Mzee Kikwete aweka rekodi sawa, Uchumi wa Kati waliopanga na Mkapa ni wastani wa dola 3,000 kila Mtanzania

Johnny Sack

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2017
Posts
8,984
Reaction score
19,288
Kikwete naona kaweka sawa kuhusu hizi propaganda kuwa Magufuli kafikia uchumi wa Kati kabla ya muda uliopangwa.

Kikwete kaweka sawa kuwa Uchumi wa Kati uliopangwa ni dola 3,000 na sio hii 1080. Na kampa Magufuli challenge kuwa 2025 inatakiwa awe amefikia kipato hicho kwa kila mtanzania.

Pia kaweka rekodi nyingine sawa kuwa Uchumi kukua kwa asilimia 7 Ni Mkapa ndio aliweka na baada ya Mkapa haijawahi kushuka hiyo Kasi.

Pia soma > Benki ya Dunia yaitangaza Tanzania kuingia rasmi katika orodha ya Nchi zilizo katika uchumi wa kati

Hii ni tofauti na propaganda za Sasa hivi kuwa Magufuli ndio kapandisha Kasi ya ukuaji Uchumi.

 
MATAGA watamuona JK ni bonge la Snitch.

Amesema kazi ya Magu sasa ni kututoa hapa kwny kipato cha $1,080 na kufikia $3,000 by 2025 ili kufikia uchumi wa Kati.

Yaani kama tangu 2005 mpk 2020 wamepambana marais hatari ndio tumefikia $1080 sijui miujiza ya aina gani itafanyika ndani ya miaka 5 kufikisha $1,920 zingine.
 
Acha ramli chonganishi rais Magufuli alielezea vizuri tangu siku anarudisha form ya urais kuwa kazi ya kuipeleka nchi uchumi wa kati ilianzishwa na wa tangulizi wake. Kwenye timu ya mpira sifa anapewa mfungaji bora anayepokea pasi ya mwisho.
 
Acha ramli chonganishi rais Magufuli alielezea vizuri tangu siku anarudisha form ya urais kuwa kazi ya kuipeleka nchi uchumi wa kati ilianzishwa na wa tangulizi wake. Kwenye timu ya mpira sifa anapewa mfungaji bora anayepokea pasi ya mwisho.
Sio ramli chonganishi,
Zimekuwepo propaganda kuwa tumefikia Uchumi wa Kati kabla ya Muda Tena muda mwingine Kutoka kwa Magufuli mwenyewe, nikipata video nitakuwekea hapa
 
Hawezi! Hata kufanikisha ifike USD 1200 hatoweza kutokana na kukuru kakara zake!
 
Sio ramli chonganishi,
Zimekuwepo propaganda kuwa tumefikia Uchumi wa Kati kabla ya Muda Tena muda mwingine Kutoka kwa Magufuli mwenyewe, nikipata video nitakuwekea hapa
Yani Mpango na Magufuli tena wakahutubia taifa kabisa. Ukiwa muongo kwa vitu vinavyoonekana kuaminika kwa visivyoonekana ni ndoto ya mchana!
 
Kikwete ninampenda bure. Maana watanzania walijua kuwa wamefika pato la 3000 kabla ya 2025.

Watanzania vilaza ndio waliamini tumefikia kipato cha kati. Ila hata maelezo ya WB wamesema kabisa kuwa ni uchumi wa kati wa chini. Lakini hilo neno uchumi wa kati wa chini, linarukwa kimakusudi ili kuhadaa wajinga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…