Mzee Jakaya Kikwete, rudisha hilo hekalu Serikalini lipigwe mnada pesa zisaidie wananchi

Mzee Jakaya Kikwete, rudisha hilo hekalu Serikalini lipigwe mnada pesa zisaidie wananchi

Ukikubali matunda ya unyonyaji na wewe ni mnyonyaji hata kama unyonyaji huo umehalalishwa na sheria mbovu.

Hiyo sheria siyo ya leo ni ya toka enzi za Mkapa ambayo naye alikuwa waziri mwandamizi, Pia alipokuwa rais alikuwa na uwezo wa kuibadili alipokuwa rais lakini aliiacha maana yske ni kuwa potentially aliridhika na sheria hiyo huku akijua naye ni mnufaika ajaye wa hiyo sheria, na kweli leo kanufaika!, Ukiachilia mbali hilo, hata alipopewa wazo la kujengewa angekuwa muungwana kweli angekataa, lakini naamini alishiriki kikamilifu hata kupendekeza ramani Hekalu lake lionekaneje!

Siku hizi wakitaka kufanya dhulma wanazitungia sheria ili kuhalalisha dhuluma zao. Mfano wa utaratibu huohuo ni kama walioutumia Kutunga sheria za Spika, Waziri Mkuu, Naibu Spika wasishtakiwe, kwa sababu walikuwa na malengo yao vichwani mwao, pfobably hata ya kufanya dhuluma katika nchi.

Kwa hiyo huko Mbeleni Watu wakitaka kumwajibisha Ndugai kwa kuvunja katiba kuna kundi la watu litaibuka kumtetea kwa kisingizio cha sheria kuwa "Sheria inamlinda, kwamba Ilaumuni sheria na si Ndugai"
Hkn kitu km hicho eti ufanye makosa mtu akutetee!! Huo ni uongo na majungu ya kiswahili!!

Watu wakiwa na ghadhabu wanakushusha mzima mzima na hkn wa kuwazuia
Al bashir yuko wapi leo??
Mtoto wa Hisene habre analia na moto weeee!!!

Watu wakikukataa wamekataa tu.

Wewe unatamka km wewe ukimgusa kikwete wafwa.....Anakubalika...Gwajima yuko wapi,? Ameshuka ziiiii!!! Hapo ni
Baada ya kumsema kikwete!!

Bora asingeenda kujianika huko!! Ataporomoka!!! nzi ana afadhali!!
 
Sheria ilikuwepo toka wakati wa Mkapa.
Mkapa hakumjengea Nyumba Mwinyi.

Kikwete alipo ingia Madarakani, hakumjengea Mkapa.

Ila JPM, Mzalendo, Msomi wa PhD alipata uchungu baada ya kuona lile HEKALU la Mkapa pale Lushoto-Tanga ni kijunba kisicho na hadhi ya Rais Mstaafu. Akaamua mjengea nyumba Mkapa.

Mzalendo na Kipenzi cha Wanyonge aliona lile Jumba la Mwinyi pale Mikocheni ni kijumba hakina hadhi ya Rais, pia aliona lile Kasri la Mzee Mwinyi pale Zanzibar (Maisara) ni kijumba hakimfai Mzee Mwinyi akaamua kumjengea dude JINGINE UFUKWENI.

Mzalendo na Jemedari aka JEMBE aliona ile nyumba mitaa ya Ursino haina hadhi ya kukaa Kikwete lakini pia aliona lile HEKALU la Msoga ni kijumba kisicho na HADHI akaamua mjengea JUMBA la Hadhi Mh Kikwete.

Hakuishia wajengea nyumba tu, pia aliwagawia TAUSI wa IKULU baada ya yeye kujigawia na kuwapeleka CHATO.

Werevu wanajua kwanini RAIS MWENYE PhD ya Sayansi aliyafanya haya.
Alitekeleza sheria kama ambavyo wabunge ukigusia zile posho zao wanajibu kuwa zipo kwa mujibu wa sheria, kwahiyo tatizo ni sheria.
 
Hatuna umasikini huo WA kushindwa kuwajengea Ma Rais wastaafu..

Nyumba hiyo moja thamani yake si pesa za mbunge aliestaafu?Na wabunge wako wangapi?..

Kama tuko serious tuanze na kupunguza mishahara ya wabunge...na posho na kiinua mgongo...

Mtu akishakuwa Rais hata akistaafu anapata wageni mbalimbali wa wa kimataifa

Tuache kuwaza kimasikini kuwa nyumba ni sehemu Tu ya kulala...

Sioni tatizo kabisa Kwa wastaafu kupewa nyumba wala magari...

