kimbendengu
JF-Expert Member
- Jun 7, 2013
- 8,394
- 16,128
Kikwete ni mlafi
HahahahaJamani plz msiweke picha ya hilo kasri, mie ntakufa kwa presha, [emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]
Sent from my Infinix X652C using JamiiForums mobile app
Aiseee! Kumbe Tanzania ni kubwa. How did you know, even, kwamba nina hivo vitu vyako!??
Kama huna unayo ile nyingine.Waache wafu wapumzike wameimaliza kazi Yao.Sio kila dk sijui angekuwa Fulani angepiga cm,Jana imepita na mambo yake uwezi irudisha mama anaendelea kwa ajili ya kesho ya Tanzania.Aiseee! Kumbe Tanzania ni kubwa. How did you know, even, kwamba nina hivo vitu vyako!???
Mtamuonea bure tu, Kikwete alijijengea nyumba yake kule msoga kijijini kwao na akahamia huko alipotoka State House.
Hii Sheria ilikuwepo Ila hakutaka kutumia pesa zenu Ila alipokuja Magufuli aliamua kutekeleza hiyo sheria kwa kuwajengea wastaafu wote nyumba kama stahikk ya kisheria kwa Marais wastaafu.
Hata mzee Mwinyi hakujijengea nyumba ambayo ni stahiki yake, alitumia fedha zake kujenga nyumba yake.
Magufuli ndio aliamua kuwajengea nyumba Marais wastaafu wote, sasa unaanzaje kumtaka Kikwete arudishe nyumba?
Lawama ziende kwa aliyeamua kuwajengea.
Kama huna unayo ile nyingine.Waache wafu wapumzike wameimaliza kazi Yao.Sio kila dk sijui angekuwa Fulani angepiga cm,Jana imepita na mambo yake uwezi irudisha mama anaendelea kwa ajili ya kesho ya Tanzania.
Hakulazimishwa kuipokea, angeweza kukataa kujengewa hiyo nyumba tena kwa maandishi na hoja za wazi kuwa haihitaji na serikali ingemsikiliza!Mtamuonea bure tu, Kikwete alijijengea nyumba yake kule msoga kijijini kwao na akahamia huko alipotoka State House.
Hii Sheria ilikuwepo Ila hakutaka kutumia pesa zenu Ila alipokuja Magufuli aliamua kutekeleza hiyo sheria kwa kuwajengea wastaafu wote nyumba kama stahikk ya kisheria kwa Marais wastaafu.
Hata mzee Mwinyi hakujijengea nyumba ambayo ni stahiki yake, alitumia fedha zake kujenga nyumba yake.
Magufuli ndio aliamua kuwajengea nyumba Marais wastaafu wote, sasa unaanzaje kumtaka Kikwete arudishe nyumba?
Lawama ziende kwa aliyeamua kuwajengea.
Basi kama yeye hakuifuta hata Magufuli angeweza kuifuta tu. Naona mmeamua tu kutafuta wa kumtupia maneno.Hakulazimishwa kuipokea, angeweza kukataa kujengewa hiyo nyumba tena kwa maandishi na hoja za wazi kuwa hakiitaji na serikali ingemsikiliza!
Lakini tunamlaumu kwa sababu sheria hiyo ilitungwa wakati wa Mkapa lakini yeye Kikwete wakati akiwa ni rais angeweza kuirekebisha au kuifuta lakini aliiacha tu.
Kitendo cha kuiacha maana yske kinatoa room kwa mstaafu yoyote in the future kuandiks barua serikali kuidai hata kama ana majumba 100
Magufuli hayuko hai, hatuwezi kumuandikia barua ya wazi akaisomaBasi kama yeye hakuifuta hata Magufuli angeweza kuifuta tu. Naona mmeamua tu kutafuta wa kumtupia maneno.
Lakini ndio alianzisha mchakato wa kujenga hizo nyumba na alishasema viongozi waliomtangulia waache kuwashwawashwa so ulitaka waanze kumuingilia kwenye masuala ya uongozi wake? Let's be honest kwenye hili hata wewe usingekataa maana unakataa kwa sababu zipi?Magufuli hayuko hai, hatuwezi kumuandikia barua ya wazi akaisoma
Kama ni muungwana alirudishe kwa umma, lipigwe mnada pesa zikasaidie kutatua kero za wananchi. Yeye ana mijumba mingi hana uhitaji huo wa kukamua wananchi kujengewa nyumba nyingineLakini ndio alianzisha mchakato wa kujenga hizo nyumba na alishasema viongozi waliomtangulia waache kuwashwawashwa so ulitaka waanze kumuingilia kwenye masuala ya uongozi wake? Let's be honest kwenye hili hata wewe usingekataa maana unakataa kwa sababu zipi?
Mwishowe angeonekana amesusa napo mngesema mwacheni bana , aliyepata kapata tu.
