Mzee Jakaya Kikwete, rudisha hilo hekalu Serikalini lipigwe mnada pesa zisaidie wananchi

Mzee Jakaya Kikwete, rudisha hilo hekalu Serikalini lipigwe mnada pesa zisaidie wananchi

wabunge na raisi huwa wanalindana kimaslahi. unakuta wabunge wanapisha sheria ya kujiongezea posho raisi anapitisha huku akijua wazi kesho itakuwa rahisi wabunge kupitisha sheria ya kumlinda raisi
Wanapewa milioni kumi kupitisha hoja zenye haraka
 
Sheria ilikuwepo lakini marais wote waliona Haya kuitekeleza, akaja Jiwe mwenye PhD ya unafiki akawajengea wote Kwa mpigo. Lawama ni Kwa Jiwe sio JK
... nchi iliachana na umaskini (uchumi wa kati) kipindi cha Magufuli so ilikuwa sahihi yeye (na sio watangulizi wake) kuwajengea majumba marais wastaafu! Ni katika kipindi cha Magufuli tumehakikishiwa nchi hii ni tajiri mno!
 
Sheria ilikuwepo lakini marais wote waliona Haya kuitekeleza, akaja Jiwe mwenye PhD ya unafiki akawajengea wote Kwa mpigo. Lawama ni Kwa Jiwe sio JK
Sikiliza wewe tahira!

Sheria mbovu inafutwa siyo kuonewa aibu!

Kwa hiyo hao watangulizi wa jiwe walipaswa kuifuta siyo kuionea aibu.
 
The problem tuu ni kwamba wanafanya mchana kweupe bila haya wala woga, they know hamwezi kufanya lolote. Mfano mechi ya jana. Ingekuwa JPM lazima papohapo angepiga simu laivu uwanjani na mechi ingechezwa saa kumi na moja kama ilivyopangwa. Huu ni ushamba na ulemavu wa akili uliokithiri.
Acha ujinga wako
Hizo nyumba jiwe ndiyo aliwajengea wote

Alijua na yeye atajenga zaid ya hekalu
Ili mkilalamika anawaambia mbona JK BM wote nimewajengea?
 
... nchi iliachana na umaskini (uchumi wa kati) kipindi cha Magufuli so ilikuwa sahihi yeye (na sio watangulizi wake) kuwajengea majumba marais wastaafu! Ni katika kipindi cha Magufuli tumehakikishiwa nchi hii ni tajiri mno!
Na wewe ulitembea kifua mbere!
 
alisikika mlevi mmoja akisema "umaskini ni mbaya hasa ukiamia kwenye akili kias kwamb hata jiran yako akila nyama anamatumiz mabaya ya fedha " hiy dunia hata uwajengee kila mwananchi ghorofa lawama zipo palepale fanya unaloweza
 
Wanajimegea tu keki ya Taifa bila kujali umasikini wa wananchi wetu

20210414_161105.jpg
 
The problem tuu ni kwamba wanafanya mchana kweupe bila haya wala woga, they know hamwezi kufanya lolote. Mfano mechi ya jana. Ingekuwa JPM lazima papohapo angepiga simu laivu uwanjani na mechi ingechezwa saa kumi na moja kama ilivyopangwa. Huu ni ushamba na ulemavu wa akili uliokithiri.
Alikuwa anapenda sifa za ajabu zisizo na tija. Kazi iendeleee Sheria nzuri ziheshimiwe mbovu ziboreshwe

Sent from my vivo 1915 using JamiiForums mobile app
 
Ningependa kuona makasri ya wastaafu wote
Kweli kama sheria ilipita bungeni kelele zetu sijui zitasikika wapi labda mbinguni
moja wapo wa sheria mbaya sana katika nchi ii inabidi ibadilishwe haraka sana
haiwezekani mtu madaraka anayataka mwenyewe anaomba tumpigie kura
halafu eti anakaa wanajitungia masheria yakujinufaisha kupita kiasi
Kwani alipokuwa kiongozi alikuwa alipwi mshahara,
mbona wastaafu wenginge wa serikali wanalipwa mafao kiduchu sana utafikiriwa nao sio
binadamu
HII SHERIA YA MAFAO YA VIONGOZI WASTAAFU NI BATILI IBADITLISHWE KUPUNGUZA IDADI YA VIONGOZI NA KIASI CHA MAFAO WANACHOPATA
 

Barua ya wazi kwa rais mstaafu Kikwete.

Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu

Nakuandikia barua hii mimi kama raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuonesha kukasirishwa, kutopendezewa na kitendo cha serikali yetu kukujengea Jumba kubwa utadhani Kasri la Wafalme na wewe bila haya au aibu unalipokea kwa bashasha bila kujali kuwa nchi hii bado ni masikini sana na bado ina uhitaji mkubwa sana wa kila senti kwenda kuondoa umasikini wa kutisha wa watu wetu.

Ninafahamu kuwa mlijitungia sheria kuwa mstaafu akistaafu basi apewe pakeji nono ikiwemo kujengewa nyumba, licha ya kwamba hukuwa rais wakati sheria hiyo inatungwa, lakini ulikuwemo serikalini wakati inatungwa, baadae ukawa rais na hukuirekebisha hiyo sheria!, Na wala hujawahi kusikika popote kuonyesha kutofurahishwa na Mzigo mzito wa sisi wananchi kuwagharamieni nyinyi wastaafu kupitia kodi zetu.

