Magufuli aliua nguvu ya wazee kwenye maamuzi ya chama. Nguvu ya wazee iliasisiwa na Nyerere. Kwankulitambua Hilo Magufuli akaamua kuwapunguza nguvu na kuwato katika sehemu ya maamuzi magumu ya chama. Akàanzisha kilichoitwa Baraza la ushauri ambalo halina meno. Kama mnavyojua ushauri ni ama ukubaliwe au ukataliwe. Baada ya kuwanyima nguvu akaanza kuwang'ong'a hadharani wazi wazi akijua hakuna WA kumfanya chilochote. Akaingiza kundi la wajinga na watumia nguvu kwenye chama kuliko hoja huku wakiimarisha ndoa Yao na vyombo vya Dola sambamba na mabadiliko lukuki ya Sheria za usalama na ulinzi!
Uadui miongoni mwa watanzania kwa misingi ya chama iliasisiwa na huyo na Wala hakiwezekani kupingwa. Kikwete alipeleka maendeleo kwa maeneo yalichagua upinzani kama njia ya wlkwashawishi wananchi wakuunge mkono na chama chake. Magufuli aliweka bayana kwamba hawezi na hatopeleka maendeleo Kwa watu wenye itikadi tofauti na chama chake. Alienda mbali kuwafananisha na magunzi na kutaka hadharani. Hii ilichochea na kurasimisha ukatili na uadui dhidi ya upinzani.