Hata makampuni huwa yanatoa bonuses Kwa ma CEO wao...hata kama mishahara ya watu wa chini midogo..

Urais ni ofisi hata ukisha staafu
Hao wageni wa kimataifa hawajui nchi yetu ni masikini? Kwa hiyo wewe ukitembelewa na mgeni uko tayari kukopa umchinjie ng'ombe akuone u tajiri huku familia yako haina uwezo ? Yaani unafurahia 'show off' kwa wageni badala ya furaha kwa wananchi? Lengo la KIKWETE kuomba urais ilikuwa kuwa mtumishi wa wananchi ama mzigo kwao? Na elimu yote aliyonayo anashindwa kuona mzigo wa ufukara waliobebeshwa na serikali kugharamia anasa za viongozi walioko madarakani na waliostaafu! Kweli uhuru wetu ulikuwa kubadilisha rangi za wakoloni tu.
 
Hujajibu swali nililokuuliza na ulilojibu sijakuuliza.

Mbunge wako anayeweza kupeleka hoja ya kubadili sheria bungeni umemuandikia?
Mbunge wangu yupi katika hawa walioingia bungeni kimagumashi?
Yaani kesi ya Ngedere nitafute wakili nyani? —You are not serious
 
Lakini c mlipewa magufuli mkamtukana? Wacha mama agawe tu mali za serikali na matajiri wenzie, sie akina kajamba nani tulie na kusaga meno
 
Mbunge wangu yupi katika hawa walioingia bungeni kimagumashi?
Yaani kesi ya Ngedere nitafute wakili nyani? —You are not serious
Hahaaa,

Watanzania wengi ni mahodari w kupiga kelele JF lakini kubadili mambo ya msingi hawataki.

Sasa hao wabunge magumashi umeavhiaje wakaingia bungeni?

Na kama wewe umeachia wbunge magumashi waingie bungeni, wewe huna lawama kuchia wabunge magumashi waingie bungeni kupitisha miswada magumashi?

Kwa nini na wewe usiwe sehemu ya watu walioruhusu magumashi Tanzania?
 
Nilitumia haki yangu ya kupiga kura, lakini yaliyotokea baada ya hapo ni ya kisikitisha ni ujambazi kwenda mbele. Sasa nashangaa unataka nimtume jambazi kwenye kikao cha majambazi kwenda kuomesha ujambazi. It foesn't work
 
Umeshindwa kuzuia ujambazi wa kumfanya jambazi kuwa mbunge, una tatizo kubwa kuliko Kikwete kukurudishia jumba hilo.

Kwa sababu hata Kikwete akikurudishia jumba hilo, huna uhakika kwamba hatapewa jingine kubwa kuliko hilo, kisheria.

Jipange kubadilisha sheria, sio kuleta mngonjera JF na kuleta threads za uanaharakati wa kick.

Kikwete mwenyewe aliposakamwa na kusikia alishasema "ni upepo tu, utapita".

Sasa wewe ambaye unaleta uanaharakati wa JF hatujui hata kama kakusikia unategemea arudishe jumba kweli au unamaliza hasira zako tu hapa JF?
 
Ndugu yangu nimekuelewa vizuri.Hapa kuna sheria ambazo zimegawanyika katika makundi mawili makubwa.Zipo zenye hasara na kuumiza na zipo zenye hasara "laini".Hasara inayoumiza ni kama hii ya kinga kwa watu kama Ndugai na wengine,sheria za uhujumu uchumi,sheria za mitandao,n.k.Hii inawapelekea kufanya watakavyo bila kujali madhara yake na huku wakiitegemea kinga hiyo.Lakini kuna hizi sheria zenye hasara "laini" ambazo katika maisha ni vitu vya kawaida.Jakaya kupewa kasri ni suala tu la sehemu na thamani ya eneo (valuation basis).Kajengewa nyumba Masaki au Mikocheni.Mchanga ni huu huu na hautoki Ujerumani,Cement ni ileile ya Wazo Hill au dangote,Nondo ni hizi hizi ,kokoto ni zile zile za kunduchi,mafundi ni wale wale,Matofali ni yale yale na ya ardhi hii hii ya Tanzania.Tofauti iliopo ni sehemu gani na pana hadhi gani,basi.Kasri hilo hilo likijengwa Vingunguti au Chanika impact yake itakuwa ndogo sana kuliko Masaki.

Ukikubali matunda ya unyonyaji na wewe ni mnyonyaji hata kama unyonyaji huo umehalalishwa na sheria mbovu.

