Mzee Jakaya Kikwete, rudisha hilo hekalu Serikalini lipigwe mnada pesa zisaidie wananchi

Mzee Jakaya Kikwete, rudisha hilo hekalu Serikalini lipigwe mnada pesa zisaidie wananchi


Barua ya wazi kwa rais mstaafu Kikwete.

Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu

Nakuandikia barua hii mimi kama raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuonesha kukasirishwa, kutopendezewa na kitendo cha serikali yetu kukujengea Jumba kubwa utadhani Kasri la Wafalme na wewe bila haya au aibu unalipokea kwa bashasha bila kujali kuwa nchi hii bado ni masikini sana na bado ina uhitaji mkubwa sana wa kila senti kwenda kuondoa umasikini wa kutisha wa watu wetu.

Ninafahamu kuwa mlijitungia sheria kuwa mstaafu akistaafu basi apewe pakeji nono ikiwemo kujengewa nyumba, licha ya kwamba hukuwa rais wakati sheria hiyo inatungwa, lakini ulikuwemo serikalini wakati inatungwa, baadae ukawa rais na hukuirekebisha hiyo sheria!, Na wala hujawahi kusikika popote kuonyesha kutofurahishwa na Mzigo mzito wa sisi wananchi kuwagharamieni nyinyi wastaafu kupitia kodi zetu.

Ndugu Jakaya Rais mstaafu, hebu niambie, wewe kama mtu uliyefanya kazi kwenye chama na serikali toka mwaka 1975 hadi mwaka 2015 ina maana hadi ulipostaafu, yaani jumla ya miaka 40 hukujenga nyumba yoyote?, ina maana miaka yote hiyo ulikuwa unapanga? —ina maana uliacha kujenga nyumba ukitatrajia kuwa one day utakuwa raisi siku moja ili ukistaafu ujengewe nyumba kwa kodi za wananchi?

Ndugu Jakaya Je nyumba yako ya Msoga haikutoshi? Unataka tena hilo hekalu ulipeleke wapi? Unataka umuachie urithi Ridhiwani?, umuachie urithi Miraji?, Umuachie urithi Mama Salma kupitia jasho la wananchi?

Nakuandikia barua hii nikitambua kuwa ulikuwa kijana wa TANU wewe, na nyie vijana wa kipindi hicho mlikuwa mkituaminisha kuwa mmeiva kwenye Itikadi za kukataa "unyonyaji",Najiuliza, kama mliweza kuwaaminisha wananchi kuwa siyo wanyonyaji na wakawaamini mpaka kuwapa nyadhifa kubwa huko mbeleni, mbona basi mnageuka wanyonyaji katika kustaafu kwenu?—Ina maana mikogo yenu ile ya kipindi hicho ya kujifanya siyo wapenda kujitajiridhisha kwa kutumia kivuli cha nyadhifa zenu ilikuwa feki?. Mnapata wapi usingizi wa kuenjoy mimali yote hii katikati ya lindi zito la umasikini wa watu wenu tena kwa kujitajirisha kupitia jasho lao?

Ndugu Jakaya, mimi sitaki kukueleza umasikini wa nchi hii kwa sababu unaujua, Umeujua ukiwa bado kijana na uliujua ukiwa mzee—Hebu tutazame sisi wananchi walalahoi machoni, ambao masilahi yetu tunaambiwa hatuwezi kupata kwanza kwa sababu uchumi wa nchi umeshuka, tuambie Jakaya hilo Hekalu lako ulilojengewa na Serikali uliyopambana sana kuiweka madarakani linatusaidiaje sisi wananchi kuondoa adha za ukosefu wa maji, Ukosefu wa madawa, ukosefu wa madawati, upungufu wa ajira kwa vijana wetu, nasilahi ya wakulina na wafanyakazi?

Ndugu Jakaya, wewe unalipwa asilimia 80 ya mshahara wa rais aliyeko madarakani, hivyo ndivyo nyie wanene mlivyojipangia, Unashindwaje kwa mshahara kujijengea nyumba nyingibe ukiihitaji mpaka serikali ikujengee Hekalu lote hilo kwa kodi za wananchi?

Najua unaweza kusingizia kuwa eti hivyo ndivyo sheria inavyotaka, lakini je kwani ungekataa kujengewa hilo hekalu ungelazimishwa?, Na kama ukilazimishwa kwani huwezi kulikataa?

