Mzee Chapuo wa 'Maskani ya Kapten G Habash'

matumbo

JF-Expert Member
Joined
Jul 9, 2011
Posts
7,224
Reaction score
3,951
Mwenye kumfahamu vizuri uyu Mzee Chapuo anayetangaza ndani ya kipindi cha Maskani Times Fm kinachoongozwa na Kapt Gadna G Habash atufahamishe.
Nimemsikia juzi na leo kwenye kipindi,naweza kusema uyu mtu ni kichwa haswa,na 'star' mpya kwenye game ya utangazaji wa 'ucheshi' lakini ameibuka ghafla mno binafsi sijui lolote kuhusu background yake,na uzoefu wake kwenye hii tasnia.mwenye kumfahamu atujuze haswa mimi binafsi ambaye nimetokea kumkubali.

Nb:ukiona matumbo kamkubali mtu, ujue uyo mtu ni mkali haswa.
 
Ngoja waje..

mkuu kwani we haujamskia bado uyu Mzee??tafuta muda siku moja jioni umskie,mimi binafsi kanikosha sana.niliacha kuskiliza redio za kibongo ila kanirudisha kwa ss nikitoka mitkas nikiwa foleni lazma nimtafute nimskie.
 
Huwa namkubali pia mgosi mkoloni kwenye malalamiko
 
Gadna ana kipaji sana,Maskani naweza kusema ndio kipindi bora cha jioni kwa sasa..na mzee Chapua anatisha ile mbaya,nilimskia siku moja anapiga stori ya zamani kinyozi ananyoa na kiwembe kile kama kisu alafu ikatokea anamnyoa mtu aliyemtongoza mkewe,nilicheka siku nzima siku iyo.
 
Mwenye kumfahamu vizuri uyu Mzee Chapuo anayetangaza ndani ya kipindi cha Maskani Times Fm kinachoongozwa na Kapt Gadna G Habash atufahamishe.
Nimemsikia juzi na leo kwenye kipindi,naweza kusema uyu mtu ni kichwa haswa,na 'star' mpya kwenye game ya utangazaji wa 'ucheshi' lakini ameibuka ghafla mno binafsi sijui lolote kuhusu background yake,na uzoefu wake kwenye hii tasnia.mwenye kumfahamu atujuze haswa mimi binafsi ambaye nimetokea kumkubal
Nb:ukiona matumbo kamkubali mtu, ujue uyo mtu ni mkali haswa.

Namfagilia sana huyo jamaa kwanza haishiwi story za kufurahisha pili jinsi anavyoaanza kuisimilia hakika anakipaji sana
 
Mzee chapuo ni mchekeshaji wa sikunyingi wa KBC Nairobi... Enzi hizo miaka ya 90's walikua na kipindi chao kinaitwa Janja na janjaule...
 
Huyu ni Chapuo Chepeo Chap Chap Mla Chake wa late 80s ...alikuwa Kenya, enzi hizo tuliangalia sana vichekesho vyake. Hapo bado TZ hakuna mitambo, lazima uwe na ariel ndeeefu kuona Kenya na ZnZ kama hutaki chenga zitawale
 
yap nimekusoma..kumbe wa kitambo.sasa mbona hana lafudhi ya kikenya?
 
madame ulimwangalia miaka ya 80??duh nyie video na antena mlikuwa nazo kitambo sana!
 
kipindi
ni
muda
gan?naomba
mnifahamishe.
 
yap nimekusoma..kumbe wa kitambo.sasa mbona hana lafudhi ya kikenya?

Asili yake MTZ kama sikosei au mtu wa pwani ya kenya, lakini alikuwa hatumii accent ngumu ya kikenya si unajua usanii
 
ukitaka kumsikiliza vizuri, sikiliza kila jumapili saa 2 hadi 4 asubuhi times fm anakipindi cha taarabu asilia. jaribu kumsikiliza vizuri hapo ..
 
mkuu kwani we haujamskia bado uyu Mzee??tafuta muda siku moja jioni umskie,mimi binafsi kanikosha sana.niliacha kuskiliza redio za kibongo ila kanirudisha kwa ss nikitoka mitkas nikiwa foleni lazma nimtafute nimskie.

duh.! Mi nipo makalioni mwa nchi hiyo redio haifiki tunaisikia tu kwenye magazeti..hicho kipindi ni saa ngapi na siku gani siku nikitembelea dar nimsikilize.!
 
Mwenye kumfahamu vizuri uyu Mzee Chapuo anayetangaza ndani ya kipindi cha Maskani Times Fm kinachoongozwa na Kapt Gadna G Habash atufahamishe.
Nimemsikia juzi na leo kwenye kipindi,naweza kusema uyu mtu ni kichwa haswa,na 'star' mpya kwenye game ya utangazaji wa 'ucheshi' lakini ameibuka ghafla mno binafsi sijui lolote kuhusu background yake,na uzoefu wake kwenye hii tasnia.mwenye kumfahamu atujuze haswa mimi binafsi ambaye nimetokea kumkubali.

Nb:ukiona matumbo kamkubali mtu, ujue uyo mtu ni mkali haswa.

Kwenye maskani naona humfaidi vzr tune times fm kila j2 kuanzia saa 3 hadi 5 asubuhi ana kipindi cha taarab asilia na huyu mtu amekaa sana mombasa
 
Back
Top Bottom