Mzee Jakaya Kikwete, rudisha hilo hekalu Serikalini lipigwe mnada pesa zisaidie wananchi

JK Ramona haya Bali alikuwa goigoi kutekeleza mipango ya maendeleo na sharia, kwani alikuwa busy nagano kuzunguka Dunia! JPM ngosha in bingwa wa kutekeleza mipango yote ya maendeleo na ni msomi mzuri na mfuatiliaji wa mambo na hivyo kuyaibua hata yaliyozikwa!
Kama JK angekuwa na haya hakika angeikataa hiyo nyumba!
Alikuwa na haya kuijenga ila kupokea... Hakuna haya....!!
 
They rightly say, When you see smoke rising, then there is fire. And you won't believe it!???
Pole Sana!Kwa taarifa tu hakuna juu ya jiwe litakalo salia.Tutayasaga tote.Waambie ndugu zako watulie 25 hakuna jina litakalorudi.
 
Hatuna umasikini huo WA kushindwa kuwajengea Ma Rais wastaafu..

Nyumba hiyo moja thamani yake si pesa za mbunge aliestaafu?Na wabunge wako wangapi?..

Kama tuko serious tuanze na kupunguza mishahara ya wabunge...na posho na kiinua mgongo...

Mtu akishakuwa Rais hata akistaafu anapata wageni mbalimbali wa wa kimataifa

Tuache kuwaza kimasikini kuwa nyumba ni sehemu Tu ya kulala...

Sioni tatizo kabisa Kwa wastaafu kupewa nyumba wala magari...

Hata makampuni huwa yanatoa bonuses Kwa ma CEO wao...hata kama mishahara ya watu wa chini midogo..

Urais ni ofisi hata ukisha staafu
Suala la mishahara na marupurupu ya wabunge inatisha ni wakati sasa wa kutazama upya.
 
Barua ya wazi kwa rais mstaafu Kikwete.

Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu

Nakuandikia barua hii mimi kama raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuonesha kukasirishwa, kutopendezewa na kitendo cha serikali yetu kukujengea Jumba kubwa utadhani Kasri la Wafalme na wewe bila haya au aibu unalipokea kwa bashasha bila kujali kuwa nchi hii bado ni masikini sana na bado ina uhitaji mkubwa sana wa kila senti kwenda kuondoa umasikini wa kutisha wa watu wetu.

Ninafahamu kuwa mlijitungia sheria kuwa mstaafu akistaafu basi apewe pakeji nono ikiwemo kujengewa nyumba, licha ya kwamba hukuwa rais wakati sheria hiyo inatungwa, lakini ulikuwemo serikalini wakati inatungwa, baadae ukawa rais na hukuirekebisha hiyo sheria!, Na wala hujawahi kusikika popote kuonyesha kutofurahishwa na Mzigo mzito wa sisi wananchi kuwagharamieni nyinyi wastaafu kupitia kodi zetu.

Ndugu Jakaya Rais mstaafu, hebu niambie, wewe kama mtu uliyefanya kazi kwenye chama na serikali toka mwaka 1975 hadi mwaka 2015 ina maana hadi ulipostaafu, yaani jumla ya miaka 40 hukujenga nyumba yoyote?, ina maana miaka yote hiyo ulikuwa unapanga? —ina maana uliacha kujenga nyumba ukitatrajia kuwa one day utakuwa raisi ili ukistaafu ujengewe nyumba kwa kodi za wananchi?

Ndugu Jakaya, Je nyumba yako ya Msoga haikutoshi? Unataka tena hilo hekalu ulipeleke wapi? Unataka umuachie urithi Ridhiwani?, umuachie urithi Miraji?, Umuachie urithi Mama Salma kupitia jasho la wananchi?

Nakuandikia barua hii nikitambua kuwa ulikuwa kijana wa TANU wewe, na nyie vijana wa kipindi hicho mlikuwa mkituaminisha kuwa mmeiva kwenye Itikadi za kukataa "unyonyaji",Najiuliza, kama mliweza kuwaaminisha wananchi kuwa siyo wanyonyaji na wakawaamini mpaka kuwapa nyadhifa kubwa huko mbeleni, mbona basi mnageuka wanyonyaji katika kustaafu kwenu?—Ina maana mikogo yenu ile ya kipindi hicho ya kujifanya siyo wapenda kujitajiriisha kwa kutumia kivuli cha nyadhifa zenu ilikuwa feki?. Mnapata wapi usingizi wa kuenjoy mimali yote hii katikati ya lindi zito la umasikini wa watu wenu tena kwa kujitajirisha kupitia jasho lao?

Ndugu Jakaya, mimi sitaki kukueleza umasikini wa nchi hii kwa sababu unaujua, Umeujua ukiwa bado kijana na unaujua ukiwa mzee—Hebu tutazame sisi wananchi walalahoi machoni, ambao masilahi yetu tunaambiwa hatuwezi kupata kwanza kwa sababu uchumi wa nchi umeshuka, kisha tuambie ndugu Jakaya, hilo hekalu lako ulilojengewa na serikali uliyopambana sana kuiweka madarakani linatusaidiaje sisi wananchi kuondoa adha za ukosefu wa maji, Ukosefu wa madawa, ukosefu wa madawati, upungufu wa ajira kwa vijana wetu, masilahi ya wakulima na wafanyakazi?

