mimi kuwa na taarifa. Nina wasiwasi kifo cha mwanangu si cha kawaida."
"Ninaomba kupaziwa sauti ili haki itendeke. Baba ninakuomba nina maumivu makali."
Izidory Petro Chinyo,
Mzazi.
20 Novemba 2024.
Hawa polisi wetu wa nchi za dunia ya tatu sijui ni elimu ndogo au ni uvivu hata sielewi maana hawafanyi kazi kwa weledi kabisa yani inasikitisha sana.Unaweza kumsaidia mtu amegongwa kaanguka hapo. Ukienda kuchukua PF 3 ili atibiwe, unakamatwa wewe unayetoa msaada.
Inafikirisha sana. Inaogopesha sana. Tujiongeze laasivyo, kila mtu atakuwa mpenzi mtazamaji kwenye mambo yanayohitaji utu na huruma
hv inawezekana muweka sumu akupeleke kutibiwa ili hali mlikuwa wapenzibwa siri!!???????Tayari kuna kianzio hapo..
1.Sababu ya kifo sumu
2. Mtu aliyemleta hospital