Hivi huyu huyu Sumaye, na miaka yake hii mi nne akiwa CHADEMA, alitaka ashike uongozi wa juu kabisa (M/kiti ) wa CHADEMA? Serious?
Hivi hajui kwamba, hata kumpa uwenyekiti wa Kanda, ilikuwa ni heshima kubwa mno kwake?
Kwake demokrasia nikuongoza wengine tu, siyo wengine kumwongoza?
Kwamba, kuwa mgombea pekee Kanda ya Pwani kwake ilikuwa demokrasia, ila wapiga kura kumkataa, kwake imekuwa sio demokrasia?
Hivi huko ccm, anaubavu hata tu wa kutangaza nia ya kuchukua fomu ya kugombea uenyekiti wa ccm taifa, achilia mbali kugombea kwenyewe?
Hivi hawa watu wanaokuwa wamekimbia CCM na kwenda vyama pinzani, wana matatizo gani?
Wanadhani ubabe ubabe walikuwa nao huko ndio huo huo wanaweza kuutumia na kule?
Halafu unashangaa kabisa mtu ana sapoti ujinga ujinga wa mzee huyu!!
Kwanza, binafsi nimefurahishwa sana na uamzi wake wa kupumzika siasa, ingawa najua kabisa amerudi nyumbani "time will tell"
Kwa kuwa naiona chadema isiyo na makandokando inazaliwa tena.
Pili nashauri (Kama alivyowahi kushauri humu wakili msomi P. Mselewa) kwamba, ni mda mwafaka kwa CHADEMA na vyama vya upinzani kwa ujumla, kuwatimua wooote waliotoka ccm kwa mihemko ya kukosa vyeo au nafasi za kugombea, warudi walikotoka.
Na Kama mtabaki nao, msiruhusu kuwapa vyeo mapema au nafasi za kugombea mapema (kama Lowassa) badala yake muwe na mda mrefu wa kuwapima. Pole mr. 0