Ndugu Jakaya, wewe unalipwa asilimia 80 ya mshahara wa rais aliyeko madarakani, hivyo ndivyo nyie wanene mlivyojipangia, Unashindwaje kwa mshahara kujijengea nyumba nyingibe ukiihitaji mpaka serikali ikujengee Hekalu lote hilo kwa kodi za wananchi?

Najua unaweza kusingizia kuwa eti hivyo ndivyo sheria inavyotaka, lakini je kwani ungekataa kujengewa hilo hekalu ungelazimishwa?, Na kama ukilazimishwa kwani huwezi kulikataa?

Nakuandikia haya huku nikijua kuwa Rais Mkapa alijengewa Jumba lake, Mwinyi akajengewa Kasri lake na wewe leo umekabidhiwa Hekalu lako. Katika wote hao nimeamua nikuandikie wewe barua hii ya wazi kwa sababu Mzee Mkapa hatunaye, hawezi kujibu, Mzee Mwinyi ni mtu mzima sana, ni dhahiri anasukumiziwamo tu, Ila wewe bado una nguvu uko active na bila shaka unafuatilia kwa karibu sana yanayojiri nchi hii!

Kuna swali moja tu ningependa unijibu, JE TANU ILIWAFUNDISHA VIJANA WAKE MKIPATA MADARAKA AU KUSTAAFU MGEUKE WANYONYAJI?

Jakaya nakuomba kwa heshima na taadhima, wewe umeshiba, wenye njaa nchi hii ni wengi, wananchi wenye uhitaji wasioweza kumudu mahitaji yao ya msingi ni wengi, Hilo hekalu lako linaweza kujenga maelfu ya vyumba vya madarasa kusaidia watoto ambao wanafaulu darasa la saba lakini haweawezi kuendelea kutokana na upungufu wa madarasa nchini. Hilo hekalu lako ni zaidi ya Zahanati 50, Hilo hekalu lako ni zaidi ya madawati 5000.

Hebu niambie Jakaya mtu mwenye majumba, una familia yenye kipato kizuri, Unawezaje kukubali kuwa na Hekalu lote hilo kwa jasho la wananchi wenye uhitaji wa kila senti ya jasho lao?

Tafadhali rudisha hilo hekalu kwa wananchi liwasaidie, ukifanya hivyo utakuwa muungwana sana!
Mbona mwendazake hujamuandikia barua yoyote alipojijengea kiwanja cha ndege kwao chato?
 
Msilalamikie nyumba walizopewa kihalali na kisheria, lalamikieni majumba mengine wanayomiliki ambayo hayaendani na mishahara yao. Hizo nyumba wanazojengewa wakistaafu ni tone la maji baharini kwa utajiri wanaoupata madarakani.
 
KAWAULIZE WASUKUMA WENZIO UWANJA WA NDEGE WA CHATO HADI SASA UMETUMIA KIASI GANI?KWA TAKWIMU SAHIHI MILIONI 900,achilia mbali Majumba na Hifadhi ya wanyama n.k MBONA SUKUMA GANG MTAUMBUKA MWAKA HUU.HII NI AWAMU YA SITA,KAMA UMETUMWA NA ANAYEJIITA KIGOGO HUTOPATA KITU.KESHACHOKA.SINA ZAIDI ILI KUMTAKIA MH RAIS MSTAAFU KIKWETE MWENYEZI MUNGU AMLINDE NA HAWA WAPUUZI NA AMJAALIE MAISHA MAREFU NA BILA WOGA AENDELEE KUTUPA NASAHA ANAPOHITAJIKA.
 
Mzee chepe yeye kapewa jumba na gari ya kifahari ( Mercedes Benz ) juu ya bei mbaya maccm sio majitu hata aibu hayana
Screenshot_20210509-131828.png
 
Hata JK a atakuwa kuona haya... Hii ni kama vile dhuluma kwa walipa kodi... Ndiyo maana yeye hakufanya hivyo kwa watangulizi wake.

Kama kweli serikali inataka kuwatunza basi iwaweke kwenye nyumba za serikali mpaka Siku wao na Waja wao waondoke duniani. Yaani hizo nyumba ziwe ni mali ya serikali.
Eti wanajificha kwenye sheria,yaani wanatumia Sheria kujipendelea
 
Wote ni Wanyonyaji tu. Hivi Magufuli hakujiuliza kwa nini we zake hawakujengeana mpaka yeye akaamua kuwajengea wote.... Tatizo lilikuwa wapi?

Kikwete anadai ni haki yake, mbona sasa yeye hakumjengea Mkapa na Mwinyi mpaka wakasubiri Magufuli awajengee...!!

Kwa maoni yangu binafsi, huu ni muendelezo wa kujirundikia mali na matumizi mbaya ya pesa za wananchi.
JPM alifanya haya kama njia ya kuwafumba MDOMO wastaafu.
 
Back
Top Bottom