Mzee Jakaya Kikwete, rudisha hilo hekalu Serikalini lipigwe mnada pesa zisaidie wananchi

Mnaunga mkono viongozi wastaafu wenye kila kitu kujengewa Makasri na Mahekalu kwa faida ipi kwa wananchi masikini wa Tanzania wenye shida lukuki za msingi?
Usitupigie kelele bwana chunguza kuna mambo mangapi yakuwafaidisha hao maskini siyo nyumba za wastaafu waambie na mawaziri na wabunge wapunguzwe mishahara watembele vitz au ist mbona vitu vingine mtambue heshima na nafasi za watu siyo kubwabwaja tu Tasaf haifanyi kazi yake? hadi mjadili nyumba za wastaafu kwani bajeti hazisomwi huko bungeni msitufanye wote machizi kwa hoja zenu dhaifu na roho za kwanini
 
Watanzania sijui tumelogwa Mimi sielewi. Yaani badala ya kupambana ili kuondoa nfumo unaosababisha Yale tusiyoyataka tuko bize kupambana na tusiyoyataka. Hivi wewe ukipewa zawadi ya nyumba utaikataa kuonyesha uzalendo? Nani asiyetaka nyumba nzuri kama ile? Kama mazingira yanaruhusu were kupewa nyumba kwa nini ukatae?
 
Yaani huyu bibie mie simwelewi. Yaani anajitoa ufahamu kutoa Benz la Birthday 🎂 kuwa nchi ndo imemzawadia .ccm hapa mtajibu na naamini mtapata ile mnastahli
 
Usitupigie kelele bwana chunguza kuna mambo mangapi yakuwafaidisha hao maskini siyo nyumba za wastaafu waambie na mawaziri na wabunge wapunguzwe mishahara watembele vitz au ist mbona vitu vingine mtambue heshima na nafasi za watu siyo kubwabwaja tu Tasaf haifanyi kazi yake? hadi mjadili nyumba za wastaafu kwani bajeti hazisomwi huko bungeni msitufanye wote machizi kwa hoja zenu dhaifu na roho za kwanini
Safi sasa unakuja kwenye hoja ya msingi badala ya blahblah zako za awali.

Ni hivi tunaupinga ubadhirifu wa pesa za umma kwa nguvu zote including hayo uliyoyasema ila tu mada hii tuliyomo inahusu Hekalu la Jakaya.

Ukitaka mada za kulaani wabunge kupewa miposho minene minene zimo humu JF au unaweza kuandika nyingine maana Motto ya JF ni "Where We Dara Talk Openly"

Kama unampenda sana Jakaya kanywe naye chai, ila sisi tunamuomba kiungwana arududhe hilo hekalu serikalini lipigwe mnada pesa zikatatue matatizo ya wananchi.

Jakaya gana shida ya nyumba, anazo nyingi, Kuendelea kupokea Mihekalu kama hii kwa kisingizio cha sheria ni "Unyonyaji" na hiyo sheria ndo Mriha wenyewe walioutengeneza kutunyonya wananchi
 
Mnaunga mkono viongozi wastaafu wenye kila kitu including majumba kedekede kujengewa Makasri na Mahekalu ya mabilioni ya fedha kwa faida ipi kwa wananchi masikini wa Tanzania wenye shida lukuki za msingi?.
Uzalendo wenu uko wapi?
Hao viongozi walitoka mbinguni? si walichaguliwa na wananchi/ CCM nani anawachagua, sheria hizo katunga nani? sio bunge na wabunge waliochaguliwa. Ziko sheria mbaya zaidi kuliko haya hakuna viongozi wa juu kushtakiwa na wameongeza mpaka waziri mkuu na wabunge mbona watu kimyaa. Viongozi wakuu wa nchi kama marais wanalindwa kisheria maslahi yao. Hawa kama hawatunzwi wanauwezo wa kuiba zaidi ya hayo wakiwa madarakani. Kwa kuwa hajavunja sheria hakuna mwenye makosa. Manataka badilisheni sheria bungeni.
 
