Judithkaunda
Member
- Aug 21, 2022
- 90
- 231
Habari wana JF,
Asilimia kubwa humu wazazi wetu wameishia elimu ya msingi na wengine hawakusoma kabisa, lakini wamepambana kwaajili yetu na kwakiwango kikubwa wamefanikiwa tumesoma sekondari na wengine mpaka chuo.
Hata wewe hapo ulipo unapambana mwanao afikie elimu ambayo wewe hukufika na ili kufanikisha hilo utatakiwa kumsomesha shule nzuri itakayomuandaa kufika huko.
Wakati unapambana na kujinyima ili upate ada na mahitaji yake, usisahau kujilipa na wewe kwa kuwekeza kwenye miradi itakayokuja kukuingizia pesa bila kufanya kazi wakati ambao hautakuwa na nguvu ya kupambana na kazi kama sasa.
Tena kuna wengine wanasomesha shule za gharama wakati wako kwenye nyumba za kupanga, hilo siyo tatizo lakini ni hatari sana kama mtoto akifeli halafu bili zimeisha na mwenye nyumba anataka kodi yake.
Tuwasomeshe kama jukumu letu na siyo kuweka malengo ya kula matunda yao. Mfano mzuri jitafakari wewe ni asilimia ngapi mpaka sasa mzazi wako amekula matunda yako?;Mfikirie yule baba na mama yako waliohangaika kwaajili yako wamenufaika nini kwako?
Na mpaka umri huu wa utu uzima kuna wengine tukikwama bado tunaomba msaada kwao. Tangu anazaliwa anakutegemea mpaka anafika chuo, akimaliza tayari ni mtu mzima anaoa au kuolewa anaanza majukumu kama mzazi, niambie hapo bado unatarajia matunda gani na hali ilivyongumu?
Tuwekeze wapendwa tusije kuwa ombaomba kwa watoto wetu, matokeo yake tutaanza kutia huruma kwa watoto waliotakiwa kutuheshimu. Huyo unayempigania leo, kesho atapigania familia yake kwanza kabla yako. Utapanda wewe lakini utakuwa wa mwisho kuvuna.
Wakati wewe unaishi kwenye nyumba ya tope, mwanao anaishi geti kali halafu anakwambia maisha magumu sana. Tujiandae tusije kuwalaumu watoto wetu na kuwapa laana. Na bado ukifa atarithi hicho kidogo chako, lakini yeye akifa unaweza usipate kitu.
Elimu ni muhimu sana lakini wakati tunapambana tusisahau kupanga maisha yetu ya baadae.