Kinuju
JF-Expert Member
- Mar 20, 2021
- 2,386
- 5,325
Tangu tarehe 17 mwezi march Tanzania imekumbwa na simanzi isiyo na kifani mara baada ya kutangazwa kwa kifo cha rais Magufuli.Mnamkumbuka yule mzee aliyempa Magufuli zawadi ya Jogoo kule Kilwa? Mzee Shaweji Kimbwembwe amepanda basi kutoka huko kijijini kwao kuelekea Dar ili apate fursa ya kumuaga Rais Magufuli.
Alimpa Rais Magufuli Jogoo baada ya kuelezea kadhia ya huduma hafifu za afya katika eneo lake la Somanga ikiwemo kina mama wanaojifungua wakati Rais akisalimia wananchi katika ziara zake. Rais Magufuli alimpa ahadi ya kujenga kituo cha afya na kutimiza ahadi hiyo.
Ndipo Rais alipopita kwa mara nyingine wakati akitoka kwenye mazishi ya Rais mstaafu, hayati Benjamin Mkapa akamzawadia Jogoo kwa kutimiza ahadi yake na kumuomba ampelekee mama yake mzazi Chato kwa kumfundisha wema na huruma kwa wanadamu, pia alimtabiria ushindi kwenye uchaguzi wa 2020.
Rais Magufuli alimpokea jogoo na kumtania kwamba siku akienda Chato atamkabidhi mama yake ali awe baba yake
I pray awahi kufika ili, asijekuta washaelekea Dodoma, roho yake ikamuuma.
Rais atasafirishwa kuelekea Dodoma, saa 11 jioni
PIA, SOMA=> Somanga: Rais Magufuli asikitishwa na uzembe wa Wizara ya Ujenzi kutokarabati barabara Somanga. Azawadiwa jogoo
Mamilioni ya watanzania wameangua kilio kila kona kwamba sasa mwokozi wao ameondoka, cha kushitusha ni kwamba wananchi wa hali ya chini kabisa ndiyo wanaoongoza kwa kilio kinyume na tulivyokuwa tumeaminishwa kwamba Magufuli alikuwa ananyonga wanyonge!
Kitendo cha hayati rais Magufuli kuagwa na mamilioni ya watanzania huku wakiangua vilio njia nzima na kutandika kanga zao chini ili mwili upite imeenda kinyume kabisa na wasaliti wa nchi hii akina Tundu Lisu na genge lake.
Kwa jinsi msiba huu unavyoenda naamini utakuwa darasa tosha kwa wasaliti wa nchi hii akina Tundu Lisu ,Godbless Lema, Chahali, Ngurumo, Mange Kimambi na wengine wengi, sasa wataelewa kumbe watanzania siyo vilaza.
Wataelewa kumbe watanzania wanajua yupi anapigania haki zao kwa vitendo na ni yupi ni mpiga makelele nyuma ya keyboard.
Kwa mapenzi haya yanayoonyeshwa na Watanzania kwenye msiba huu ni lofa tu atakayeendelea kuamini kwamba eti Tundu Lisu aliibiwa kura kwenye uchaguzi mkuu uliopita.
Wito wangu kwa wasaliti wa nchi hii wanaoshangilia msiba kwamba sasa Magufuli ameondoka watarudi Tanzania na kuanza tena kutumika kuiba rasilimali za nchi hii kama walivyokuwa wanafanya huko nyuma wajue tu kwamba wanapoteza muda.
Watanzania siyo vilaza ,wanajua fika Tundu Lisu aliwatisha kwamba watashitakiwa MIGA ikiwa watabadili sheria za madini.
Tundu Lisu aelewe kuwa hawezi kuwa rais wa Tanzania kwa kushinda Twitter akikejeli kila lililojema kuhusu nchi yetu,
Tundu Lisu kupitia msiba huu atakuwa ameelewa na kupata darasa kwamba ukitaka kupendwa na Watanzania tumikia watanzania na siyo kutumikia Acacia.