Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
MZAZI JUKUMU LAKO NI KUNIFUNDISHA JINSI YA KUFANYA MAAMUZI SAHIHI NA SIO UNIFANYIE MAAMUZI.
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli
Wewe ni wewe. Mimi ni Mimi. NI kweli wewe ni mzazi na mimi ni mtoto. Lakini hiyo haimaanishi kuwa wewe ni Mimi. Utabaki kuwa mzazi lakini hautakuwa mimi na mimi sitakuja kuwa wewe.
Ndoto zako sio ndoto zangu ingawaje wakati mwingine zinaweza kufanana. Hobbies zako sio hobbies zangu ingawaje zinaweza kufanana.
Mimi ni mimi. Na wewe ni wewe.
Mimi nitakuwa mzazi baadaye lakini haitamaaanisha watoto wangu watakuwa Mimi.
Nimwoe nani Sio kazi yako.
Nimpende nani hiyo sio juu yako.
Nifanye kazi gani hiyo niachie mwenyewe.
Usinione mkaidi kwa sababu ya kuvuka mipaka yako.
Nifundishe jinsi ya kufanya maamuzi sahihi lakini kamwe sitakuruhusu unifanyie maamuzi.
Ninauchaguzi na uhuru wa kuchagua njia niitakayo. Kwani huo ndio ubinadamu.
Umri wa utoto ndio umri wa kumfundisha mtoto yale yote unayotaka ayafuate. Ndio umri pekee wa kumfanyia mtoto Maamuzi.
Samaki mkunje angali mbichi.
Mlee mtoto katika njia impasayo naye hataiacha mpaka atakapokuwa mzee.
Acha Nipumzike sasa.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam