Mzee Kikwete akanusha kuwepo kwa Mawaziri wanaotafuta fedha na mikopo nje ya nchi kumg'oa Samia Uchaguzi 2025

Mzee Kikwete akanusha kuwepo kwa Mawaziri wanaotafuta fedha na mikopo nje ya nchi kumg'oa Samia Uchaguzi 2025

Hao mawaziri ni Mwigulu, January Makamba,Nape Nauye,iko wazi kabisa,sema Chalamila kagusa watoto pendwa,sidhani kama ataendelea kuwa RC tena,
Hii nchi msemakweli ni adui mkubwa wa walamba asali,naona Samia kapewa maelekezo na boss wake kikwete lililobaki ni utekelezaji wa kutengua Chalamila
Kumbeee! Hongera mwenzetu kwa kujua hili. Umesema lipo wazi lakini huwezi kuamini, wengine sisi hata hatujui.
 
Eh, kumbe ameagiza Chalamila achukuliwe hatua?!!!!! Hilo nilikuwa sijasikia, sijui alilisema pale au pembeni?
Hivi zaidi ya kutoa angalizo tu kidogo kuna jingine kalisema hadi unasema 'ameelekeza lawama nzito' kama vile alinena hayo kwa muda mreefu?!!!!
Kama hukusikiliza hotuba ya JK tafadhali usiwapotezee muda great thinkers wanaojadili matamshi ya Mstaafu Kikwete na hatma ya Chama cha Mapinduzi.. Chama hiki ni kikubwa
 
Swali rahisi sana la kuhoji.
Hivi Kikwete yeye ni nani katika CCM, Serikali na dunia hii mpaka ajue kama hao mawaziri wanaodaiwa kusaka pesa za kutaka urais kweli wapo au hawapo?
Tangu lini Kikwete akawa ndio kipimo cha hayo yote?

Kikwete akisema mawaziri hao wapo siwezi kushangaa (maana maoni ya namna hiyo yapo ndani ya wigo wa utashi wake), lakini akisema kwa uhakika hawapo hapo nitashangaa, maana hilo lipo zaidi ya uwezo wa yeye kuweza kujua mwenendo ya kila waziri.
 
Labda yeye mstaafu anavyo vyombo vya uchunguzi mahiri zaidi ?? Hapo Alichemsha kwa lugha ya mtaani halafu amesababisha yawepo maswali mengi yasiyo na majibu!! Ukichanganya na Maneno ya Mzee Makamba unapata wasiwasi kidogo ! Ndo maana wengine wakauliza je wanamtisha Mkuu ??!!!
Endapo JK analo jambo la kushauri alipeleke kwa utaratibu unaofahamika na Mama atalipokea kwa kuwa Mama yetu ni msikivu na mnyenyekevu tofauti na yeye JK ambaye wakati wa utawala wake aliwafukuza marais wastaafu Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi ili afanye maamuzi atakavyo.
 
Kama hukusikiliza hotuba ya JK tafadhali usiwapotezee muda great thinkers wanaojadili matamshi ya Mstaafu Kikwete na hatma ya Chama cha Mapinduzi.. Chama hiki ni kikubwa
Sawa kiongozi, Nanyamaza nawapisha great thinkers waendelee na huu ulozi. Kama hili linaloendelea humu ndo u-great thinker wenyewe, basi sijilaumu tena kwa kutokuwa great thinker. Dah!
 
Hii kitaalamu tunasema,"Sabuni ya mkaa haiwezi kusafisha kanzu nyeupe".
 
Sawa kiongozi, Nanyamaza nawapisha great thinkers waendelee na huu ulozi. Kama hili linaloendelea humu ndo u-great thinker wenyewe, basi sijilaumu tena kwa kutokuwa great thinker. Dah!
Rais Mstaafu Kikwete anamwambia Rais Samia kwamba kwenye utawala wake hakukubali upuuzi huo, Lakini watanzania wote tunakumbuka nchi alivyoitumbukiza kwenye matatizo mengi kama uendeshaji duni wa chama na Serikali mpaka ikafikia hatua hatua ya KUJIVUA GAMBA ili kuinusuru CCM, mikataba mibovu kama Richmond, IPTL, Bandari ya Bagamoyo na Escrow mbayo ilisababisha hasara kubwa kwa nchi yetu lakini pia tunakumbuka bandari ya Dar es Salaam JK alivyoikabidhi kwa GSM hadi kusababisha mfarakano mkubwa na wafanyabiashara hadi watu kumwagiwa tindikali. leo Mzee Kikwete anapata wapi kiburi cha kutamka hayo hadharani kwamba jkwenye utawala wake hakukubali upuuzi huo.
 
Na

Mama akijua hayo,anashukuru kimya kimya yale matokeo ya UNEC yalivyojipanga!!

Kipara wa 11 na Pena 9,madeluu 13 huko!

Hiyo imekata ngebe za mbio za kijiti kama zipo KWA wahusika wale!

Nashukuru kuwa ile kampeni ya kumng'oa katelephone pia ilibuma vilivyo!

