Mzee Jakaya Kikwete, rudisha hilo hekalu Serikalini lipigwe mnada pesa zisaidie wananchi

Mzee Jakaya Kikwete, rudisha hilo hekalu Serikalini lipigwe mnada pesa zisaidie wananchi

Angekataa

Au kama kweli ni muungwana alirudishe hilo hekalu lipigwe bei, pesa zikasaidie wananchi
Mbona mko kimya kwa Mkapa na Mwinyi? Wote walijengewa na mwendazake na walisha kabidhiwa. Mbona hamkusema kitu? Kikwete tu alikuwa bado hajakabidhiwa. Of course hata mimi mantiki ya kuwajengea hawa viongozi nymba sioni kabisa. |After all bado tunawagharia. Lakini kusema JMK peke yake arudishe si haki. Wale wa kwanza walipokea basi ikajenga precedence na yeye hawezi kukataa!!
 
Hata JK a atakuwa kuona haya... Hii ni kama vile dhuluma kwa walipa kodi... Ndiyo maana yeye hakufanya hivyo kwa watangulizi wake.

Kama kweli serikali inataka kuwatunza basi iwaweke kwenye nyumba za serikali mpaka Siku wao na Waja wao waondoke duniani. Yaani hizo nyumba ziwe ni mali ya serikali.
Exactly
 
Mbona mko kimya kwa Mkapa na Mwinyi? Wote walijengewa na mwendazake na walisha kabidhiwa. Mbona hamkusema kitu? Kikwete tu alikuwa bado hajakabidhiwa. Of course hata mimi mantiki ya kuwajengea hawa viongozi nymba sioni kabisa. |After all bado tunawagharia. Lakini kusema JMK peke yake arudishe si haki. Wale wa kwanza walipokea basi ikajenga precedence na yeye hawezi kukataa!!
Mkapa ni marehemu hawezi kusoma au kujibu hii barua ya wazi

Mwinyi ni mzee sana na hana kumbukumbu nzuri.

Ila Jakaya yupo, ana afya tele, kwa hiyo ujumbe huu na umfikie popote alipo nchini maana huwa namuona ana smartphone, hii inaonyesha kuwa huwa anaingia mitandaoni na atatusoma hapa!
 
Jamani plz msiweke picha ya hilo kasri, mie ntakufa kwa presha, [emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]

Sent from my Infinix X652C using JamiiForums mobile app
 
Civics haikukupita pembeni ndugu ndo maana huwezi kuwa na wivu sababu maarifa ya kutosha unayo kichwani ila elimu ikiwa haijakusaidia au ikikupta pembeni basi mambo ndo kama haya kuja na uzi wa kindezi kama huu
 
Rais ni sehemu moja ya bunge, kasome katiba vizuri

Pili kurekebisha makosa ya rais aliyepita siyo kuvunjia heshima.

Mwinyi aliunda tume ya Nyalali kupitia sheria zisizofaa, Nyalali akaja na sheria 40 ambazo zilikuwa hazifai na nyingine zilirungwa enzi za Nyerere. Mwinyi alizifuta baadhi yake nyingine alizirekebisha. Kyzifuta huko haimaanishi kuwa Mwinyi alimvunjia heshina Nyerere.

Kwa hiyo kama Kikwete angekuwa serious kuchukizwa na unyonyaji huu angeweza kufuta hicho kipengele cha kupeana mahekalu au angekiwekea condition kuwa incase mstaafu hana nyumba kabisa basi ajengewe AU angeweza kuirekebisha ikasema, serijali itajenga nyumba zake ambazo mstaafu yeyote atakayetaka ataishi mpaka kifo chake na mjane/mgane wake ataishi humo mpaka kifo chake lakini nyumba hiyo ni mali ya serikali!
sasa unamjudge mtu mmoja kwa uamuzi wa wengi wape we vipi bwana ..................................
 
Hatuna umasikini huo WA kushindwa kuwajengea Ma Rais wastaafu..

Nyumba hiyo moja thamani yake si pesa za mbunge aliestaafu?Na wabunge wako wangapi?..

Kama tuko serious tuanze na kupunguza mishahara ya wabunge...na posho na kiinua mgongo...

Mtu akishakuwa Rais hata akistaafu anapata wageni mbalimbali wa wa kimataifa

Tuache kuwaza kimasikini kuwa nyumba ni sehemu Tu ya kulala...

Sioni tatizo kabisa Kwa wastaafu kupewa nyumba wala magari...

Hata makampuni huwa yanatoa bonuses Kwa ma CEO wao...hata kama mishahara ya watu wa chini midogo..