Nakuandikia haya huku nikijua kuwa Rais Mkapa alijengewa Jumba lake, Mwinyi akajengewa Kasri lake na wewe leo umekabidhiwa Hekalu lako. Katika wote hao nimeamua nikuandikie wewe barua hii ya wazi kwa sababu Mzee Mkapa hatunaye, hawezi kujibu, Mzee Mwinyi ni mtu mzima sana, ni dhahiri anasukumiziwamo tu, Ila wewe bado una nguvu uko active na bila shaka unafuatilia kwa karibu sana yanayojiri nchi hii!

Kuna swali moja tu ningependa unijibu, JE TANU ILIWAFUNDISHA VIJANA WAKE MKIPATA MADARAKA AU KUSTAAFU MGEUKE WANYONYAJI?

Jakaya nakuomba kwa heshima na taadhima, wewe umeshiba, wenye njaa nchi hii ni wengi, wananchi wenye uhitaji wasioweza kumudu mahitaji yao ya msingi ni wengi, Hilo hekalu lako linaweza kujenga maelfu ya vyumba vya madarasa kusaidia watoto ambao wanafaulu darasa la saba lakini haweawezi kuendelea kutokana na upungufu wa madarasa nchini. Hilo hekalu lako ni zaidi ya Zahanati 50, Hilo hekalu lako ni zaidi ya madawati 5000.

Hebu niambie Jakaya mtu mwenye majumba, una familia yenye kipato kizuri, Unawezaje kukubali kuwa na Hekalu lote hilo kwa jasho la wananchi wenye uhitaji wa kila senti ya jasho lao?

Tafadhali rudisha hilo hekalu kwa wananchi liwasaidie, ukifanya hivyo utakuwa muungwana sana!
Acheni wivu wa kike.
 
Kwani Mkapa alipewa yuko kaburini? si alipewa hai mlikuwa wapi. Jiulize ingekuwa wewe umepewa stahiki yako ungeipiga mnada au kuikataa? Jiulize kwanza wewe, sisi ni rahisi kusema lakini hakuna hata mtanzania mmoja akataa stahiki yake na wengine hata kama sio stahiki yake atachukuwa. wangapi Tanzania hii watafanya unayoyataka wewe JK afanye.
Mkapa, Jakaya, Magufuli wote walizingua, Maana hiyo sheria ya Kujinufaisha pindi wakistaafu kila mmoja katika hao kashiriki kwa namna yake.

Mkapa ndiye aliyeitunga, huku Magufuli na Kikwete wakiwa ni sehemu ya serikali yake

Hakaya akairithi hiyo sheria lakini hakuifuta au kuirekebisha huenda ili na yeye akistaafu anyonye jasho la wananchi

Magufuli yeye akaitekeleza hiyo sheria kwa kuwajengea hao wastaafu Makasri wasiyohitaji

Sasa Nimemuandikia barua Kikwete kwa sababu, Yeye yuko hai na ana akili timamu, Mzee Mwinyi yeye ana ugonjwa wa kumbukumbu kwa hiyo huyu nimemuexclude maana huenda hata hajui ksma alipewa kasri anyway!

Mkapa na Magufuli ni marehemu, na wafu hawaandikiwi barua za wazi.

Kwa hiyo, Jakaya kama ni muungwana arudishe!
 
Kosa la Kikwete.

1. Kukubali kujengewa hiyo nyumba wakati hana uhitaji wa Nyumba, anayo majumba mengi tu tunayoyajua, bado anayo marupurupu mengi tu ambayo bado ananufaika kutokana na jasho letu wananchi ikiwemo kulipwa asilimia 80 ya mshahara wa rais aliyeko madarakani

2. Alipokuwa rais hajawahi kuifuta au kuirekebisha hiyo sheria.

3. Kuipokea nyumba ya Mabilioni ya fedha na kuifanya yake binafsi , huku akijua nchi hii ni masikini vya kutisha, hospitali zinapungukiwa dawa, watu wana shida ya maji, shule hazina madawati, hilo lijumba lingesaidia kupunguza adha hizo za wananchi.

Tunajua kuwa hata marais wenzie wastaafu walijengewa mikasri wakati hawana uhitaji nayo nayo ni makosa pia, ni unyonyaji
Hiyo nyumba ya kikwete ni 1.5Trillion za ASAD Hebu msitake turejee tusiyotaka kukumbuka hiyo nyumba ni zahanati ngapi na miradi mingapi ambayo utasema Tanzania itageuka leoleo iwe kitu gani sijui watu mna roho mbayaa Chato kuna benki ya hadhi ya nyota 5 na Hospitali hamuongei mnakuja kuongelea nyumba ya Fadhila ........................tena chato tunafahamu kabisa hayo majengo hayakustahili kuwepo huko ila kwasababu Mwendazake alikuwa mbabe sababu alishajua watu ni wajinga kiasi gani hawawezi kumhoji Kikwete kujifanya mpole na mwelewa ndo haya yanamkuta Dawa ya Mwafrika ni kumtishia na kumtesa watu wengine Ujinga na Wivu unawasumbua sana
 