KWA hiyo kazi ya 0101 imetukuka Sana na kutamalaki nchi kavu!

Ndio maana povu liliwatoka baada ya kuona ndani ya mboga mboga VIJANA wao hawakufua dafu wakadhani labda LOPOKO LA CHALAMILA limetia kinyesi kwenye supu ikanuka!
 
Kikwete ni mnafiki na mtu wa kuwashwawashwa toka enzi za Mzee Mwinyi.Ni naibu wazir wa kwanza kumchongea wazir wake Kighoma Malima.Huyu ni mtu hatari sana na wa kuogopwa sana.Yaan hana nia njema na hata na Samia.Ni mtu wa tamaa sana.Amepanda mpaka kuwa Rais kwa unafiki tu.Lowassa hana hamu nae.Na hana aibu
 
Kumbeee! Hongera mwenzetu kwa kujua hili. Umesema lipo wazi lakini huwezi kuamini, wengine sisi hata hatujui.
Je Mheshimiwa Mstaafu Jakaya Kikwete kwanini atumie nguvu kubwa kukanusha kuwepo kwa mawaziri wanao tafuta fedha na mikopo nje ya nchi kwa ajili ya kufanikisha uchaguzi wa mwaka 2025 na kumbwaga Rais aliyeko madarakani Mama yetu Samia Suluhu Hassan.

Kwa vyovyote vile mawaziri waliotajwa na Chalamila, Mzee Kikwete atakuwa anawajua kwa majina na wizara wanazoziongoza ni washirika wake katika kupanga njama za kumtoa Rais Samia 2025 ndio maana povu jingi likamtoka kuwatetea hadharani bila aibu.
 
Rais Samia Suluhu anafanya maamuzi ya serikali yake yeye mwenyewe na ndio maana aliahidi kuwa viongozi wote waliokinyume na yeye watachaniwa mkeka hivyo watanzania hatuna wasiwasi maana Tanzania ni salama na Samia
 
Eh, kumbe ameagiza Chalamila achukuliwe hatua?!!!!! Hilo nilikuwa sijasikia, sijui alilisema pale au pembeni?
Hivi zaidi ya kutoa angalizo tu kidogo kuna jingine kalisema hadi unasema 'ameelekeza lawama nzito' kama vile alinena hayo kwa muda mreefu?!!!!
Watanzania wengi wamezoea kupindisha maneno ili mradi tu kiongozi aonekane hayuko sahihi
 
Je Mheshimiwa Mstaafu Jakaya Kikwete kwanini atumie nguvu kubwa kukanusha kuwepo kwa mawaziri wanao tafuta fedha na mikopo nje ya nchi kwa ajili ya kufanikisha uchaguzi wa mwaka 2025 na kumbwaga Rais aliyeko madarakani Mama yetu Samia Suluhu Hassan.

Kwa vyovyote vile mawaziri waliotajwa na Chalamila, Mzee Kikwete atakuwa anawajua kwa majina na wizara wanazoziongoza ni washirika wake katika kupanga njama za kumtoa Rais Samia 2025 ndio maana povu jingi likamtoka kuwatetea hadharani bila aibu.
Kwahiyo msimamo wenu ni upi haswa?!!!!! Maana kila siku mnatuambia kuwa Rais sasa ni JK kwa kuwa Samia ni dada yake na amemfanya mshauri wake wa kwanza kwa kila jambo......mnawaita wala asali. Leo mnabadilisha stori, kuwa anataka kumpindua 2025 kupitia kina Nape, Mwigulu na Januari?!!!!! Wamegombana lini tena? Kisa nini?!!
Aiseee!! Kweli mi niko mbali mno na kuwa great thinker maana hata sielewielewi tu huku wenyewe mkijadili kwa mshawasha kweli.
 
Well, wastaafu wetu tunawaheshimu na kuwapenda ila mzee wetu JK mbona kama analazimisha kila mtu ajue kua “yeye ndio man of the show” ?

Tunajua ni mastermind wa siasa za Tz hasa kipindi hiki cha awamu hii but mambo mengine angeachia wahusika “wapambane” !
 
Watanzania wengi wamezoea kupindisha maneno ili mradi tu kiongozi aonekane hayuko sahihi
Kikwete amesema waiteni muwahoji kwenye chama hatua zinaanza baada ya kuhoji
Kwahiyo msimamo wenu ni upi haswa?!!!!! Maana kila siku mnatuambia kuwa Rais sasa ni JK kwa kuwa Samia ni dada yake na amemfanya mshauri wake wa kwanza kwa kila jambo......mnawaita wala asali. Leo mnabadilisha stori, kuwa anataka kumpindua 2025 kupitia kina Nape, Mwigulu na Januari?!!!!! Wamegombana lini tena? Kisa nini?!!
Aiseee!! Kweli mi niko mbali mno na kuwa great thinker maana hata sielewielewi tu huku wenyewe mkijadili kwa mshawasha kweli.
Ndio maana unaona maswali yamekuwa mengi kwanini atokwe povu kama wako kitu kimoja?
 
Back
Top Bottom