Mzee Jakaya Kikwete, rudisha hilo hekalu Serikalini lipigwe mnada pesa zisaidie wananchi

Hkn kitu km hicho eti ufanye makosa mtu akutetee!! Huo ni uongo na majungu ya kiswahili!!

Watu wakiwa na ghadhabu wanakushusha mzima mzima na hkn wa kuwazuia
Al bashir yuko wapi leo??
Mtoto wa Hisene habre analia na moto weeee!!!

Watu wakikukataa wamekataa tu.

Wewe unatamka km wewe ukimgusa kikwete wafwa.....Anakubalika...Gwajima yuko wapi,? Ameshuka ziiiii!!! Hapo ni
Baada ya kumsema kikwete!!

Bora asingeenda kujianika huko!! Ataporomoka!!! nzi ana afadhali!!
 
Alitekeleza sheria kama ambavyo wabunge ukigusia zile posho zao wanajibu kuwa zipo kwa mujibu wa sheria, kwahiyo tatizo ni sheria.
 
Hao wageni wa kimataifa hawajui nchi yetu ni masikini? Kwa hiyo wewe ukitembelewa na mgeni uko tayari kukopa umchinjie ng'ombe akuone u tajiri huku familia yako haina uwezo ? Yaani unafurahia 'show off' kwa wageni badala ya furaha kwa wananchi? Lengo la KIKWETE kuomba urais ilikuwa kuwa mtumishi wa wananchi ama mzigo kwao? Na elimu yote aliyonayo anashindwa kuona mzigo wa ufukara waliobebeshwa na serikali kugharamia anasa za viongozi walioko madarakani na waliostaafu! Kweli uhuru wetu ulikuwa kubadilisha rangi za wakoloni tu.
 
Hujajibu swali nililokuuliza na ulilojibu sijakuuliza.

Mbunge wako anayeweza kupeleka hoja ya kubadili sheria bungeni umemuandikia?
Mbunge wangu yupi katika hawa walioingia bungeni kimagumashi?
Yaani kesi ya Ngedere nitafute wakili nyani? —You are not serious
 
Lakini c mlipewa magufuli mkamtukana? Wacha mama agawe tu mali za serikali na matajiri wenzie, sie akina kajamba nani tulie na kusaga meno
 
Mbunge wangu yupi katika hawa walioingia bungeni kimagumashi?
Yaani kesi ya Ngedere nitafute wakili nyani? —You are not serious
Hahaaa,

Watanzania wengi ni mahodari w kupiga kelele JF lakini kubadili mambo ya msingi hawataki.

Sasa hao wabunge magumashi umeavhiaje wakaingia bungeni?

Na kama wewe umeachia wbunge magumashi waingie bungeni, wewe huna lawama kuchia wabunge magumashi waingie bungeni kupitisha miswada magumashi?

Kwa nini na wewe usiwe sehemu ya watu walioruhusu magumashi Tanzania?
 
Nilitumia haki yangu ya kupiga kura, lakini yaliyotokea baada ya hapo ni ya kisikitisha ni ujambazi kwenda mbele. Sasa nashangaa unataka nimtume jambazi kwenye kikao cha majambazi kwenda kuomesha ujambazi. It foesn't work
 
Nilitumia haki yangu ya kupiga kura, lakini yaliyotokea baada ya hapo ni ya kisikitisha ni ujambazi kwenda mbele. Sasa nashangaa unataka nimtume jambazi kwenye kikao cha majambazi kwenda kuomesha ujambazi. It foesn't work
Umeshindwa kuzuia ujambazi wa kumfanya jambazi kuwa mbunge, una tatizo kubwa kuliko Kikwete kukurudishia jumba hilo.

Kwa sababu hata Kikwete akikurudishia jumba hilo, huna uhakika kwamba hatapewa jingine kubwa kuliko hilo, kisheria.

Jipange kubadilisha sheria, sio kuleta mngonjera JF na kuleta threads za uanaharakati wa kick.

Kikwete mwenyewe aliposakamwa na kusikia alishasema "ni upepo tu, utapita".

Sasa wewe ambaye unaleta uanaharakati wa JF hatujui hata kama kakusikia unategemea arudishe jumba kweli au unamaliza hasira zako tu hapa JF?
 
Ndugu yangu nimekuelewa vizuri.Hapa kuna sheria ambazo zimegawanyika katika makundi mawili makubwa.Zipo zenye hasara na kuumiza na zipo zenye hasara "laini".Hasara inayoumiza ni kama hii ya kinga kwa watu kama Ndugai na wengine,sheria za uhujumu uchumi,sheria za mitandao,n.k.Hii inawapelekea kufanya watakavyo bila kujali madhara yake na huku wakiitegemea kinga hiyo.Lakini kuna hizi sheria zenye hasara "laini" ambazo katika maisha ni vitu vya kawaida.Jakaya kupewa kasri ni suala tu la sehemu na thamani ya eneo (valuation basis).Kajengewa nyumba Masaki au Mikocheni.Mchanga ni huu huu na hautoki Ujerumani,Cement ni ileile ya Wazo Hill au dangote,Nondo ni hizi hizi ,kokoto ni zile zile za kunduchi,mafundi ni wale wale,Matofali ni yale yale na ya ardhi hii hii ya Tanzania.Tofauti iliopo ni sehemu gani na pana hadhi gani,basi.Kasri hilo hilo likijengwa Vingunguti au Chanika impact yake itakuwa ndogo sana kuliko Masaki.

 
Lakini c mlipewa magufuli mkamtukana? Wacha mama agawe tu mali za serikali na matajiri wenzie, sie akina kajamba nani tulie na kusaga meno
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] mother Theresa anadai yeye ni mwenye huruma sana.

Sent from my Infinix X652C using JamiiForums mobile app
 
Sheria ilikuwepo lakini marais wote waliona Haya kuitekeleza, akaja Jiwe mwenye PhD ya unafiki akawajengea wote Kwa mpigo. Lawama ni Kwa Jiwe sio JK
Sawa, lakini haramu ni haramu tu hata iweje!
 
Najua Magu alifanya hivyo maksudi, ili kuwapumbaza wenzake kwa aliyokuwa anafanya Chato.
 
Basi wajengewe ofisi na sio Mahekalu ya gharama kubwa. Maana ofisi km ofisi gharama yake ni around mil.20 au 30 sio hayo Mahekalu yenye thamani ya bil.1.5 +
 
Huna lolote wivu tu na roho mbaya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…