Kufuatana na taarifa ya Kashmiri, hicho cheo cha 'meja' alichopewa hakikuwa 'formal'. Hivi ni vyeo alivyo shinikizwa Kambona avitunuku wakati huo wa maasi. Kashmiri, anasema Kambona alipandishwa juu ya meza kutangaza hivyo vyeo kwa maofisa walio kuwepo kwenye tukio hilo kwenye kambi ya'Colito'.
Sarakikya hakuwepo kwenye tukio hilo, yeye alikuwa Tabora.
..ngoja nianze mbali kidogo, nitakuomba uwe nami.
..Mkuu wa Tanganyika Rifles alikuwa mzungu Brigadier.Patrick Sholto Douglas.
..maasi ya Tanganyika Rifles yalifanywa na non commissioned officer waliokuwa wakidai mishahara, vyeo, na africanization jeshini.
..wakati wa maasi maofisa wote walikamatwa na kutupwa rumande. Maafisa wa Kizungu waliamriwa kurudi kwao Uingereza.
..zoezi la kumpata mkuu mpya wa Tanganyika Rifles lilianza na Alexander Nyirenda alikataliwa alipopendekezwa.
..baada ya hapo ndipo akapendekezwa Luteni Elisha Kavana. Taarifa zinasema alitolewa mahabusu na kupachikwa cheo cha Brigadier badala ya mzungu ambaye alikuwa hatakiwi.
..hata ukisoma vitabu vya historia vinaeleza kwamba Elisha Kavana alionekana kushtushwa na tukio hilo na alilazimishwa na askari waasi kuchukua wadhifa huo.
..maasi hayo yalikuja kuzimwa kwa msaada wa askari toka Uingereza. baada ya hapo Mwalimu Nyerere alivunja jeshi la Tanganyika Rifles, na akaunda jeshi jipya, Jeshi la Wananchi wa Tanzania.
..Mwalimu pia alimteua Kapten Mirisho Sarakikya kuwa Mkuu wa kwanza wa Jwtz akiwa na cheo cha Brigadier. Siku hizi cheo hicho kinaitwa Brigadier General.
..picha hiyo hapo chini inathibitisha kwamba Elisha Kavana alikuja kuwa Meja ktk Jwtz. Kumbuka kwamba wakati wa maasi Elisha Kavana alikuwa Luteni, na Mirisho Sarakikya alikuwa Kapten.