Mzee Butiku: Mkataba wa Bandari umeshapitishwa, wanaposema tuzungumze, tuzungumze nini?

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
"Hili jambo la bandari limeshakwenda serikalini na bungeni, raia tukaulizwa maswali kidogo na tukajibu. Baada ya hapo jambo hili la bandari lilirudi bungeni na kupitishwa na Bunge. Kwa mujibu wa utaratibu wa kikatiba, limeshapitishwa na hivyo ni la kutekeleza. Hivyo sasa wanaposema tuzungumze, tuzungumze kitu gani?" Joseph Butiku, Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere
 
Ni ajabu sana.

Yaani ni sawa na kusema kwamba mtuhumiwa amefikishwa Mahakamani na kisha akahukumiwa moja kwa moja adhabu ya kifungo gerezani bila ya mtuhumiwa mwenyewe kusomewa mashtaka yake wala bila ya kupewa nafasi ya kujitetea kwa tuhuma zake. Kisha baadaye wakati mtuhumiwa huyo yupo kwenye kifungo gerezani akitumikia adhabu aliyohukumiwa, ndipo anaambiwa kwamba sasa unaweza kuanza kujitetea kwa makosa yako uluyotuhumiwa nayo mpaka yakakusababishia kwenda jela na kufungwa gerezani
 
useless

bunge letu
 
Attachments

  • images.jpg
    images.jpg
    28.2 KB · Views: 2
"Hili jambo la bandari limeshakwenda serikalini na bungeni, raia tukaulizwa maswali kidogo na tukajibu. Baada ya hapo jambo hili la bandari lilirudi bungeni na kupitishwa na Bunge. Kwa mujibu wa utaratibu wa kikatiba, limeshapitishwa na hivyo ni la kutekeleza. Hivyo sasa wanaposema tuzungumze, tuzungumze kitu gani?" Joseph Butiku, Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere
Majaliwa ni mtu mwongo sana
 
Aiseeh! Kumbe mambo tayari
Ccm inawachora tu wananchi wanavyobweka!

Anyway waTz 2025 sio mbali sasa hivi ni zamu ya waTz kuishangaza ccm hili chozi lilipwe!
 
Hiyo kauli yao ya tuzungumze inaonesha vile wasivyojielewa, wameshaharibu, wanajua hawana majibu ya uharibifu wao, sasa wamebaki kuokoteza maneno ilimradi watujibu, maneno yenyewe ndio hayo yasiyokuwa na maana yoyote.
 
Aiseeh! Kumbe mambo tayari
Ccm inawachora tu wananchi wanavyobweka!

Anyway waTz 2025 sio mbali sasa hivi ni zamu ya waTz kuishangaza ccm hili chozi lilipwe!
Usijidanganye. Kamwe CCM haiwezi kuondoka madarakani kwa uchaguzi wa siasa au kutokana na kukosa kura kwenye uchaguzi wa siasa. Usitarajie Jambo hilo kutokea hapa Tz.
 
Kuondoka inaweza ila sio kwa juhidi ya nyie keyboard warriors mitaani suala la bandari halipo kabisa.
 
Hivi CCM imeamua kuuza kila kitu kwa faida ya nani?
1. Migodi
2. Mbuga za wanyama (ngorongoro na Loliondo
3. Vitalu vya Gas mtwara/Lindi
4. Na sasa Bandari
 
Kuondoka inaweza ila sio kwa juhidi ya nyie keyboard warriors mitaani suala la bandari halipo kabisa.
Ungepata kunifahamu wala hata usingeniita kwamba Mimi ni "keyboard warrior", ila nakupa pole sana kwa hilo. "Wenzako" wananifahamu vizuri sana, tena sana tu, natumaini watakujulisha vizuri ya kunihusu.
 
Mbona CCM hujaipundua mpaka leo kama wewe ni mkali, badala ya kupambana mambo muhimu ya taifa kama katiba rule of law, eti unapambania bandari....
 
CCM acheni kiburi, sikilizeni hawa wazee waasisi wa TANU.
 
Back
Top Bottom