Mkubwa unahangaika bure tu kujaribu kuweka sawa uelewa na ufahamu wa jamaa wa chama cha kijani ambao wameamua kutoa tafsiri yao ya jambo rahisi linaloeleweka kama hili ili mradi tu kupaint picha waitakayo juu ya mtu huyu wanayemchukia kupita maelezo ya kawaida.....
Kwenye hotuba hiyo hiyo ametoa statement nyingine inayofanana na hii hii inayotafsiriwa na kila anayeamua kupotosha ili mradi tu kila asiye mpenda Bw Freeman Mbowe afurahishe nafsi yake kwa muda fulani....
Katika hotuba hiyo amesema pia hivi;
"......baada ya chaguzi hizi, CHADEMA inakwenda kuunda KIKOSI HATARI...."
Sasa sijui wasiompenda Freeman Mbowe, watatengeneza tafsiri gani tu ktk kauli hii kwa mara nyingine.....
Usishangae baadaye kwenye platforms mbalimbali za propaganda za jamaa wa nguo za kijani kukutana na vijihabari vya umbea na title za habari kama;
"MBOWE ASEMA ATAUNDA KIKOSI HATARI KUVURUGA AMANI YA NCHI"
au
"MBOWE AAHIDI KUUNDA KIKOSI HATARI CHA KURUSHA MABOMU"