Tucdanganyane hata ww ukipewa hutoiwacha. Ila pia kuna umuhim w viongoz kufanya yale yalio n manufaa kw wananchi,co kizawadiana mimali tuu
 
Yaani huyu bibie mie simwelewi. Yaani anajitoa ufahamu kutoa Benz la Birthday 🎂 kuwa nchi ndo imemzawadia .ccm hapa mtajibu na naamini mtapata ile mnastahli
Mzee hawezi kuhimili urefu wa v8 mnataka aje aanguke muhoji tena hapa hawezi kubadilishiwa gari mpaka anaanguka kumbukeni wote wanaofanya hivyo vitu wana akili siyo mnakuja na vijudgement mlivyokaa navyo hapo kwenye nyumba zenu unajuaje kama iliulizwa au familia yake ikapendekeza hilo gari ili kumsaidia kumbukeni raisi mstaafu bado ana hadhi yake au mlitaka aende na crown kwenye hadhi za kitaifa vilevile hizo pesa ya mfukoni kabla sijajua uwezo wa mwanae hana pamoja na kwamba ni Raisi .....zile gari ni bei ghali kama Raisi alioana apewe kama pongezi tusiingize midomo kwenye fadhila za watu sanasana tuihoji TASAF na mpango wa pesa za serikali kusaidia wananchi walio maskini wengineo tusio kwenye mpango wa TASAF tufanye kazi kwa bidii tukatoe hoja huko bungeni siyo hapa kweye fake IDs
 
Hao viongozi walitoka mbinguni? si walichaguliwa na wananchi/ CCM nani anawachagua, sheria hizo katunga nani? sio bunge na wabunge waliochaguliwa. Ziko sheria mbaya zaidi kuliko haya hakuna viongozi wa juu kushtakiwa na wameongeza mpaka waziri mkuu na wabunge mbona watu kimyaa. Viongozi wakuu wa nchi kama marais wanalindwa kisheria maslahi yao. Hawa kama hawatunzwi wanauwezo wa kuiba zaidi ya hayo wakiwa madarakani. Kwa kuwa hajavunja sheria hakuna mwenye makosa. Manataka badilisheni sheria bungeni.
Rais ni sehemu ya bunge.

Miswada mingi huanzia kwenye baraza la mawaziri kabla ya kupelekwa bungeni.

Pia rais ndiye huweka saini muswada ili uwe sheria.

Kwa hiyo Marais husika hawawezi kukwepa lawama ya sheria mbovu kwa sababu ama ilianzia kwao kabla ya kwenda bungeni,, au waliisaini au Hawakuibadilisha pindi inapotakiwa kuibadilisha.

Jakaya mtu aliyekuwa rais ana zigo la lawama kwa kuvumilia sheria hii pindi akiwa rais, maana angeweza kupeleka muswada bungeni kuirekebisha lakini hakufanya, bila shaka alijua naye akistaafu atanufaika nayo!.

Na leo ananudaika na sheria hiyo ya kinyonyaji basi kama ni muungwana kweli arudishe hilo hekalu serikalini lipigwe mnada pesa zikasaidie wananchi!
 
Safi sasa unakuja kwenye hoja ya msingi badala ya blahblah zako za awali.

Ni hivi tunaupinga ubadhirifu wa pesa za umma kwa nguvu zote including hayo uliyoyasema ila tu mada hii tuliyomo inahusu Hekalu la Jakaya.

Ukitaka mada za kulaani wabunge kupewa miposho minene minene zimo humu JF au unaweza kuandika nyingine maana Motto ya JF ni "Where We Dara Talk Openly"

Kama unampenda sana Jakaya kanywe naye chai, ila sisi tunamuomba kiungwana arududhe hilo hekalu serikalini lipigwe mnada pesa zikatatue matatizo ya wananchi.

Jakaya gana shida ya nyumba, anazo nyingi, Kuendelea kupokea Mihekalu kama hii kwa kisingizio cha sheria ni "Unyonyaji" na hiyo sheria ndo Mriha wenyewe walioutengeneza kutunyonya wananchi
Rejea sentensi yangu kwamba Kuna hadhi za Viongozi na stahiki zao so hata kama ni hizo v8 za mawaziri japo ni hela nyingi wanastahili kutokana na shughuli zao na hadhi zao vilevile kwa nyumba za wastaafu .................kataa kubali
 
Barua ya wazi kwa rais mstaafu Kikwete.

Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu

Nakuandikia barua hii mimi kama raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuonesha kukasirishwa, kutopendezewa na kitendo cha serikali yetu kukujengea Jumba kubwa utadhani Kasri la Wafalme na wewe bila haya au aibu unalipokea kwa bashasha bila kujali kuwa nchi hii bado ni masikini sana na bado ina uhitaji mkubwa sana wa kila senti kwenda kuondoa umasikini wa kutisha wa watu wetu.

Ninafahamu kuwa mlijitungia sheria kuwa mstaafu akistaafu basi apewe pakeji nono ikiwemo kujengewa nyumba, licha ya kwamba hukuwa rais wakati sheria hiyo inatungwa, lakini ulikuwemo serikalini wakati inatungwa, baadae ukawa rais na hukuirekebisha hiyo sheria!, Na wala hujawahi kusikika popote kuonyesha kutofurahishwa na Mzigo mzito wa sisi wananchi kuwagharamieni nyinyi wastaafu kupitia kodi zetu.

Ndugu Jakaya Rais mstaafu, hebu niambie, wewe kama mtu uliyefanya kazi kwenye chama na serikali toka mwaka 1975 hadi mwaka 2015 ina maana hadi ulipostaafu, yaani jumla ya miaka 40 hukujenga nyumba yoyote?, ina maana miaka yote hiyo ulikuwa unapanga? —ina maana uliacha kujenga nyumba ukitatrajia kuwa one day utakuwa raisi siku moja ili ukistaafu ujengewe nyumba kwa kodi za wananchi?

Ndugu Jakaya Je nyumba yako ya Msoga haikutoshi? Unataka tena hilo hekalu ulipeleke wapi? Unataka umuachie urithi Ridhiwani?, umuachie urithi Miraji?, Umuachie urithi Mama Salma kupitia jasho la wananchi?

Nakuandikia barua hii nikitambua kuwa ulikuwa kijana wa TANU wewe, na nyie vijana wa kipindi hicho mlikuwa mkituaminisha kuwa mmeiva kwenye Itikadi za kukataa "unyonyaji",Najiuliza, kama mliweza kuwaaminisha wananchi kuwa siyo wanyonyaji na wakawaamini mpaka kuwapa nyadhifa kubwa huko mbeleni, mbona basi mnageuka wanyonyaji katika kustaafu kwenu?—Ina maana mikogo yenu ile ya kipindi hicho ya kujifanya siyo wapenda kujitajiridhisha kwa kutumia kivuli cha nyadhifa zenu ilikuwa feki?. Mnapata wapi usingizi wa kuenjoy mimali yote hii katikati ya lindi zito la umasikini wa watu wenu tena kwa kujitajirisha kupitia jasho lao?

Ndugu Jakaya, mimi sitaki kukueleza umasikini wa nchi hii kwa sababu unaujua, Umeujua ukiwa bado kijana na uliujua ukiwa mzee—Hebu tutazame sisi wananchi walalahoi machoni, ambao masilahi yetu tunaambiwa hatuwezi kupata kwanza kwa sababu uchumi wa nchi umeshuka, tuambie Jakaya hilo Hekalu lako ulilojengewa na Serikali uliyopambana sana kuiweka madarakani linatusaidiaje sisi wananchi kuondoa adha za ukosefu wa maji, Ukosefu wa madawa, ukosefu wa madawati, upungufu wa ajira kwa vijana wetu, nasilahi ya wakulina na wafanyakazi?

Ndugu Jakaya, wewe unalipwa asilimia 80 ya mshahara wa rais aliyeko madarakani, hivyo ndivyo nyie wanene mlivyojipangia, Unashindwaje kwa mshahara kujijengea nyumba nyingibe ukiihitaji mpaka serikali ikujengee Hekalu lote hilo kwa kodi za wananchi?

Najua unaweza kusingizia kuwa eti hivyo ndivyo sheria inavyotaka, lakini je kwani ungekataa kujengewa hilo hekalu ungelazimishwa?, Na kama ukilazimishwa kwani huwezi kulikataa?

Nakuandikia haya huku nikijua kuwa Rais Mkapa alijengewa Jumba lake, Mwinyi akajengewa Kasri lake na wewe leo umekabidhiwa Hekalu lako. Katika wote hao nimeamua nikuandikie wewe barua hii ya wazi kwa sababu Mzee Mkapa hatunaye, hawezi kujibu, Mzee Mwinyi ni mtu mzima sana, ni dhahiri anasukumiziwamo tu, Ila wewe bado una nguvu uko active na bila shaka unafuatilia kwa karibu sana yanayojiri nchi hii!

