TANZIA Mzee David Makerege (80) Afariki Dunia Akiwa Chumbani Kwenye Hoteli ya Mbezi Garden Jijini Dar es Salaam

TANZIA Mzee David Makerege (80) Afariki Dunia Akiwa Chumbani Kwenye Hoteli ya Mbezi Garden Jijini Dar es Salaam

Mzee wa miaka 80 alienda kupiga kazi ya miaka 33 huku akiwa na 37,000 mfukoni baada ya chipsi na mishkaki 3.

Inasemwa kwamba daktari ndiye anaweza declare mtu kufariki, hivyo huu uongozi wa gesti kudai uligundua mteja wao amefariki na kuamua kutaarifu polisi ni move sahihi kweli?

As walitumia kipimo gani? Achana na muvi ule mtindo wa kusikiliza kifua... Mimi naona na mtu aliyetoa taarifa ya kifo angehojiwa pia.
Tukirudisha umri wa marehemu miaka 33 nyuma,tunakutana na kichwa cha habari mzee wa Miaka 50 afikishwa mahakamani kwa kosa la kubaka kitoto kichanga cha mwaka mmoja.
 
AFANDE RPC (R)RCO(R)STAFF OFFICER (R)OPP OFFICER (R)OCD MABWEPANDE


YAH: TUKIO LA KIFO CHA MASHAKA
GBA/IR/142/2021

MLAL: O.A.MSHANGAMA - ASP

Mlalamikaji anaeleza kuwa mnamo tarehe 16/1/2021 majira ya saa 18:00hrs akiwa kituo cha polisi Mabwepande alipokea taarifa toka kwa incharge CID Goba A/Insp. Gwake kuwa huko Mbezi Makonde katika hoteli ya Mbezi Garden kuna mteja amefariki chumbani(x)

Taarifa kamili ni

Kwamba mnamo tarehe 16/01/2021 majira ya saa 17:55hrs huko goba kituo cha polisi(x) a/insp.gwake mwakapande alipokea taarifa toka kwa meneja wa hoteli ya mbezi garden aitwaye Newton s/o Simkonda, Mnyiha, 44yrs, Mkristo, Meneja, mkazi wa Ukonga Majohe(x)kuwa huko Mbezi Garden hotelini kwake katika wlaya ya kipolisi Mabwapande na mkoa wa Kinondoni kuna mteja amefariki dunia chumbani alipokodi akiwa na mwanamke wake(x)baada ya taarifa hiyo kupokelewa Mkuu wa Upelelezi Mabwepande pamoja na I/C CID Goba walifika eneo la tukio na kumkuta mwanamke aitwaye Neema d/o Kibaya, Mpare, 33yrs, biashara, Mkristo, mkazi wa Goba Marobo aliyekuwa na marehemu na (x) kueleza kuwa alifika hotelini hapo leo tarehe 16/01/2021majira ya saa 15:00hrs walipokuwa wamekubaliana wakutane na kumkuta marehemu ameshachukua chumba namba 22 akiwa na maji na juice(x)

Baada ya kufika aliweza kuagiziwa chips na mishikaki mitatu na marehemu(x) akiwa anasubiria chips hizo huku wakiwa wanaendelea maandalizi ya tendo la ngono(x) ghafla alimwona marehemu akipumua kwa shida ndipo akatoka kwenda mapokezi kuomba msaada(x)baada ya taarifa wahudumu waliongozana na uongozi wa hoteli walifika na kumkuta marehemu haongei na hafanyi chochote huku akiwa ametoa macho ambapo uongozi wa hoteli ulibaini kuwa mteja wao amefariki dunia (x) ndipo meneja akachukua jukumu la kuwajulisha polisi ambapo walifika eneo la tukio.

Katika uchunguzi wa awali uliofanyika mwili wa marehemu haujakutwa na jeraha lolote (x). Katika upekuzi marehemu alikutwa na simu aina ya tecno na pesa Sh. 37,000/=na kitambulisho cha mpiga kura na kuweza kumtambua kwa jina la Davis Makerege Mabeba, Mluli, 80yrs, Mkristo, mkazi wa Goba kwa Ndambi(x)mwanamke aliyekuwa na marehemu chumbani anashikiliwa kituo cha polisi goba kwa mahojiano(x)tukio limekaguliwa na OC CID Mabwepande O. A Mshangama ASP akisaidiana na Incharge CID Goba A/Insp. Gwake pamoja na timu ya makachero (x)

Mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Mwananyamala kwa uchunguzi (x) taarifa kituoni na Newton S/O Simkonda na kupokelewa na J 92 PC Inocent leo 16/01/2021 saa18:44hrs(x) fcr maendeleo zitafuata(x)

-Mwisho-

Toka Crime Mabwepande

====

David Makerege (80) Mkazi wa Goba Dar es salaam amefariki Dunia akiwa kwenye Hotel ya Mbezi Garden (chumba No.22), January 16,2021, Polisi Kinondoni wamethibitisha.

“Kwenye chumba hicho tulimkuta pia Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Neema Kibaya (33) ambaye ameeleza kuwa Marehemu alikuwa ni Mpenzi wake”- POLISI

“Uchunguzi wa awali umeonesha mwili hauna jeraha lolote, baadaye mwili ulipelekwa Hospitali ya Mwananyamala kwa ajili ya uchunguzi zaidi na hifadhi” -POLISI
View attachment 1680143View attachment 1680144

Sent using Jamii Forums mobile app
Atafufuliwa kila moja juu lile alilofia juu yake.
Hakuna kupumzika huko
 
Mzee wa miaka 80 alienda kupiga kazi ya miaka 33 huku akiwa na 37,000 mfukoni baada ya chipsi na mishkaki 3.

Inasemwa kwamba daktari ndiye anaweza declare mtu kufariki, hivyo huu uongozi wa gesti kudai uligundua mteja wao amefariki na kuamua kutaarifu polisi ni move sahihi kweli?

As walitumia kipimo gani? Achana na muvi ule mtindo wa kusikiliza kifua... Mimi naona na mtu aliyetoa taarifa ya kifo angehojiwa pia.
Inasemwa wapi, Tanzania watu wanazikaga tuu bila hata taarifa kuwafikia hao maDR au police. Unakuta mtu kafa asubuhi kazikwa jioni hila hata kujua labda alikuwa kazimia tuu
 
Mungu amsamehe huko aendako,, Mimi Sio daktari,, lakini VIAGRA hizi ni mtihani mkubwa,,,
Tangu mwanzo wakati nasoma tu huu uzi akili yangu ikaanza kusense kwenye Viagra. Sio mchezo. Mzee alitaka pesa yake iende ki halali,,, Siku hizi wenzie wanatumia "Vumbi la Congo", Viagra wameshaishitukia, hakunywa maji ya kutosha huyo..
 
Back
Top Bottom