Jamani tusiwalaumu kwanza bali turekebishe sheria inayoruhusu wajengewe hizo nyumba ifutwe. Ukigombana na JK sasa utagombana na wangapi?Wote ni Wanyonyaji tu. Hivi Magufuli hakujiuliza kwa nini we zake hawakujengeana mpaka yeye akaamua kuwajengea wote.... Tatizo lilikuwa wapi?
Kikwete anadai ni haki yake, mbona sasa yeye hakumjengea Mkapa na Mwinyi mpaka wakasubiri Magufuli awajengee...!!
Kwa maoni yangu binafsi, huu ni muendelezo wa kujirundikia mali na matumizi mbaya ya pesa za wananchi.
Hapana Mambo mengine yanakuwa kama wivu binafsi, mwacheni, he served the nation na hiyo ni stahiki aliyoikuta hata hakupitisha yeye hiyo sheria. Aliyepaswa kujua haya no aliyemjengea.Kama ni muungwana alirudishe kwa umma, lipigwe mnada pesa zikasaidie kutatua kero za wananchi. Yeye ana mijumba mingi hana uhitaji huo wa kukamua wananchi kujengewa nyumba nyingine
Is too late kulalama sasa. Hizi sheria zingewza kubadilishwa Bungeni. Lakini wakati Wapinani hasa CGADEMA wwakilalamika kubanwa ns Spiika au wanamna alivyoiuba uchaguzi na sisi tuka kaa kimya haya ndiyo matokeo yake. Wako wapi akina Lissu, Lema, Mbowe watete hoja hii Bungeni? Wapi Zitto Kanwe na Mnyika
Barua ya wazi kwa rais mstaafu Kikwete.
Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu
Nakuandikia barua hii mimi kama raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuonesha kukasirishwa, kutopendezewa na kitendo cha serikali yetu kukujengea Jumba kubwa utadhani Kasri la Wafalme na wewe bila haya au aibu unalipokea kwa bashasha bila kujali kuwa nchi hii bado ni masikini sana na bado ina uhitaji mkubwa sana wa kila senti kwenda kuondoa umasikini wa kutisha wa watu wetu.
Ninafahamu kuwa mlijitungia sheria kuwa mstaafu akistaafu basi apewe pakeji nono ikiwemo kujengewa nyumba, licha ya kwamba hukuwa rais wakati sheria hiyo inatungwa, lakini ulikuwemo serikalini wakati inatungwa, baadae ukawa rais na hukuirekebisha hiyo sheria!, Na wala hujawahi kusikika popote kuonyesha kutofurahishwa na Mzigo mzito wa sisi wananchi kuwagharamieni nyinyi wastaafu kupitia kodi zetu.
Ndugu Jakaya Rais mstaafu, hebu niambie, wewe kama mtu uliyefanya kazi kwenye chama na serikali toka mwaka 1975 hadi mwaka 2015 ina maana hadi ulipostaafu, yaani jumla ya miaka 40 hukujenga nyumba yoyote?, ina maana miaka yote hiyo ulikuwa unapanga? —ina maana uliacha kujenga nyumba ukitatrajia kuwa one day utakuwa raisi ili ukistaafu ujengewe nyumba kwa kodi za wananchi?
Ndugu Jakaya, Je nyumba yako ya Msoga haikutoshi? Unataka tena hilo hekalu ulipeleke wapi? Unataka umuachie urithi Ridhiwani?, umuachie urithi Miraji?, Umuachie urithi Mama Salma kupitia jasho la wananchi?
Nakuandikia barua hii nikitambua kuwa ulikuwa kijana wa TANU wewe, na nyie vijana wa kipindi hicho mlikuwa mkituaminisha kuwa mmeiva kwenye Itikadi za kukataa "unyonyaji",Najiuliza, kama mliweza kuwaaminisha wananchi kuwa siyo wanyonyaji na wakawaamini mpaka kuwapa nyadhifa kubwa huko mbeleni, mbona basi mnageuka wanyonyaji katika kustaafu kwenu?—Ina maana mikogo yenu ile ya kipindi hicho ya kujifanya siyo wapenda kujitajiriisha kwa kutumia kivuli cha nyadhifa zenu ilikuwa feki?. Mnapata wapi usingizi wa kuenjoy mimali yote hii katikati ya lindi zito la umasikini wa watu wenu tena kwa kujitajirisha kupitia jasho lao?
Ndugu Jakaya, mimi sitaki kukueleza umasikini wa nchi hii kwa sababu unaujua, Umeujua ukiwa bado kijana na unaujua ukiwa mzee—Hebu tutazame sisi wananchi walalahoi machoni, ambao masilahi yetu tunaambiwa hatuwezi kupata kwanza kwa sababu uchumi wa nchi umeshuka, kisha tuambie ndugu Jakaya, hilo hekalu lako ulilojengewa na serikali uliyopambana sana kuiweka madarakani linatusaidiaje sisi wananchi kuondoa adha za ukosefu wa maji, Ukosefu wa madawa, ukosefu wa madawati, upungufu wa ajira kwa vijana wetu, masilahi ya wakulima na wafanyakazi?
