Mwanamke mwenye Pumu afuate taratibu zipi ili kumuepusha kijacho wake na Pumu?
Kuna mambo mengi ya kuzingatia kwa mzazi wa aina hii:
1: Kama hajaolewa au kupata mwenza: ni vyema kuwa na hali ya kuepuka kupata mwenza mwenye tatizo kama lake. Kwani akimpata mwenza wa aina hiyo, basi uwezekano wa kupata mtoto mwenye pumu kali zaidi unakuwa mkubwa. Kibaiolojia.
2: Anapokuwa mjamzito, ajiepushe na vitu vinavyoweza kumfanya apate mtoto njiti, kwani watoto njiti wana nafasi kubwa ya kuwa na pumu au mzio. Hivyo:
A: Ajiepushe na kuvuta sigara
B: Ajiepushe na matumizi ya pombe
C: Ajitahisi kupata mlo kamili kwa muda wote
D: Ajiepushe na stress nk.
3: Mtoto atakapozaliwa ajiepushe:
A: Kumpa maziwa ya wanyama chini ya umri wa mwaka mmoja
B: Anyonyeshe maziwa ya mama tu kwa miezi sita.
C: Amwepushe mtoto na matumizi ya vyakula vyenye rangi zisizo za asili.
D: Amwepushe na matumizi ya vitu vyenye harufu kali (mafuta ya kupaka vs sabuni).
E: Mwepushe na matumizi ya karanga, blueband, unga wa mbegu za maboga.
F: Epuka matumizi ya feni na air condition.