Kuna swali moja tu ningependa unijibu, JE TANU ILIWAFUNDISHA VIJANA WAKE MKIPATA MADARAKA AU KUSTAAFU MGEUKE WANYONYAJI?

Jakaya nakuomba kwa heshima na taadhima, wewe umeshiba, wenye njaa nchi hii ni wengi, wananchi wenye uhitaji wasioweza kumudu mahitaji yao ya msingi ni wengi, Hilo hekalu lako linaweza kujenga maelfu ya vyumba vya madarasa kusaidia watoto ambao wanafaulu darasa la saba lakini haweawezi kuendelea kutokana na upungufu wa madarasa nchini. Hilo hekalu lako ni zaidi ya Zahanati 50, Hilo hekalu lako ni zaidi ya madawati 5000.

Hebu niambie Jakaya mtu mwenye majumba, una familia yenye kipato kizuri, Unawezaje kukubali kuwa na Hekalu lote hilo kwa jasho la wananchi wenye uhitaji wa kila senti ya jasho lao?

Tafadhali rudisha hilo hekalu kwa wananchi liwasaidie, ukifanya hivyo utakuwa muungwana sana!
Ni wivu tu
 
Hii nchi ni ya kinyonyaji sana haina huruma na wananchi wake masikini, hekalu lote hilo unampelekea mtu aliyeshiba wakati kuna watanzania wanakufa kwa njaa, maradhi na ukosefu wa maji pia miundombinu duni, hii nchi kweli ina laana.

Barua ya wazi kwa rais mstaafu Kikwete.

Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu

Nakuandikia barua hii mimi kama raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuonesha kukasirishwa, kutopendezewa na kitendo cha serikali yetu kukujengea Jumba kubwa utadhani Kasri la Wafalme na wewe bila haya au aibu unalipokea kwa bashasha bila kujali kuwa nchi hii bado ni masikini sana na bado ina uhitaji mkubwa sana wa kila senti kwenda kuondoa umasikini wa kutisha wa watu wetu.

Ninafahamu kuwa mlijitungia sheria kuwa mstaafu akistaafu basi apewe pakeji nono ikiwemo kujengewa nyumba, licha ya kwamba hukuwa rais wakati sheria hiyo inatungwa, lakini ulikuwemo serikalini wakati inatungwa, baadae ukawa rais na hukuirekebisha hiyo sheria!, Na wala hujawahi kusikika popote kuonyesha kutofurahishwa na Mzigo mzito wa sisi wananchi kuwagharamieni nyinyi wastaafu kupitia kodi zetu.

Ndugu Jakaya Rais mstaafu, hebu niambie, wewe kama mtu uliyefanya kazi kwenye chama na serikali toka mwaka 1975 hadi mwaka 2015 ina maana hadi ulipostaafu, yaani jumla ya miaka 40 hukujenga nyumba yoyote?, ina maana miaka yote hiyo ulikuwa unapanga? —ina maana uliacha kujenga nyumba ukitatrajia kuwa one day utakuwa raisi siku moja ili ukistaafu ujengewe nyumba kwa kodi za wananchi?

Ndugu Jakaya Je nyumba yako ya Msoga haikutoshi? Unataka tena hilo hekalu ulipeleke wapi? Unataka umuachie urithi Ridhiwani?, umuachie urithi Miraji?, Umuachie urithi Mama Salma kupitia jasho la wananchi?

Nakuandikia barua hii nikitambua kuwa ulikuwa kijana wa TANU wewe, na nyie vijana wa kipindi hicho mlikuwa mkituaminisha kuwa mmeiva kwenye Itikadi za kukataa "unyonyaji",Najiuliza, kama mliweza kuwaaminisha wananchi kuwa siyo wanyonyaji na wakawaamini mpaka kuwapa nyadhifa kubwa huko mbeleni, mbona basi mnageuka wanyonyaji katika kustaafu kwenu?—Ina maana mikogo yenu ile ya kipindi hicho ya kujifanya siyo wapenda kujitajiridhisha kwa kutumia kivuli cha nyadhifa zenu ilikuwa feki?. Mnapata wapi usingizi wa kuenjoy mimali yote hii katikati ya lindi zito la umasikini wa watu wenu tena kwa kujitajirisha kupitia jasho lao?

