TANZIA Mzee Kavana (alishiriki Maasi ya 1964) afariki dunia!

TANZIA Mzee Kavana (alishiriki Maasi ya 1964) afariki dunia!

Mzee Kavana ameishi akiwa private tangu 1964 hadi hii August 2024.....hapo Changombe maduka 2....
 
Kuna taarifa hapo juu, kwamba alipandishwa cheo kuwa Meja siku hiyo ya maasi hapo Kambini Colito. Kambona alishinikizwa kufanya hivyo. Msome huyo "Mdosi Mzalendo", Kashmir, kaeleza kwenye simulizi yake, yeye akiwa ndani (mahabusu) siku hiyo.

..nadhani alipandishwa cheo kuwa Brigedia.

..nasema hivyo kwasababu Mzungu aliyekuwa akiongoza Tanganyika Rifles alikuwa na cheo cha Brigedia.

..haileti maana Waafrika waliokuwa wakidai vyeo jeshini wamuondoe Mzungu Brigedia, halafu wateue Muafrika kuwa na cheo cha chini cha Meja.

..Nimewahi kusoma kitabu cha maasi ya Tanganyika Rifles na Elisha Kavana hakuhusishwa na maasi hayo, zaidi ya hilo tukio la kupachikwa ukuu wa majeshi.

cc bagamoyo
 
Labda ni kwa vile marehemu hasemwi vibaya, ila kwa kuweka rekodi sawa nadhani ni sawa kuelezea jambo hili kwa jinsi lilivyokuwa, kwani ni sehemu ya historia ya hii nchi tuliyopo leo na vizazi vyetu.

Kiukweli, kwa namna hadi Luteni Elisha Kavana anapendekezwa kuwa kiongozi badala ya Askari wa Kizungu, tayari wote wasiounga mkono uasi ule walikuwa chini ya Ulinzi, na kubaki waliounga mkono.

Wakati Oscar Kambona amefikishwa kwenye kambi ya Colito, Kavana hakuwa chini ya ulinzi, na alikuwa miongoni mwa waliopiga yowe kumkataa Alex Nyirenda aliyetajwa awali kuwa kiongozi.

Hii ni tofauti na ilivyokuwa kwa Mrisho Sarakikya kwa kambi ya Tabora, ambaye aliteuliwa kuwa kiongozi huku akiwa mahabusu, kwani ilibidi atolewe mahabusu na kupewa taarifa, kisha akatoa amri ya kusitisha uasi.

Lakini, Kavana alitajwa jina lake kwa kupendekezwa huku mwenyewe akiwepo na kuvishwa kofia palepale na kushangiliwa, mbele ya Kambona ambaye wakati huo alikuwa ndiye Waziri wa Ulinzi.

Uamuzi uliompa uongozi Kavana ulifanywa na Kambona kwa shinikizo la Sgt. Ilogi na askari waliokuwako Colito wakati huo, akiwemo Kavana, wakimtisha kumpiga risasi Kambona asipotii matakwa yao.

RIP Mzee Elisha Kavana.

Ova
Sasa askari(offisa) mwenye historia kubwa namna hiyo mnashindwa kupata picha yake toka vyanzo mbali mbali vilivyopo?
 
Kweli hapa JamiiForums kijiwe kimejaa vizazi vya rika mbalimbali, hongera kwa JamiiForums kuwezesha hali hii ya mtandao kukusanya jamii pana ya watanzania.
Mkuu hilo ni kweli kabisa.
DSM miaka hiyo ni watu wachache sana
Wakati mwingine tunakaa kimya tu.
Huwezi amini lakini nimesoma pamoja na Jabsli la Muziki, Marijani Rajabu, 1971, Tambaza Sec.
 
Namkumbuka Temeke Lutheran Church. Atakuwa amefikisha over 80 years.
RIP Mzee Kavana.
Mzee Kavana mmoja wa wazee wa zamani kabisa Temeke Lutheran Church.
Kanisa la Temeke ndilo lilimokuwa wanasali viongozi wengi wa baadaye serikalini.
Hata wapigania uhuru wengi kama kina Chissano, aliyekuwa Rais wa Msumbiji, ambao walikuwa wanakaa Chang'ombe, walikuwa washarika hapo.
Baada ya Azania Front, kanisa la Temeke lilikuwa la pili kwa ukubwa hapa DSM.
 
Mzee Kavana, aliyekuwa Captain Kavana mwaka 1964 na aliyechagulia na askari wa Tanganyika Rifles walioasi ili awe kiongozi wao badala ya wazungu, amefariki jana 9/8/2024.

Captain Kavana wakati huo alikuwa hana hili wala lile huku askari waasi wakishinikiza kuwa kwa vile tumepata uhuru, lazima tuongozwe na muafrika, wakati huo kuna wimbi la Africanisation ya sehemu zote za ungozi nchini.