Hiyo sheria siyo ya leo ni ya toka enzi za Mkapa ambayo naye alikuwa waziri mwandamizi, Pia alipokuwa rais alikuwa na uwezo wa kuibadili alipokuwa rais lakini aliiacha maana yske ni kuwa potentially aliridhika na sheria hiyo huku akijua naye ni mnufaika ajaye wa hiyo sheria, na kweli leo kanufaika!, Ukiachilia mbali hilo, hata alipopewa wazo la kujengewa angekuwa muungwana kweli angekataa, lakini naamini alishiriki kikamilifu hata kupendekeza ramani Hekalu lake lionekaneje!

Siku hizi wakitaka kufanya dhulma wanazitungia sheria ili kuhalalisha dhuluma zao. Mfano wa utaratibu huohuo ni kama walioutumia Kutunga sheria za Spika, Waziri Mkuu, Naibu Spika wasishtakiwe, kwa sababu walikuwa na malengo yao vichwani mwao, pfobably hata ya kufanya dhuluma katika nchi.

Kwa hiyo huko Mbeleni Watu wakitaka kumwajibisha Ndugai kwa kuvunja katiba kuna kundi la watu litaibuka kumtetea kwa kisingizio cha sheria kuwa "Sheria inamlinda, kwamba Ilaumuni sheria na si Ndugai"
 
Lakini c mlipewa magufuli mkamtukana? Wacha mama agawe tu mali za serikali na matajiri wenzie, sie akina kajamba nani tulie na kusaga meno
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] mother Theresa anadai yeye ni mwenye huruma sana.

Sent from my Infinix X652C using JamiiForums mobile app
 
Wote ni Wanyonyaji tu. Hivi Magufuli hakujiuliza kwa nini wenzake hawakujengeana mpaka yeye akaamua kuwajengea wote.... Tatizo lilikuwa wapi?

Kikwete anadai ni haki yake, mbona sasa yeye hakumjengea Mkapa na Mwinyi mpaka wakasubiri Magufuli awajengee...!!

Kwa maoni yangu binafsi, huu ni muendelezo wa kujirundikia mali na matumizi mbaya ya pesa za wananchi.
Najua Magu alifanya hivyo maksudi, ili kuwapumbaza wenzake kwa aliyokuwa anafanya Chato.
 
Hatuna umasikini huo WA kushindwa kuwajengea Ma Rais wastaafu..

Nyumba hiyo moja thamani yake si pesa za mbunge aliestaafu?Na wabunge wako wangapi?..

Kama tuko serious tuanze na kupunguza mishahara ya wabunge...na posho na kiinua mgongo...

Mtu akishakuwa Rais hata akistaafu anapata wageni mbalimbali wa wa kimataifa

Tuache kuwaza kimasikini kuwa nyumba ni sehemu Tu ya kulala...

Sioni tatizo kabisa Kwa wastaafu kupewa nyumba wala magari...

Hata makampuni huwa yanatoa bonuses Kwa ma CEO wao...hata kama mishahara ya watu wa chini midogo..

Urais ni ofisi hata ukisha staafu
Basi wajengewe ofisi na sio Mahekalu ya gharama kubwa. Maana ofisi km ofisi gharama yake ni around mil.20 au 30 sio hayo Mahekalu yenye thamani ya bil.1.5 +
 
Barua ya wazi kwa Rais mstaafu Kikwete.

Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu

Nakuandikia barua hii mimi kama raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuonesha kukasirishwa, kutopendezewa na kitendo cha serikali yetu kukujengea Jumba kubwa utadhani Kasri la Wafalme na wewe bila haya au aibu unalipokea kwa bashasha bila kujali kuwa nchi hii bado ni masikini sana na bado ina uhitaji mkubwa sana wa kila senti kwenda kuondoa umasikini wa kutisha wa watu wetu.

Ninafahamu kuwa mlijitungia sheria kuwa mstaafu akistaafu basi apewe pakeji nono ikiwemo kujengewa nyumba, licha ya kwamba hukuwa rais wakati sheria hiyo inatungwa, lakini ulikuwemo serikalini wakati inatungwa, baadae ukawa rais na hukuirekebisha hiyo sheria!, Na wala hujawahi kusikika popote kuonyesha kutofurahishwa na Mzigo mzito wa sisi wananchi kuwagharamieni nyinyi wastaafu kupitia kodi zetu.