Ndugu Jakaya, mimi sitaki kukueleza umasikini wa nchi hii kwa sababu unaujua, Umeujua ukiwa bado kijana na uliujua ukiwa mzee—Hebu tutazame sisi wananchi walalahoi machoni, ambao masilahi yetu tunaambiwa hatuwezi kupata kwanza kwa sababu uchumi wa nchi umeshuka, tuambie Jakaya hilo Hekalu lako ulilojengewa na Serikali uliyopambana sana kuiweka madarakani linatusaidiaje sisi wananchi kuondoa adha za ukosefu wa maji, Ukosefu wa madawa, ukosefu wa madawati, upungufu wa ajira kwa vijana wetu, nasilahi ya wakulina na wafanyakazi?

Ndugu Jakaya, wewe unalipwa asilimia 80 ya mshahara wa rais aliyeko madarakani, hivyo ndivyo nyie wanene mlivyojipangia, Unashindwaje kwa mshahara kujijengea nyumba nyingibe ukiihitaji mpaka serikali ikujengee Hekalu lote hilo kwa kodi za wananchi?

Najua unaweza kusingizia kuwa eti hivyo ndivyo sheria inavyotaka, lakini je kwani ungekataa kujengewa hilo hekalu ungelazimishwa?, Na kama ukilazimishwa kwani huwezi kulikataa?

Nakuandikia haya huku nikijua kuwa Rais Mkapa alijengewa Jumba lake, Mwinyi akajengewa Kasri lake na wewe leo umekabidhiwa Hekalu lako. Katika wote hao nimeamua nikuandikie wewe barua hii ya wazi kwa sababu Mzee Mkapa hatunaye, hawezi kujibu, Mzee Mwinyi ni mtu mzima sana, ni dhahiri anasukumiziwamo tu, Ila wewe bado una nguvu uko active na bila shaka unafuatilia kwa karibu sana yanayojiri nchi hii!

Kuna swali moja tu ningependa unijibu, JE TANU ILIWAFUNDISHA VIJANA WAKE MKIPATA MADARAKA AU KUSTAAFU MGEUKE WANYONYAJI?

Jakaya nakuomba kwa heshima na taadhima, wewe umeshiba, wenye njaa nchi hii ni wengi, wananchi wenye uhitaji wasioweza kumudu mahitaji yao ya msingi ni wengi, Hilo hekalu lako linaweza kujenga maelfu ya vyumba vya madarasa kusaidia watoto ambao wanafaulu darasa la saba lakini haweawezi kuendelea kutokana na upungufu wa madarasa nchini. Hilo hekalu lako ni zaidi ya Zahanati 50, Hilo hekalu lako ni zaidi ya madawati 5000.

Hebu niambie Jakaya mtu mwenye majumba, una familia yenye kipato kizuri, Unawezaje kukubali kuwa na Hekalu lote hilo kwa jasho la wananchi wenye uhitaji wa kila senti ya jasho lao?

Tafadhali rudisha hilo hekalu kwa wananchi liwasaidie, ukifanya hivyo utakuwa muungwana sana!
 
Rais ni sehemu ya bunge.

Miswada mingi huanzia kwenye baraza la mawaziri kabla ya kupelekwa bungeni.

Pia rais ndiye huweka saini muswada ili uwe sheria.

Kwa hiyo Marais husika hawawezi kukwepa lawama ya sheria mbovu kwa sababu ama ilianzia kwao kabla ya kwenda bungeni,, au waliisaini au Hawakuibadilisha pindi inapotakiwa kuibadilisha.

Jakaya mtu aliyekuwa rais ana zigo la lawama kwa kuvumilia sheria hii pindi akiwa rais, maana angeweza kupeleka muswada bungeni kuirekebisha lakini hakufanya, bila shaka alijua naye akistaafu atanufaika nayo!.