Hili lilimletea matatizo mzee Kavana maana hakuhusika na maasi wala kuwepo kuyapanga , lakini askari wa chini ndiyo walipenda waongozwe na askari Ofisa mzalendo badala ya wazungu.

Mzee Kavana ameishi kwa utulivu na amani nyumbani kwake Chang'ombe miaka yote.

RIP Mzee Kavana
RIP Kamanda
 
..Nimewahi kusoma kitabu cha maasi ya Tanganyika Rifles na Elisha Kavana hakuhusishwa na maasi hayo, zaidi ya hilo tukio la kupachikwa ukuu wa majeshi.
Kwa faida ya wengi hapa unge kitaja hicho kitabu.

Lakini hicho cheo cha 'Major', aliyo eleza mjeshi Kashmiri hapo juu, bandiko#38, inaeleweka vizuri. Huyu hakuendelea kuwa jeshini baada ya hayo maasi.
 
Mzee Kavana mmoja wa wazee wa zamani kabisa Temeke Lutheran Church.
Kanisa la Temeke ndilo lilimokuwa wanasali viongozi wengi wa baadaye serikalini.
Hata wapigania uhuru wengi kama kina Chissano, aliyekuwa Rais wa Msumbiji, ambao walikuwa wanakaa Chang'ombe, walikuwa washarika hapo.
Baada ya Azania Front, kanisa la Temeke lilikuwa la pili kwa ukubwa hapa DSM.
True, nilipata kipaimara hapo. Bonge la usharika.
Una uhusiano na yule Mzee brigadier wa JKT?
 
Mzee Kavana ameishi akiwa private tangu 1964 hadi hii August 2024.....hapo Changombe maduka 2....
Alijihusisha na biashara au alipata ajira kuendeshea maisha baada ya jeshi?

Hatma (fate) ya maisha ya mtu ni ya kipekee sana. Huyu na elimu yake hiyo wakati kama huo ungefikiri dunia ilikuwa inamsubiri tu kutengeneza maisha yake zaidi ya hapo alipo ishia. Tukio la muda mfupi tu linaweza kubadili mwelekeo mzima wa maisha.
 
Kwa faida ya wengi hapa unge kitaja hicho kitabu.

Lakini hicho cheo cha 'Major', aliyo eleza mjeshi Kashmiri hapo juu, bandiko#38, inaeleweka vizuri. Huyu hakuendelea kuwa jeshini baada ya hayo maasi.

..Kavana alifikaje kuwa Major ukizingatia wakati wa maasi alikuwa Lieutenant?

..ndio maana nasema aliondoka jeshini wakati wa Tpdf, na sio wakati wa Tanganyika Rifles.

..wakati wa maasi the highest ranking native officer was Captain Mirisho Sarakikya.
 
..kusema Elisha Kava alishiriki maasi ni kumchafua marehemu.

..walioshiriki maasi ya 1964, kwa mfano, Sajent Hingo Ilogi, walishtakiwa na kuhukumiwa.
Tena nasikia huyo Sgt Ilogi alienda hadi ikulu kumsaka Nyerere, lakina akakuta wanausalama wameshamkimbiza mafichoni.
 
..wakati wa maasi the highest ranking native officer was Captain Mirisho Sarakikya.
Kufuatana na taarifa ya Kashmiri, hicho cheo cha 'meja' alichopewa hakikuwa 'formal'. Hivi ni vyeo alivyo shinikizwa Kambona avitunuku wakati huo wa maasi. Kashmiri, anasema Kambona alipandishwa juu ya meza kutangaza hivyo vyeo kwa maofisa walio kuwepo kwenye tukio hilo kwenye kambi ya'Colito'.
Sarakikya hakuwepo kwenye tukio hilo, yeye alikuwa Tabora.
 
Mzee Kavana, aliyekuwa Captain Kavana mwaka 1964 na aliyechagulia na askari wa Tanganyika Rifles walioasi ili awe kiongozi wao badala ya wazungu, amefariki jana 9/8/2024.

Captain Kavana wakati huo alikuwa hana hili wala lile huku askari waasi wakishinikiza kuwa kwa vile tumepata uhuru, lazima tuongozwe na muafrika, wakati huo kuna wimbi la Africanisation ya sehemu zote za ungozi nchini.

Hili lilimletea matatizo mzee Kavana maana hakuhusika na maasi wala kuwepo kuyapanga , lakini askari wa chini ndiyo walipenda waongozwe na askari Ofisa mzalendo badala ya wazungu.

Mzee Kavana ameishi kwa utulivu na amani nyumbani kwake Chang'ombe miaka yote.

RIP Mzee Kavana
Rip captain Kavana
 
Sasa askari(offisa) mwenye historia kubwa namna hiyo mnashindwa kupata picha yake toka vyanzo mbali mbali vilivyopo?
Kwani niliagizwa nilete picha yake? Nilijisikia kusema tu jambo kumhusu kwa ajili ya kuweka sawa historia ya nchi yetu.

Ova
 
Back
Top Bottom