Urais ni ofisi hata ukisha staafu
Depends on scenario Mkuu, sasa mfano JK Jumba lake lile la Msoga kweli Tena Umjengee Kasri lingine? Wastage of Funds.... Au Mzee mwinyi kupewa BENZ wakati tayari Ana VXR ni Misuse of Resource. Hivi ni lini Tutakomboka kifikra Watanzania?
 

Barua ya wazi kwa rais mstaafu Kikwete.

Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu

Nakuandikia barua hii mimi kama raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuonesha kukasirishwa, kutopendezewa na kitendo cha serikali yetu kukujengea Jumba kubwa utadhani Kasri la Wafalme na wewe bila haya au aibu unalipokea kwa bashasha bila kujali kuwa nchi hii bado ni masikini sana na bado ina uhitaji mkubwa sana wa kila senti kwenda kuondoa umasikini wa kutisha wa watu wetu.

Ninafahamu kuwa mlijitungia sheria kuwa mstaafu akistaafu basi apewe pakeji nono ikiwemo kujengewa nyumba, licha ya kwamba hukuwa rais wakati sheria hiyo inatungwa, lakini ulikuwemo serikalini wakati inatungwa, baadae ukawa rais na hukuirekebisha hiyo sheria!, Na wala hujawahi kusikika popote kuonyesha kutofurahishwa na Mzigo mzito wa sisi wananchi kuwagharamieni nyinyi wastaafu kupitia kodi zetu.

Ndugu Jakaya Rais mstaafu, hebu niambie, wewe kama mtu uliyefanya kazi kwenye chama na serikali toka mwaka 1975 hadi mwaka 2015 ina maana hadi ulipostaafu, yaani jumla ya miaka 40 hukujenga nyumba yoyote?, ina maana miaka yote hiyo ulikuwa unapanga? —ina maana uliacha kujenga nyumba ukitatrajia kuwa one day utakuwa raisi siku moja ili ukistaafu ujengewe nyumba kwa kodi za wananchi?

Ndugu Jakaya Je nyumba yako ya Msoga haikutoshi? Unataka tena hilo hekalu ulipeleke wapi? Unataka umuachie urithi Ridhiwani?, umuachie urithi Miraji?, Umuachie urithi Mama Salma kupitia jasho la wananchi?

Nakuandikia barua hii nikitambua kuwa ulikuwa kijana wa TANU wewe, na nyie vijana wa kipindi hicho mlikuwa mkituaminisha kuwa mmeiva kwenye Itikadi za kukataa "unyonyaji",Najiuliza, kama mliweza kuwaaminisha wananchi kuwa siyo wanyonyaji na wakawaamini mpaka kuwapa nyadhifa kubwa huko mbeleni, mbona basi mnageuka wanyonyaji katika kustaafu kwenu?—Ina maana mikogo yenu ile ya kipindi hicho ya kujifanya siyo wapenda kujitajiridhisha kwa kutumia kivuli cha nyadhifa zenu ilikuwa feki?. Mnapata wapi usingizi wa kuenjoy mimali yote hii katikati ya lindi zito la umasikini wa watu wenu tena kwa kujitajirisha kupitia jasho lao?

Ndugu Jakaya, mimi sitaki kukueleza umasikini wa nchi hii kwa sababu unaujua, Umeujua ukiwa bado kijana na uliujua ukiwa mzee—Hebu tutazame sisi wananchi walalahoi machoni, ambao masilahi yetu tunaambiwa hatuwezi kupata kwanza kwa sababu uchumi wa nchi umeshuka, tuambie Jakaya hilo Hekalu lako ulilojengewa na Serikali uliyopambana sana kuiweka madarakani linatusaidiaje sisi wananchi kuondoa adha za ukosefu wa maji, Ukosefu wa madawa, ukosefu wa madawati, upungufu wa ajira kwa vijana wetu, nasilahi ya wakulina na wafanyakazi?

Ndugu Jakaya, wewe unalipwa asilimia 80 ya mshahara wa rais aliyeko madarakani, hivyo ndivyo nyie wanene mlivyojipangia, Unashindwaje kwa mshahara kujijengea nyumba nyingibe ukiihitaji mpaka serikali ikujengee Hekalu lote hilo kwa kodi za wananchi?

Najua unaweza kusingizia kuwa eti hivyo ndivyo sheria inavyotaka, lakini je kwani ungekataa kujengewa hilo hekalu ungelazimishwa?, Na kama ukilazimishwa kwani huwezi kulikataa?