Na leo ananudaika na sheria hiyo ya kinyonyaji basi kama ni muungwana kweli arudishe hilo hekalu serikalini lipigwe mnada pesa zikasaidie wananchi!
Ni stahiki siyo kwamba hakusaini sijui nini na nini mnataka Raisi aishi kwenye Banda kama ana nyumba nyingi mwombe akupe moja siyo kuja kutupigia kelele na wewe tupe hata kati ya vingi ulivyonavyo au wewe huna chakutusaidia.............
 
Rejea sentensi yangu kwamba Kuna hadhi za Viongozi na stahiki zao so hata kama ni hizo v8 za mawaziri japo ni hela nyingi wanastahili kutokana na shughuli zao na hadhi zao vilevile kwa nyumba za wastaafu .................kataa kubali
Umeona tunahoji kila aina ya stahiki humu?

Tupo specific kwenye makasri na Mahekalu wakati hao watu wana majumba kedekede tayari na pia marupurupu yao mengine tunayowapa bado ni mengi tu na yanawatosha kujenga nyumba zao binafsi kwa idadi watakayotaka! .

Marekani ni nchi tajiri sana lakini rais wake akiondoka madarakani hajengewi nyumba, Sembuse sisi nchi masikini badala ya tutumie fedha kwa mambo ya msingi ya wananchi sisi tunazipeleks kwa watu waliokula wakashiba na kusaza!
 
Halafu inashangaza watu wanajifanya Malaika wakati matendo yao tu ikiwa wameshawahi saidia hata wasiojiweza hapo mtaani kwao wanasubiri serikali watu wasijengewe nyumba kisa maskini tena mwengine alikataa shule mwenyewe alikataa kulima mwenyewe yani watu wanataka wakae tuu hela ziwashukie kwenye vitanda juhudi za wengine wengine wafaidike tena Kikwete alivyopewa havimtoshi.............kwa mtizamo wangu
 
Rais sio sehemu ya bunge sio sawa, serikali inapeleka mswaada bungeni na wabunge wakipitisha ndio Rais anasign. Bunge lingekataa isingepita na wabunge ndio wawikilishi wa wananchi kwa maana wakipitisha wao ndio wananchi. Pili sheria alipeleka Mkapa sio JK na kawaida kubadili mambo kama haya ni kumvunjia heshima Rais aliyepita kama maboresho ni kuyafanya yawe bora tu sio kubadili sheria. Mbona JPM hakubadili hizi sheria? tuseme JK alikuwa mbaya JPM kwanini hakubadili mtu ambaye tunahubiri rais wa wanyonge. Ni yeye JPM alimkabidhi Mwinyi nyumba na ni yeye alianza mchakato wa kumjengea Kikwete. JK hakuanza ujenzi wakati yuko madarakani. JPM Rais wa wanyonge kwanini hakubadili hili alichobadili sehemu ya kuzika viongozi tu. JK hana kosa lolote na JPM anajengewa stahiki yake.
 
Rais ni sehemu moja ya bunge, kasome katiba vizuri

Pili kurekebisha makosa ya rais aliyepita siyo kuvunjia heshima.

Mwinyi aliunda tume ya Nyalali kupitia sheria zisizofaa, Nyalali akaja na sheria 40 ambazo zilikuwa hazifai na nyingine zilirungwa enzi za Nyerere. Mwinyi alizifuta baadhi yake nyingine alizirekebisha. Kyzifuta huko haimaanishi kuwa Mwinyi alimvunjia heshina Nyerere.

Kwa hiyo kama Kikwete angekuwa serious kuchukizwa na unyonyaji huu angeweza kufuta hicho kipengele cha kupeana mahekalu au angekiwekea condition kuwa incase mstaafu hana nyumba kabisa basi ajengewe AU angeweza kuirekebisha ikasema, serijali itajenga nyumba zake ambazo mstaafu yeyote atakayetaka ataishi mpaka kifo chake na mjane/mgane wake ataishi humo mpaka kifo chake lakini nyumba hiyo ni mali ya serikali!
 
[emoji3][emoji3][emoji3] Kama waliweza kushindwa kuacha ubunge wa mtwara wapi sijui huko kwa watanzania wengine nao wapate nafasi badala yake wakalundikana familia nzima bungeni kupiga hata hizo 12mil za ubunge wataweza kuacha Jumba lote Hilo la Bure Tena bila hata kutoa Jasho lolote, Never brother!
 
Back
Top Bottom