Hiyo nyumba ya kikwete ni 1.5Trillion za ASAD Hebu msitake turejee tusiyotaka kukumbuka hiyo nyumba ni zahanati ngapi na miradi mingapi ambayo utasema Tanzania itageuka leoleo iwe kitu gani sijui watu mna roho mbayaa Chato kuna benki ya hadhi ya nyota 5 na Hospitali hamuongei mnakuja kuongelea nyumba ya Fadhila ........................tena chato tunafahamu kabisa hayo majengo hayakustahili kuwepo huko ila kwasababu Mwendazake alikuwa mbabe sababu alishajua watu ni wajinga kiasi gani hawawezi kumhoji Kikwete kujifanya mpole na mwelewa ndo haya yanamkuta Dawa ya Mwafrika ni kumtishia na kumtesa watu wengine Ujinga na Wivu unawasumbua sana
Ufisadi mmoja si uhalali wa ufisadi mwingine, hata kama ufisadi huo umehalalishwa na sheria!
 
Mzee JK kama utapitia huu uzi wala usiumize kichwa kuna binadamu tumeumbwa na roho mbaya na uhasidi tu ingekuwa yeye kapewa angepiga mnada? watu wanaongea kwa sababu hawajapata hiyo nafasi lakini hakuna mtu hata mmoja Tanzania hii apewe nyumba tena kisheria halafu aseme hapana naiuza mnada isaidie watu maskini. labda Mama Thereza. tuache roho mbaya na unafiki. Mzee haijaiba iba kapewa ni haki yake.
Nashangaa sana nchi limekuwa na miwatu yenye wivu daah mpaka unaweza waza kuwepo kwenye postal kodi ya 255 ni shida
 
Mkapa, Jakaya, Magufuli wote walizingua, Maana hiyo sheria ya Kujinufaisha pindi wakistaafu kila mmoja katika hao kashiriki kwa namna yake.

Mkapa ndiye aliyeitunga, huku Magufuli na Kikwete wakiwa ni sehemu ya serikali yake

Hakaya akairithi hiyo sheria lakini hakuifuta au kuirekebisha huenda ili na yeye akistaafu anyonye jasho la wananchi

Magufuli yeye akaitekeleza hiyo sheria kwa kuwajengea hao wastaafu Makasri wasiyohitaji

Sasa Nimemuandikia barua Kikwete kwa sababu, Yeye yuko hai na ana akili timamu, Mzee Mwinyi yeye ana ugonjwa wa kumbukumbu kwa hiyo huyu nimemuexclude maana huenda hata hajui ksma alipewa kasri anyway!

Mkapa na Magufuli ni marehemu, na wafu hawaandikiwi barua za wazi.

Kwa hiyo, Jakaya kama ni muungwana arudishe!
Sheria ilipita 1999 marekebisho 2005 kweli hukuyajuwa haya? Mambo yalipitishwa na wabunge yalijadiliwa na yakapita karibia miaka 15 leo ndio tunaamka? sheria ngapi zinapitishwa mbaya lakini zinapita. Wakulaumu ni wabunge na bunge lao, JK hana kosa lolote na swali langu nimeuliza ingekuwa wewe ungekataa haki yako kisheria au wewe ungeipiga mnada? na uongee ukweli wako. Hakuna binadamu wanamna hiyo Tz.
 
Mkapa ni marehemu, angekuwa hai huku ana afya njema naye tungemueleza.

Mzee Mwinyi sikumueleza ujumbe huu kwa sababu ana ugonjwa wa kusahau, huenda keshasahau kama hata naye alipewa kasri.

Halafu usilete habari za sijui roho ya korosho au kitu gani. Sisi tunamaindi kuona kodi zetu zinatumika Kiulafi

Hawa watu wana everything including hiyo mijumba, wanahitaji nini cha ziada zaidi ya kututwisha zigo sisi wananchi kugharamia mihekalu kama hiyo wakati tuna shida kibao za mambo ya msingi including upungufu wa madawati, dawa, shule, maji safi na salama etc!
Kwani Mwinyi kusahau ni nini mbele ya Hoja? Hata mtoto wake angepata huu ujumbe kama kweli ulitaget wastaafu kujengewa nyumba
 
Kwani Mwinyi kusahau ni nini mbele ya Hoja? Hata mtoto wake angepata huu ujumbe kama kweli ulitaget wastaafu kujengewa nyumba
Jumba ajengewe baba halafu barua umuandikie mtoto?
Sikumuinclude Mzee Mwinyi kwa sababu makhsusi. na sababu yenyewe ni kuwa yeye hana kumbukumbu vizuri kwa hiyo huenda hajui kama alipewa kasri!
 