Ndugu Jakaya Rais mstaafu, hebu niambie, wewe kama mtu uliyefanya kazi kwenye chama na serikali toka mwaka 1975 hadi mwaka 2015 ina maana hadi ulipostaafu, yaani jumla ya miaka 40 hukujenga nyumba yoyote?, ina maana miaka yote hiyo ulikuwa unapanga? —ina maana uliacha kujenga nyumba ukitarajia kuwa one day utakuwa raisi ili ukistaafu ujengewe nyumba kwa kodi za wananchi?

Ndugu Jakaya, Je nyumba yako ya Msoga haikutoshi? Unataka tena hilo hekalu ulipeleke wapi? Unataka umuachie urithi Ridhiwani?, umuachie urithi Miraji?, Umuachie urithi Mama Salma kupitia jasho la wananchi?

Nakuandikia barua hii nikitambua kuwa ulikuwa kijana wa TANU wewe, na nyie vijana wa kipindi hicho mlikuwa mkituaminisha kuwa mmeiva kwenye Itikadi za kukataa "unyonyaji",Najiuliza, kama mliweza kuwaaminisha wananchi kuwa siyo wanyonyaji na wakawaamini mpaka kuwapa nyadhifa kubwa huko mbeleni, mbona basi mnageuka wanyonyaji katika kustaafu kwenu?—Ina maana mikogo yenu ile ya kipindi hicho ya kujifanya siyo wapenda kujitajiriisha kwa kutumia kivuli cha nyadhifa zenu ilikuwa feki?. Mnapata wapi usingizi wa kuenjoy mimali yote hii katikati ya lindi zito la umasikini wa watu wenu tena kwa kujitajirisha kupitia jasho lao?

Ndugu Jakaya, mimi sitaki kukueleza umasikini wa nchi hii kwa sababu unaujua, Umeujua ukiwa bado kijana na unaujua ukiwa mzee—Hebu tutazame sisi wananchi walalahoi machoni, ambao masilahi yetu tunaambiwa hatuwezi kupata kwanza kwa sababu uchumi wa nchi umeshuka, kisha tuambie ndugu Jakaya, hilo hekalu lako ulilojengewa na serikali uliyopambana sana kuiweka madarakani linatusaidiaje sisi wananchi kuondoa adha za ukosefu wa maji, Ukosefu wa madawa, ukosefu wa madawati, upungufu wa ajira kwa vijana wetu, masilahi ya wakulima na wafanyakazi?

Ndugu Jakaya, wewe unalipwa asilimia 80 ya mshahara wa rais aliyeko madarakani, hivyo ndivyo nyie wanene mlivyojipangia, Unashindwaje kwa mshahara kujijengea nyumba nyingine ukiihitaji mpaka serikali ikujengee Hekalu lote hilo kwa kodi za wananchi?

Najua unaweza kusingizia kuwa eti hivyo ndivyo sheria inavyotaka, lakini je kwani ungekataa kujengewa hilo hekalu ungelazimishwa?, Na kama ukilazimishwa kwani huwezi kulikataa?

Nakuandikia haya huku nikijua kuwa Rais Mkapa alijengewa Jumba lake, Mwinyi akajengewa Kasri lake na wewe leo umekabidhiwa Hekalu lako. Katika wote hao nimeamua nikuandikie wewe barua hii ya wazi kwa sababu Mzee Mkapa hatunaye, hawezi kujibu, Mzee Mwinyi ni mtu mzima sana, ni dhahiri anasukumiziwamo tu, Ila wewe bado una nguvu uko active na bila shaka unafuatilia kwa karibu sana yanayojiri nchi hii!

Kuna swali moja tu ningependa unijibu, JE TANU ILIWAFUNDISHA VIJANA WAKE MKIPATA MADARAKA AU KUSTAAFU MGEUKE WANYONYAJI?

Jakaya nakuomba kwa heshima na taadhima, wewe umeshiba, wenye njaa nchi hii ni wengi, wananchi wenye uhitaji wasioweza kumudu mahitaji yao ya msingi ni wengi, Hilo hekalu lako linaweza kujenga maelfu ya vyumba vya madarasa kusaidia watoto ambao wanafaulu darasa la saba lakini hawawezi kuendelea kutokana na upungufu wa madarasa nchini. Hilo hekalu lako ni zaidi ya Zahanati 50, Hilo hekalu lako ni zaidi ya madawati 5000.

Hebu niambie Jakaya mtu mwenye majumba, una familia yenye kipato kizuri, Unawezaje kukubali kuwa na Hekalu lote hilo kwa jasho la wananchi wenye uhitaji wa kila senti ya jasho lao?

Tafadhali rudisha hilo hekalu kwa wananchi liwasaidie, ukifanya hivyo utakuwa muungwana sana!
Huna lolote wivu tu na roho mbaya
 
Back
Top Bottom