Nakuandikia haya huku nikijua kuwa Rais Mkapa alijengewa Jumba lake, Mwinyi akajengewa Kasri lake na wewe leo umekabidhiwa Hekalu lako. Katika wote hao nimeamua nikuandikie wewe barua hii ya wazi kwa sababu Mzee Mkapa hatunaye, hawezi kujibu, Mzee Mwinyi ni mtu mzima sana, ni dhahiri anasukumiziwamo tu, Ila wewe bado una nguvu uko active na bila shaka unafuatilia kwa karibu sana yanayojiri nchi hii!

Kuna swali moja tu ningependa unijibu, JE TANU ILIWAFUNDISHA VIJANA WAKE MKIPATA MADARAKA AU KUSTAAFU MGEUKE WANYONYAJI?

Jakaya nakuomba kwa heshima na taadhima, wewe umeshiba, wenye njaa nchi hii ni wengi, wananchi wenye uhitaji wasioweza kumudu mahitaji yao ya msingi ni wengi, Hilo hekalu lako linaweza kujenga maelfu ya vyumba vya madarasa kusaidia watoto ambao wanafaulu darasa la saba lakini haweawezi kuendelea kutokana na upungufu wa madarasa nchini. Hilo hekalu lako ni zaidi ya Zahanati 50, Hilo hekalu lako ni zaidi ya madawati 5000.

Hebu niambie Jakaya mtu mwenye majumba, una familia yenye kipato kizuri, Unawezaje kukubali kuwa na Hekalu lote hilo kwa jasho la wananchi wenye uhitaji wa kila senti ya jasho lao?

Tafadhali rudisha hilo hekalu kwa wananchi liwasaidie, ukifanya hivyo utakuwa muungwana sana!
Mfano wewe ndio ungekuwa Kikwete ungerudisha hio nyumba?
 
The problem tuu ni kwamba wanafanya mchana kweupe bila haya wala woga, they know hamwezi kufanya lolote. Mfano mechi ya jana. Ingekuwa JPM lazima papohapo angepiga simu laivu uwanjani na mechi ingechezwa saa kumi na moja kama ilivyopangwa. Huu ni ushamba na ulemavu wa akili uliokithiri.
Mkuu huo ubongo wako ufanyie factory reset.Mwache mzee wa watu apumzike.
 
Mfano wewe ndio ungekuwa Kikwete ungerudisha hio nyumba?


Ndio ustaarabu na uadilifu wenyewe huo. Kwa JK, hiyo nyumba kwake ni sawa na wewe upewe elfu 20,000 ambayo angepewa mhitaji hapo pembeni yako. Utimamu wa akili unakoforce uikatae ama ui-waive kwa mhusika ama mhitaji zaidi. Kupokea kwao, it means hawana utu, hawana uchungu na maumivu ya Watanzania, ni wabinafsi, wachumia matumbo, wanafiki, na watu wenye tamaa iliyochanganyika na uchoyo wa kuzimu. No words can rightly capture the level of such depravity.
 
Ndio ustaarabu na uadilifu wenyewe huo. Kwa JK, hiyo nyumba kwake ni sawa na wewe upewe elfu 20,000 ambayo angepewa mhitaji hapo pembeni yako. Utimamu wa akili unakoforce uikatae ama ui-waive kwa mhusika ama mhitaji zaidi. Kupokea kwao, it means hawana utu, hawana uchungu na maumivu ya Watanzania, ni wabinafsi, wachumia matumbo, wanafiki, na watu wenye tamaa iliyochanganyika na uchoyo wa kuzimu. No words can rightly capture the level of such depravity.
😟😟😟😜😜😜 but sindio asili ya watanzania karibia wote baada ya kizazi cha Nyerere
 
Depends on scenario Mkuu, sasa mfano JK Jumba lake lile la Msoga kweli Tena Umjengee Kasri lingine? Wastage of Funds.... Au Mzee mwinyi kupewa BENZ wakati tayari Ana VXR ni Misuse of Resource. Hivi ni lini Tutakomboka kifikra Watanzania?


Ugumu wa ukombozi wa fikra unakuja pale ambapo viongozi ndio mabomu kuliko raia wenyewe. Kuanza kubadili fikra zao, wakati ndio huamini kuwa bora kuliko raia ^akiliwise^ --- ni ngumu kuliko ugumu wenyewe.
 
😟😟😟😜😜😜 but sindio asili ya watanzania karibia wote baada ya kizazi cha Nyerere

Wapo waadilifu wengi sana, ila tu ni waoga kupindukia. Akitokea mzalendo mmoja aliye mstari wa mbele wa mapambano, utasikia wanasema ^Tuko pamoja^ ^Tuko nyuma yako^ The problem is, utasikia sauti yao tuu, wao hawaonekani asilani!!!
 
Back
Top Bottom