Ndugu Jakaya Rais mstaafu, hebu niambie, wewe kama mtu uliyefanya kazi kwenye chama na serikali toka mwaka 1975 hadi mwaka 2015 ina maana hadi ulipostaafu, yaani jumla ya miaka 40 hukujenga nyumba yoyote?, ina maana miaka yote hiyo ulikuwa unapanga? —ina maana uliacha kujenga nyumba ukitatrajia kuwa one day utakuwa raisi siku moja ili ukistaafu ujengewe nyumba kwa kodi za wananchi?

Ndugu Jakaya Je nyumba yako ya Msoga haikutoshi? Unataka tena hilo hekalu ulipeleke wapi? Unataka umuachie urithi Ridhiwani?, umuachie urithi Miraji?, Umuachie urithi Mama Salma kupitia jasho la wananchi?

Nakuandikia barua hii nikitambua kuwa ulikuwa kijana wa TANU wewe, na nyie vijana wa kipindi hicho mlikuwa mkituaminisha kuwa mmeiva kwenye Itikadi za kukataa "unyonyaji",Najiuliza, kama mliweza kuwaaminisha wananchi kuwa siyo wanyonyaji na wakawaamini mpaka kuwapa nyadhifa kubwa huko mbeleni, mbona basi mnageuka wanyonyaji katika kustaafu kwenu?—Ina maana mikogo yenu ile ya kipindi hicho ya kujifanya siyo wapenda kujitajiridhisha kwa kutumia kivuli cha nyadhifa zenu ilikuwa feki?. Mnapata wapi usingizi wa kuenjoy mimali yote hii katikati ya lindi zito la umasikini wa watu wenu tena kwa kujitajirisha kupitia jasho lao?

Ndugu Jakaya, mimi sitaki kukueleza umasikini wa nchi hii kwa sababu unaujua, Umeujua ukiwa bado kijana na uliujua ukiwa mzee—Hebu tutazame sisi wananchi walalahoi machoni, ambao masilahi yetu tunaambiwa hatuwezi kupata kwanza kwa sababu uchumi wa nchi umeshuka, tuambie Jakaya hilo Hekalu lako ulilojengewa na Serikali uliyopambana sana kuiweka madarakani linatusaidiaje sisi wananchi kuondoa adha za ukosefu wa maji, Ukosefu wa madawa, ukosefu wa madawati, upungufu wa ajira kwa vijana wetu, nasilahi ya wakulina na wafanyakazi?

Ndugu Jakaya, wewe unalipwa asilimia 80 ya mshahara wa rais aliyeko madarakani, hivyo ndivyo nyie wanene mlivyojipangia, Unashindwaje kwa mshahara kujijengea nyumba nyingibe ukiihitaji mpaka serikali ikujengee Hekalu lote hilo kwa kodi za wananchi?

Najua unaweza kusingizia kuwa eti hivyo ndivyo sheria inavyotaka, lakini je kwani ungekataa kujengewa hilo hekalu ungelazimishwa?, Na kama ukilazimishwa kwani huwezi kulikataa?

Nakuandikia haya huku nikijua kuwa Rais Mkapa alijengewa Jumba lake, Mwinyi akajengewa Kasri lake na wewe leo umekabidhiwa Hekalu lako. Katika wote hao nimeamua nikuandikie wewe barua hii ya wazi kwa sababu Mzee Mkapa hatunaye, hawezi kujibu, Mzee Mwinyi ni mtu mzima sana, ni dhahiri anasukumiziwamo tu, Ila wewe bado una nguvu uko active na bila shaka unafuatilia kwa karibu sana yanayojiri nchi hii!

Kuna swali moja tu ningependa unijibu, JE TANU ILIWAFUNDISHA VIJANA WAKE MKIPATA MADARAKA AU KUSTAAFU MGEUKE WANYONYAJI?

Jakaya nakuomba kwa heshima na taadhima, wewe umeshiba, wenye njaa nchi hii ni wengi, wananchi wenye uhitaji wasioweza kumudu mahitaji yao ya msingi ni wengi, Hilo hekalu lako linaweza kujenga maelfu ya vyumba vya madarasa kusaidia watoto ambao wanafaulu darasa la saba lakini haweawezi kuendelea kutokana na upungufu wa madarasa nchini. Hilo hekalu lako ni zaidi ya Zahanati 50, Hilo hekalu lako ni zaidi ya madawati 5000.

Hebu niambie Jakaya mtu mwenye majumba, una familia yenye kipato kizuri, Unawezaje kukubali kuwa na Hekalu lote hilo kwa jasho la wananchi wenye uhitaji wa kila senti ya jasho lao?

Tafadhali rudisha hilo hekalu kwa wananchi liwasaidie, ukifanya hivyo utakuwa muungwana sana!

Sukuma gang kumbukeni kuwa hizi nyumba zimejengwa na mfalme juha
 
Back
Top Bottom