Mzee Jakaya Kikwete, rudisha hilo hekalu Serikalini lipigwe mnada pesa zisaidie wananchi

Mzee Jakaya Kikwete, rudisha hilo hekalu Serikalini lipigwe mnada pesa zisaidie wananchi

Nadhani kwenye kutunga sheria unafahamu process vizuri

Process:
1. Muswada ni wa serikali au Mbunge
2. Kupitisha Muswada ni bunge
3. Kusaini Muswada ni Raisi

Kurekebisha Sheria:
1. Mapendekezo ya mabadiliko ni serikali au Mbunge
2. kupitisha Mabadiliko ni Bunge
3. Kusaini Mabadiliko ni Rais

Jakaya akiwa rais serikali yake haijawahi kupeleka muswada bungeni wa kubadili hiyo sheria ya Kujipa mahekalu.

Huwezi kushiriki kutunga sheria mbovu au kuibariki, kisha ukajificha kwenye sheria hiyohiyo kufanya Magumashi, halafu ukiulizwa kuhusu magumashi yako unaisingizia sheria kwa kusema aah, sheria ndivyo inavyotaka sasa nitafanyaje?

Tunachotaka ufanye ukatae matunda ya hiyo sheria ya dhulma kwa kupiga bei hilo hekalu pesa zikasaidie kutatua kero za wananchi!
Nakuuliza hivi, hiyo sheria ilivyopitishwa bungeni uliipinga?

Na sasa hivi umefanya nini kuibadilisha bungeni?

Kwa nini unamshambulia Jakaya kama vile Jakaya kasaini peke yake kujimilikisha hiyo nyumba bila mlolongo wa kupitisha sheria haujafuatwa?

Wakati mlolongo umefuatwa, bila kificho, wananchi wamejua, hawajapinga popote pale in significant numbers kupitishwa kwa sheria hiyo.

Ulitaka Jakaya akatae matakwa ya wawakilishi wa wananchi?
 
Nakuukiza hivi, hiyo sheria ilivyopitishwa bungeni uliipinga?

Na sasa hivi umefanya nini kuibadilishq bungeni?

Kwa nini unamshambulia Jakaya kama vile Jakaya kasaini peke yake kujimilikisha hiyo nyumba bila mlolongo wa kupitisha sheria haujafuatwa?

Wqkati mlolingo umefuatwa, bila kificho, wananchi wamejua, hawajapinga popote pale in significant numbers kupitishwa kwa sheria hiyo.

Ulitaka Jakaya akatae matakwa ya wawakilishi wa wananchi?
Hakuna time limit ya kupinga sheria za kidhalimu na matokeo ya sheria hizo.

Context ya wakati ambapo tumeona enforcement ya sheria hiyo waliyojitungia wenyewe ikijitokeza hivi karibuni, imepelekea kuraise alarm kubwa kwetu na kwa muktadha huo imetulazimu tuwaeleze ukweli beneficiary wa sheria hizo kuwa wanachofanya ni unyonyaji uliowezeshwa kisheria. Hawana excuse ya kujificha kwenye kivuli cha sheria kwa sababu pamoja na uwepo wa Sheria hiyo bado wangeweza kukataa benefits hizo za kinyonyaji.Kwa sababu kimsingi hiyo sheria inasema lazima mtu aipokee hiyo nyumba!.

Ufortunately beneficiaries waliohai ni wawili, huko juu nimeeleza why nimemuandikia barua hii ya wazi Jakaya na siyo mzee Mwinyi!

So, sijamshambulia Jakaya, bali nimemtaka aliachie hilo hekalu lipigwe mnada pesa zikasaidie wananchi. Jakaya ana mijumba mingine, ni unyonyaji kukubali hili jingine
 
Sheria ilikuwepo lakini marais wote waliona Haya kuitekeleza, akaja Jiwe mwenye PhD ya unafiki akawajengea wote Kwa mpigo. Lawama ni Kwa Jiwe sio JK
Kumbe jiwe rais wa wanyonge ndiyo ametekeleza haya? Vipi nyerere inamaana hakujengewa?
 
Kumbe jiwe rais wa wanyonge ndiyo ametekeleza haya? Vipi nyerere inamaana hakujengewa?
Nyerere alijengewa kama Zawadi, haikuwa lazima ajengewe, na haikuwa sheria ajengewe! . Ila hawa wengine waliofuata wakaigeuza hiyo act kuwa ni stahiki yao ya msingi hata kama wana mijumba mingi yao binafsi!
 