Ndugu Jakaya, wewe unalipwa asilimia 80 ya mshahara wa rais aliyeko madarakani, hivyo ndivyo nyie wanene mlivyojipangia, Unashindwaje kwa mshahara kujijengea nyumba nyingibe ukiihitaji mpaka serikali ikujengee Hekalu lote hilo kwa kodi za wananchi?
Najua unaweza kusingizia kuwa eti hivyo ndivyo sheria inavyotaka, lakini je kwani ungekataa kujengewa hilo hekalu ungelazimishwa?, Na kama ukilazimishwa kwani huwezi kulikataa?
Nakuandikia haya huku nikijua kuwa Rais Mkapa alijengewa Jumba lake, Mwinyi akajengewa Kasri lake na wewe leo umekabidhiwa Hekalu lako. Katika wote hao nimeamua nikuandikie wewe barua hii ya wazi kwa sababu Mzee Mkapa hatunaye, hawezi kujibu, Mzee Mwinyi ni mtu mzima sana, ni dhahiri anasukumiziwamo tu, Ila wewe bado una nguvu uko active na bila shaka unafuatilia kwa karibu sana yanayojiri nchi hii!
Kuna swali moja tu ningependa unijibu, JE TANU ILIWAFUNDISHA VIJANA WAKE MKIPATA MADARAKA AU KUSTAAFU MGEUKE WANYONYAJI?
Jakaya nakuomba kwa heshima na taadhima, wewe umeshiba, wenye njaa nchi hii ni wengi, wananchi wenye uhitaji wasioweza kumudu mahitaji yao ya msingi ni wengi, Hilo hekalu lako linaweza kujenga maelfu ya vyumba vya madarasa kusaidia watoto ambao wanafaulu darasa la saba lakini haweawezi kuendelea kutokana na upungufu wa madarasa nchini. Hilo hekalu lako ni zaidi ya Zahanati 50, Hilo hekalu lako ni zaidi ya madawati 5000.
Hebu niambie Jakaya mtu mwenye majumba, una familia yenye kipato kizuri, Unawezaje kukubali kuwa na Hekalu lote hilo kwa jasho la wananchi wenye uhitaji wa kila senti ya jasho lao?
Tafadhali rudisha hilo hekalu kwa wananchi liwasaidie, ukifanya hivyo utakuwa muungwana sana!
Rais sio sehemu ya bunge ndio maana haingii bungeni ule muhimili mwingine hata akienda bungeni ni mpaka aalikwe na kifungu kitenguliwe kumruhusu kuingia, tuacheni na hayo sasa ulikuwa wapi kumwambia JPM wakati alipokuwa madarakani? Mambo ya mwinyi na Nyerere sote tunajuwa tulikuwa tunatoka katika Ujamaa kuja kwenye soko huria yalikuwa ni mambo yalazima na yaliishinishwa na CCM sio Mwinyi. Hizo ni chuki binafsi kwa JK hakutunga sheria hizo mlaumu aliyetunga. Wewe ungerudisha hiyo nyumbani? sisi unafiki na chuki ndio tumetawaliwa. Ogopa watu waliojificha nyuma ya udini na ujamaa hawa ni hatari sana.Rais ni sehemu moja ya bunge, kasome katiba vizuri
Pili kurekebisha makosa ya rais aliyepita siyo kuvunjia heshima.
Mwinyi aliunda tume ya Nyalali kupitia sheria zisizofaa, Nyalali akaja na sheria 40 ambazo zilikuwa hazifai na nyingine zilirungwa enzi za Nyerere. Mwinyi alizifuta baadhi yake nyingine alizirekebisha. Kyzifuta huko haimaanishi kuwa Mwinyi alimvunjia heshina Nyerere.
Kwa hiyo kama Kikwete angekuwa serious kuchukizwa na unyonyaji huu angeweza kufuta hicho kipengele cha kupeana mahekalu au angekiwekea condition kuwa incase mstaafu hana nyumba kabisa basi ajengewe AU angeweza kuirekebisha ikasema, serijali itajenga nyumba zake ambazo mstaafu yeyote atakayetaka ataishi mpaka kifo chake na mjane/mgane wake ataishi humo mpaka kifo chake lakini nyumba hiyo ni mali ya serikali!
Halafu watu huwa tunaaminishwa Mambo ya mtaani tu, imagine hakuna aliyeamini Nyerere mpaka anastaafu hakuwa na nyumba ya maana zaidi Ile ya matofali ya kuchoma kule kwao kijijini.Kama ni muungwana alirudishe kwa umma, lipigwe mnada pesa zikasaidie kutatua kero za wananchi. Yeye ana mijumba mingi hana uhitaji huo wa kukamua wananchi kujengewa nyumba nyingine