Mwinyi anaweza kusoma, lakini kabla hajajibu anaweza kusahau niliuliza nini, kwa hiyo nimemwandikia Jakaya ujumbe mpana ufike kwa wastaafu wote waliohai, wale ambao wako madarakani kwa sasa na watakaofuata huko mbeleni.
Hukuweka kipande chochote kinachomhusu Mwinyi ili Kikwete afikishe ujumbe umeandika Uzi moja kwa moja kumlenga Kikwete bado hujajibu swali wewe ulishawahi rudisha vitu vingapi ulivyopewa kwa fadhila ili hali wengine wanavihitaji? hata chakula unachokula kuna wenye njaa wangependa uwapatie wewe utafute kingine je unafanyaga hivyo mara ngapi halafu watu wa hivi tukiwachunguzaga maisha yenu ni kama uandishi wenu huu wa roho mbaya
 
Jumba ajengewe baba halafu barua umuandikie mtoto?
Sikumuinclude Mzee Mwinyi kwa sababu makhsusi. na sababu yenyewe ni kuwa yeye hana kumbukumbu vizuri kwa hiyo huenda hajui kama alipewa kasri!
Hiyo Ripoti ya Daktari ya Mwinyi kusahau kiasi cha kutoweka ujumbe kimaandishi uliipima wewe? kwa level ya kusahau unayoongelea wewe asingeweza kuzindua Kitabu hiyo majuzi sababu hata kuongea angesahau, kubali tu una roho mbaaayaaa
 
Jpm alitaka kuongeza muda wa kukaa madarakani ndo akaona awajengee hayo majumba kuwafunga mdomo. Japo Ni kweli iyo sheria ipo lkn alipaswa kuangalia uchumi wa maskini huko vijijini. Kuliko kuwaongezea hao mabilionea nyumba.
Hapa mwenye roho mbaya atakaa kimya atajifanya haoni au haelewi chanzo...............vitu aliratibisha mwengine mje mmlaumu wengine yani mtu ukishakuwa na roho mbaya hata mada unayoleta unashindwa kuichunguza kwa kina unakurupuka nayo kumbe inakuja kumchafua mwengine
 
Wanyonge; aliye juu mngoje chini
Mabepari, mabwanyenye na makabaila; aliye juu mfuate hukohuko
Maisha ni kuchagua
Ushauri wa bure; Anza kujenga hekalu lako
 
Alitegemea na yy atajengewa kasri maskini. Ya Mungu mengi
Yaani na mijitu ilivyona roho mbaya haitasema na Jiwe isingethubutu kumsema sababu jiwe alijua mijitu ni midhaifu sana ukiitishia tu imefyata lakini Kikwete amejifanya kutuchukulia wote sawa na ubinadamu malipo yake ndo hayo mateke yani na yeye angekuwa katili tu kidogo heshima iwepo kucheka cheka sana na nyani ndo kuvuna hayo sasa
 
Sijaona tatizo kwa kiongoz yeyote kulaumiwa kwenye hili. Tatizo ni sisi wananchi mazwazwa kuchagua viongoz mazwazwa kwenda kutuwakilisha kizwazwa pale bungeni. Sheria zote za nchi hii zinaanzia bungeni. Na sheria ni msumeno. Leo mwananchi unalalamika wakati mbunge wa jimbo lako kazi ni kukonga makifi wakati sheria hiz kandamizi zinapopitishwa unategemea nn?... my take. Watanzania amkeni wapimeni viongoz kabla la kuwachagua. Kwani ndio chanzo cha haya maswahibu yote yanalolikumba taifa.
Hao viongozi wazuri utawapata wapi?Wote ni walewale na kila mmoja huonekana mzuri wakati wa kampeni.

Sent from my SM-C7000 using JamiiForums mobile app
 
Tatizo ndugu yangu kuna watu wanajifanya malaika hivi.
Mnaunga mkono viongozi wastaafu wenye kila kitu including majumba kedekede kujengewa Makasri na Mahekalu ya mabilioni ya fedha kwa faida ipi kwa wananchi masikini wa Tanzania wenye shida lukuki za msingi?.
Uzalendo wenu uko wapi?
 
Back
Top Bottom