Mzee Baraka Shamte: Wanaosema uteuzi wa Samia haujafuata katiba ya CCM, hawajaisoma

Mzee Baraka Shamte: Wanaosema uteuzi wa Samia haujafuata katiba ya CCM, hawajaisoma

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,773
Reaction score
1,174
MZEE BARAKA SHAMTE AUNGURUMA KUHUSU KANUNI NA KATIBA YA CHAMA CHA MAPINDUZI

Mzee Baraka Shante ni Mtoto wa Waziri Mkuu wa Kwanza wa Zanzibar kabla ya Mapinduzi na Kada Mbobezi wa CCM na miongoni mwa waanzilishi wa Afro Shirazi Party Youth League Wing.


Baraka Shamte amesema wanaosema uteuzi wa Samia kugombea urais wanatumiwa na watu wa nje. Wengi wanaosema hayo ni watu wa nje ya CCM, kama ni watu wa CCM wanakuwa hawajasoma kanuni na katiba ya chama.

Amesema wanaotumiwa wamekuwa ni barakala na watu wa nje. Amesema wao watatoa hoja kuonesha namna gani Katiba na Kanuni imefuatwa kwenye uteuzi wa Samia kuwa mgombea urais kupitia CCM uchaguzi mkuu 2025.
 
Huyu mzee wa Zanzibar hana akili. Huyu ni mtoto wa Waziri Mkuu wa mwisho Zanzibar.

Anasema Tanzania imepata Director WHO na Rais wa Mabunge Duniani. Mzee anasema hakuna kiongozi mwingine aliyeahi kufanya hayo.

Mzee hamkumbuki Salim Ahmed Salim aligombea Katibu Mkuu UN , kisha kuwa Katibu Mkuu OAU hadi alipotaka kustaafu. Mzee Shamte hawajui akina Balozi Mahiga, Hashim Mbita, Sinde Warioba , Samwel Malecela, Rose Asha Migiro, Mama Getrude Mongela, Nyerere akiwa na akina Palme, Indira n.k. katika kamati ya watu 6 mashuhui duniani n.k. n.k..

JokaKuu
 
Mzee Baraka akili zimetulia tangu Afro wenzake walipomteka, wakamtesa kisha wakamtupa porini aliposema Hussin awapishe 2025.
 
Mvuuvi fulani tu huyu aliyenusurika kuwa teja akapata vyeo kwa ndondokela bila elimu ya kutosha
 
Wazanzibar kwenye kuteteana huokotaokota vihoja mradi tu chao kionekane kinafaa.
 
Safari hii tumeijua rangi ya wazenji huenda waliusubiri sana huu wakati
Ndiyo na nyinyi Watanganyika msirudie makosa kuwapa nchi yenu. Mtazidi kuumia, kiajira, kiuchumi, kiardhi na kwa kweli sijui kama Tanganyika itainuka tena kwa namna ilivyoporwa na wazanzibar na waarabu.
 
MZEE BARAKA SHAMTE AUNGURUMA KUHUSU KANUNI NA KATIBA YA CHAMA CHA MAPINDUZI

Mzee Baraka Shante ni Mtoto wa Waziri Mkuu wa Kwanza wa Zanzibar kabla ya Mapinduzi na Kada Mbobezi wa CCM na miongoni mwa waanzilishi wa Afro Shirazi Party Youth League Wing.
Hatumjuhi
Siku zote alikuwa wapi
 
Safari hii tumeijua rangi ya wazenji huenda waliusubiri sana huu wakati
Sera ya CCM ni mbili kuelekea moja. Wazanzibari watapigwa na butwaa lengo hili litakapotimia.

Mikakati ya kufanikisha lengo ipo na inatekelezwa taratibu na kwa umakini mkubwa.
 
Back
Top Bottom