Missile of the Nation huwa napenda sana 'Hoja' zako japo kuna muda Mimi na Wewe huwa 'tunazinguana' hapa Jamvini ( Jukwaani )
Umeadika na Kuelezea vizuri sana ila nakulaumu sehemu Moja tu kwamba kama umeshakiri ni Sheria waliojitungia wenyewe ni kwanini Wewe Lawama ( Ngendembwe ) zako umeamua Kuzielekeza tu Kwake Rais Mstaafu Kikwete?
Halafu uliponichanganya zaidi ni pale uliposema kuwa huwezi Kumsema Mkapa kwakuwa sasa ni Hayati. Kwani Sheria hii imepitishwa baada ya Kufariki Rais Mstaafu Mkapa? Kwanini nae hukumsema Kipindi kile akiwa Hai? au Mtandao wa JamiiForums haukuwepo ili umuandikie hivi na bahati nzuri hata Yeye Mwenyewe ( Hayati Rais Mkapa ) alikuwa ni Mdau ( Member ) Mwenzetu JamiiForums?
Na uliponichanganya zaidi ni uliposema kuwa huwezi kumpa 'Makavu' yake Rais Mstaafu Mwinyi kwakuwa ni Mzee sasa na haelewi chochote.
Hivi Rais Mstaafu Mwinyi angekuwa ni Mzee na haelewi chochote kile angeandika Kitabu chake? Je, angekuwa anasafiri na hata Kuhutubia katika Hafla mbalimbali za Serikali? Je, angeweza kupokea Zawadi ya Gari jipya aina ya Benz huku akitaka Kuliendesha ( Kupiga Misele nalo ) pale pale JNICC na akifurahi kuliko Maelezo huku akimkumbatia Mkewe Mama Sitti?
Binafsi GENTAMYCINE sijawahi Kumkubali Rais Mstaafu Kikwete ( kutokana na sababu zangu Kuu Tatu tu ambazo Kimaadili sitoziweka hapa ) ila kwa hili la Kumsiliba ( Kumsema ) Yeye tu sana hivi na Kuwaacha wengine naona unamuonea na huenda tu ama ukawa una lako au una Chuki nae Binafsi na kwa hao Watoto wake akina Ridhiwani na Miraji.
Ukiondoa ( Ukiacha ) Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere ambaye nina uhakika nae kwakuwa namjua ndani nje kutokana na Ukaribu Wetu wa Kiukabila ( Uzanaki ) na hata 'Undugu' wa Kiukoo Nyumba alizonazo ni Mbili tu ya Msasani na ya Kijijini Butiama ile ya Magomeni siihesabii kwakuwa ilikuwa nadhani ni ya Chama au Serikali Kipindi hicho anaipambania nchi.
Ila kwa waliofuatia Rais Mstaafu Mzee Mwinyi Nyumba zake ninazozijua anazo kabla hajajengewa yake na Serikali ni 5, Hayati Rais Mkapa ninazozijua kabla nae hajajengewa yake na Serikali ni 6 na za Rais Mstaafu Kikwete nae ninazozijua anazo kabla hajajengewa yake na Serikali ni 10 sina uhakika sana kwa Hayati Rais Dkt. Magufuli japo nimedokezwa Yeye ndiye anaweza akaongoza kuwa na Nyumba nyingi ( japokuwa ameongoza ) kwa miaka yake Sita ( 6 ) tu.
Na hapa wa Kuwalaumu zaidi ni Wabunge wetu ambao ndiyo waliipitisha Sheria hii na siyo hawa Marais. Tuna Wabunge ambao miaka yote tu wanawekwa 'Mifukoni' mwa Watawala ( Marais ) japo na Wao ni 'Mhimili' Mkuu na unaojitegemea. Bunge la Tanzania limejaa Wabunge Wanafiki, Waoga na Watu wa 'Kujikomba' tu kwa 'State' na tatizo Kubwa la Mifumo mingi ya 'Kiutawala' nchini Tanzania huwa inaanzia huko ( hapo ) Bungeni.