TANZIA Mzee Kavana (alishiriki Maasi ya 1964) afariki dunia!


..ngoja nianze mbali kidogo, nitakuomba uwe nami.

..Mkuu wa Tanganyika Rifles alikuwa mzungu Brigadier.Patrick Sholto Douglas.

..maasi ya Tanganyika Rifles yalifanywa na non commissioned officer waliokuwa wakidai mishahara, vyeo, na africanization jeshini.

..wakati wa maasi maofisa wote walikamatwa na kutupwa rumande. Maafisa wa Kizungu waliamriwa kurudi kwao Uingereza.

..zoezi la kumpata mkuu mpya wa Tanganyika Rifles lilianza na Alexander Nyirenda alikataliwa alipopendekezwa.

..baada ya hapo ndipo akapendekezwa Luteni Elisha Kavana. Taarifa zinasema alitolewa mahabusu na kupachikwa cheo cha Brigadier badala ya mzungu ambaye alikuwa hatakiwi.

..hata ukisoma vitabu vya historia vinaeleza kwamba Elisha Kavana alionekana kushtushwa na tukio hilo na alilazimishwa na askari waasi kuchukua wadhifa huo.

..maasi hayo yalikuja kuzimwa kwa msaada wa askari toka Uingereza. baada ya hapo Mwalimu Nyerere alivunja jeshi la Tanganyika Rifles, na akaunda jeshi jipya, Jeshi la Wananchi wa Tanzania.

..Mwalimu pia alimteua Kapten Mirisho Sarakikya kuwa Mkuu wa kwanza wa Jwtz akiwa na cheo cha Brigadier. Siku hizi cheo hicho kinaitwa Brigadier General.

..picha hiyo hapo chini inathibitisha kwamba Elisha Kavana alikuja kuwa Meja ktk Jwtz. Kumbuka kwamba wakati wa maasi Elisha Kavana alikuwa Luteni, na Mirisho Sarakikya alikuwa Kapten.

 
RIP Mzee Kavana.

Kama na yeye kaandika itakuwa vizuri sana. Hata kama kwa kuandika mambo yachapishwe baada ya yeye kufariki.

Hawa wazee wa 1964 mutiny wameishi kwa kujistukia sana Tanzania.
 
RIP Mzee Kavana.

Kama na yeye kaandika itakuwa vizuri sana. Jata kama kwa kuandika mambo yachapishwe baada ya yeye kufariki.

Hawa wazee wa 1964 mutiny wameishi kwa kujistukia sana Tanzania.
Ni kweli kujistukia kuliwaathiri sana. Hata Nyirenda aliamua kuachana na jeshi kabisa akaenda kuajiriwa na BP, nao wakampeleka Zambia kwenye tawi lao la huko.

Ova
 
Kavana alipandishwa na kuwa Meja na aliapishwa kuwa Naibu wa Sarakikya.

Ova
 
Nawafahamu watoto wake.....naamini alitafuta kazi mbadala.....maisha yakasonga....ingawa najua enzi zile alikuwa under ......muda mrefu sana......
 
Mkuu 'JokaKuu', mimi sijui lolote kuhusu mkasa huu, lakini nina 'interest' ya kutaka kujuwa.
'Version' unayo ieleza wewe, kidogo ni tofauti na hii hapo juu, iliyowekwa na mkuu 'Mdakuzi', (Bandiko #16); taarifa ambayo pia inafanana na ile ya yule Mdosi, ambayo nimekwisha kuelekeza kwake mara kadhaa.

Hizi picha mbili zinazo mwonyesha Mwalimu akikutana na hao makamanda wawili Sarakikya na Kavana, ni kama zilichukuliwa siku hiyo hiyo moja, tofauti tu ni kuwa picha moja wamevalia kofia na picha ya pili hawana kofia vichwani.
Sasa sijui kama hizi picha zilipigwa baada au kabla ya maasi!

Cc: JokaKuu.
 

..hizo ni picha baada ya maasi.

..ukisoma maelezo chini ya picha, Sarakikya, na Kavana, wanatambulishwa kama viongozi ktk jeshi jipya.

..Kielelezo cha pili ni collar ya uniform aliyovaa Mirisho Sarakikya.

..Collar hiyo inafanana na uniform za askari ngazi ya Kanali, Brigedia, kwenda juu.

..Kwasababu Sarakikya alikuwa ameteuliwa kuwa Mkuu wa majeshi na Brigedia ndio maana collar ya uniform yake ikawa tofauti na collar ya uniform ya Kavana.

..pia uniform ya Sarakikya kabla ya maasi isingekuwa na alama ktk collar kwasababu alikuwa na cheo cha Kapten.

..Hakuna mashaka kwamba picha ya Sarakikya na Kavana ni ya baada ya maasi.
 
Hao sasa ndio walikua Vijana jeuri wenye uthubutu, Sio hawa Vijana wa sasa hivi, kuna muda unakaa unawaza weee unajiuliza "sperms zilizotungisha mimba za hawa Vijana wa style hii zilikua zimekomaa kweli? Au zilikua fake maybe au zilikua zina shida gani?" Basi unaishia Tu kuumia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…