Ila na wewe mtoa mada Kama hiyo Sheria ilivyotungwa hukuona Kama tatizo, alipokabidhiwa jumba mwinyi na mkapa bado hukuona Kama ni tatizo, hukutoa neno kwa mtekelezaji yaani jpm basi una chuki na jk au una lako Jambo,
 
Hakuna time limit ya kukemea jambo lisilofaa
 
Nyerere alijengewa kama Zawadi, haikuwa lazima ajengewe, na haikuwa sheria ajengewe! . Ila hawa wengine waliofuata wakaigeuza hiyo act kuwa ni stahiki yao ya msingi hata kama wana mijumba mingi yao binafsi!
Hiyo Sheria ilipitishwa mwaka gani? Ila Kama wengine wamejengewa basi hakuna namna, maana kumtaka jk asipokee wakati wengine wanazo inaonekana una lako Jambo na jk
 
Hiyo Sheria ilipitishwa mwaka gani? Ila Kama wengine wamejengewa basi hakuna namna, maana kumtaka jk asipokee wakati wengine wanazo inaonekana una lako Jambo na jk
Wengine waliojengewa kwa mujibu wa hiyo sheria ni Mkapa na Mwinyi.

Nyerere hakujengewa Nyumba kwa mujibu wa sheria hii, yeye alipewa zawadi na JWTZ

Mkapa ni marehemu, huwezi kumuandikia marehemu barua ya wazi

Mzee Mwinyi ana ugonjwa wa kusahau, ni useless kumuandikia mtu wa hivyo warwka kama huo

Aliyebaki ni huyu Jakaya, huyo ni muafaka kabisa kumuandikia barua hii
 
Watu mnaichukulia poa nafasi ya Urais hebu nendeni Nigeria muone vitu x-presidents walivyopewa ikiwemo presidential libraries! Au nendeni hapo kenya! Uhuru anajengewa jumba Narok county!
 
Ila na wewe mtoa mada Kama hiyo Sheria ilivyotungwa hukuona Kama tatizo, alipokabidhiwa jumba mwinyi na mkapa bado hukuona Kama ni tatizo, hukutoa neno kwa mtekelezaji yaani jpm basi una chuki na jk au una lako Jambo,
Ndio tatizo la watanzania huwa tuna zile siasa za msimu. Hili suala likipoa mleta mada atasahau kuwa alishaanzisha wazo lake jamii forum.

Tunakuja kulalamika lakini wakati sheria zikitungwa wawakilishi wetu ni kama hatuna mawasiliano nao.
 
Mkapa ni marehemu hawezi kusoma au kujibu hii barua ya wazi

Mwinyi ni mzee sana na hana kumbukumbu nzuri.

Ila Jakaya yupo, ana afya tele, kwa hiyo ujumbe huu na umfikie popote alipo nchini maana huwa namuona ana smartphone, hii inaonyesha kuwa huwa anaingia mitandaoni na atatusoma hapa!
Ha ha ha! Unamuonea. Mbona ulikuwa kimya mkapa alipokuwa hai? Unatakiwa unbalance. Mwinyi unamsamehe kwa vile Mzee. Kikwete anakaribia 70. No Kijana kumbe. Uzee unaanzia miaka mingapi?
 
Mwalimu akifufuka hapa anaweza kupata mshtuko na kufa tena.......hivi hawa watu ndo wamekulia kwenye itikadi za mwalimu kweli? wazee wa kujivinjari na marcedes benz na mahekalu huku mtanzania akiendelea kuogelea kwenye lindi la ufukara..
 
Nimewahi kusikia bwana mmoja akishukuru baba yake kufa ghafla.
Bwana yule amesema bora baba amefariki haraka maana angejua kama atakufa hivi karibuni angetuachia mikakati kibao
Hivyo kifo ni fursa kwa wengine
 
Si Magufuli ndio alimjengea
JPM alikuwa akitekeleza Sharma waliyojiwekea watangulizi wake kuwapima karma walikuwa serious kuzipokea Healy hizo, hii bagosha! Akashangaa wakazipokea! And wanaendelea kuzipokea Bilal haye!
 
Hata JK a atakuwa kuona haya... Hii ni kama vile dhuluma kwa walipa kodi... Ndiyo maana yeye hakufanya hivyo kwa watangulizi wake.

Kama kweli serikali inataka kuwatunza basi iwaweke kwenye nyumba za serikali mpaka Siku wao na Waja wao waondoke duniani. Yaani hizo nyumba ziwe ni mali ya serikali.
JK hakuona haya Bali alikuwa goigoi kutekeleza mipango ya maendeleo na sharia, kwani alikuwa busy angani kuzunguka Dunia! JPM ngosha ni bingwa wa kutekeleza mipango yote ya maendeleo na ni msomi mzuri na mfuatiliaji wa mambo na hivyo kuyaibua hata yaliyozikwa!
Kama JK angekuwa na haya hakika angeikataa hiyo nyumba!
 
Back
Top Bottom